News Alert: Namtumbo, Tunduru: Jeshi la Polisi linawashikilia Viongozi wa ACT Wazalendo waliokuwa kwenye Kampeni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
966
1,000
Katibu wa ACT Wazalendo wa Mkoa wa Kichama wa Selou (Majimbo ya Namtumbo, Tunduru Kusini na Kaskazini) Ndugu Abdallah Mtutura na viongozi wengine wapatao 10 wa Kata ya Ligoma (Tunduru Kusini) wanashikiliwa na Polisi baada ya vurugu zilizosababishwa na CCM kuingilia ratiba ya Mkutano wa ACT Wazalendo katika kijiji cha Msinji.

Hadi sasa, Jeshi la Polisi Tunduru halijamkamata hata mfuasi mmoja wa CCM ambao kimsingi ndio waliosababisha vurugu. Kamatakamata ya viongozi wa ACT Wazalendo inafanywa na Jeshi la Polisi kuibeba CCM ambayo ni wazi kuwa imezidiwa kupita kiasi katika Kata ya Ligoma Jimbo la Tunduru Kusini.

Kata ya Ligoma, Jimbo la Tunduru Kusini inategemewa kufanya uchaguzi wa marudio Tarehe 16 Mei 2021
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom