Namtilia shaka Mwanasheria mkuu wangu wa Serikali yangu.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namtilia shaka Mwanasheria mkuu wangu wa Serikali yangu..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Moseley, Dec 29, 2010.

 1. Moseley

  Moseley Senior Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Maelezo au maoni ya watu mbalimbali na wanazuoni kuhusu sakata hii wanaweka msimamo kumpinga Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Lakini, lipo tatizo nadhani inawezekana ni la msingi. Mara mbili sasa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametofautiana na Waziri Mkuu (ambaye naye ni mwanasheria kitaaluma).

  Kuhusu Katiba, Waziri Mkuu ameahidi kumshauri Rais walifanyie kazi. Jaji Werema amesema Katiba itawekewa viraka tu, maoni ya kuwa na Katiba Mpya yeye inaonekana hayaoni.

  Kuhusu sakata la Dowans, Waziri Mkuu amesema wataliangalia kuona namna ya kukata rufaa. Jaji Werema anasema, hapana, TANESCO watalipa, mjadala umefungwa!!

  Tutatifika 2015 kweli!? Tukifika historia itakuwa imeandikwa!.
   
 2. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Serikali ya jk imekuwa kama genge la walevi ambalo kila mmoja anataka kuzungumza,hatimaye ni kelele na vurugu kwani haingii akilini kuona kila member wa serikali anakuja na kauli yake tena kwa ishu moja.Sasa haijulikani nani mkubwa,nani anaepaswa kutoa kauli ya serikali yaani ni vurugu tupu.Suala la dowans PM anasema wataangalia namna ya kukata rufaa,AG yeye anaufunga mjadala,huku jk mwenyewe yuko kimya kama hayamuhusu vile,si wehu huu.Mi naamini kwa sasa hatuna serikali,tuna kikundi cha majangili tu wanaogombea raslimali za nchi hii basi.
   
 3. k

  kituro Senior Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  pole sana lakini ndiye aliyepewa rungu! hata kama ni kichaa!
   
 4. k

  kituro Senior Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kuhusu kodi zetu kuwapa dowans ni kutudharau kwakuwa sisi wenyewe watoto wetu wanasoma shule ambazo wenyewe sidhani kama wanazitambua kama ni shule hazina vifaa vya kujifunzia. tunawaomba kama kunapesa za kuwapa hao majambazi basi muwaongezee mishahara wafanyakazi ili nasi wafanyiwa kazi tuweze kuhudumiwa vizuri!.
   
 5. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani Werema ana interest na Dowans au anatumika tu kisiasa kulinda maslahi ya waliyomuweka na hana kabisa professional ethics. Kila mara anatoa controversial statements na inanipa wasiwasi hata huo Ujaji wake kama alipewa kwa kustahili au alibebwa tu. Kwa nafasi yake si msemaji wa serikali bali ni mshauri mkuu wa serikali kuhusu sheria, kwahiyo kauli ya kusema mjadala kuhusu dowans umefungwa hakustahili kutoa yeye, labda waziri mkuu au rais mwenyewe. Werema kama anataka siasa aingie badala ya kila kukicha kutoa kauli tata zenye sura ya kisiasa wakati yeye ni mtaalam na tunategemea atoe ushauri wa kitaalam kwa serikali na jamii ya watanzania kwa ujumla
   
Loading...