Namtafutia mchumba mdogo wangu wa miaka 22

We kaka vipi? Ndio sasa wachumba wote kawakataa, kawaona hawamfai, umenipata hapo? mbona wagumu kuelewa nyie? Je kwani mtu hauwezi kukataa hiki kama haukitaki na ukatafuta kingine? Mbona nyie waswaili wengine hamna kitu kuelewa kichwani mwenu. Yaani kumuunderstand kwanini kakataa hiki na anataka kingineiiii. sawa????????Hata nguo unaweza kuziacha hizi ukaenda kununua zile, ni upendeleo wa mtu. Hapo sasa kama akili zako timamu utaelewa bila kuelezwa kama, hizi hakuzitaka anazitaka zile. Labda nyie wanaume hamchagui mnachukua mnachokipata, au sio? Mchumba akitokea yeyote ule, mnazoa tu ka? mnachekesha sana. Au nyie wanaume ubongo wenu mgumu kuelewa?
Vile vile elewa mdogo wangu hajaniambia nimsaidie kutafuta mchumba, hapa naona wewe mwenyewe umechanganya mambo. Yeye kaniambia tu nimsaidie kimaisha, ila mie ndio nimefikiria labda ni bora tu aolewe, maana mie siwezi kumsaidia daima. Sababu hata mie nilipo ona maisha siyawezi peke yangu nikamua kuolewa ili nisaidiane kimawazo na mwenzangu. Uislam ukuwadi ndio jadi yetu,, sio uislam tu hata wazazi utafutia watoto wao wachumba hivi ulikuwa haujui eh? mbona watu wengi tu wanaolewa ki hivi na wanadumu daima, we kaka vipi umechanganyikiwa? wa wapi wewe?

Kwani wewe wa wapi??? Nadhani wewe ndo UMECHANGANYIKIWA kuleta mdogo wako hapa umtafutie mchumba . . . kama ubongo wa wanaume mgumu kuelewa ungesema unamtafutia mwanaume?? Wewe si ndo unamleta hapa mdogo wako azoe yeyote tu?!! Angalia . . .
 
Kwa nini usimchukue ukamuendeleza kielimu kwanza huko kisha akajitafutia mwenyewe mchumba kama atataka?

Miaka 22 ni mtu mzima na anatakiwa aweze kujiamulia mambo yake au hataweza hata huko kwa mume
Kwa maelezo yake wala sishauri amchukue huyo binti, anaweza mgeuza mtaji. Sikuwa nikijua kama kuna wanawake wenye akili mgando kiasi hicho mpaka leo. Hivi anadhani huyo mdogo wake ni mlemavu wa akili hata aweze kukataa hao wanaume wengine? Na je alimwambia amtafutie mume? Tena hata Mama yake tayari hamwamini. Eti anashindwa kumfungulia hata salon!!! kweli unaishi huko ulipo na kumpa ndugu yako mtaji wa salon ni tabu, school fees utaweza? Mshauri aje kwangu anitunzie watot nitamsaidia kuliko wewe.
 
mambo ya kutafutiana wachumba na baadae je kukulaumu wewe mmh pole haya mambo ya isingekuwa dada yote haya yasingenipata.
Kwani yeye hawezi kuwa na maamuzi binafsi miaka 22?:hungry:
 
Pengine alitegemea alimleta hapa ndo atapata soko kwa wingi . . . yaani hajui anachofanya kinaweza kutafsiliwa kama kumuuza mtu, hasa anaposema "Yeye kaniambia tu nimsaidie kimaisha, ila mie ndio nimefikiria labda ni bora tu aolewe" Yaan kwa akili yake anaamini njia moja wapo kumsaidia mdogo wake ni kumtafutia mwanaume ????!!!! Na hapo ktk kauli yake utagundua hata mhusika mwenyewe hajui kama anatafutiwa mwanaume????!!!!
 
mambo ya kutafutiana wachumba na baadae je kukulaumu wewe mmh pole haya mambo ya isingekuwa dada yote haya yasingenipata.
Kwani yeye hawezi kuwa na maamuzi binafsi miaka 22?:hungry:

First Lady . . .! Mimi ni mwanaume, na ninawapenda sana nyie wanawake kuliko hata ninavyowapenda wanaume wenzangu. Hii ni kutokana na mateso niliyojionea LIVE ya wanawake kudundwa dundwa mpaka makovu usoni na wanaume. Na moja ya vyanzo vya kudundwa huko mwanzo wake ni kama thread hii inavyoelezea. Jose Chamelion ameimba "Jamila", Taasisi na makundi mbalimbali ya haki za binadamu yanajitahidi kuelimisha, lakin bado unakuta kuna mtu anakuja na kudai ANAMSAIDIA MTU KIMAISHA, TENA MDOGO WAKE WA DAMU ETI KWA KUMTAFUTIA MWANAUME???? Mimi huwa machozi yananitoka kwa kweli, mpaka najishangaa! Umeshawahi kuangalia filamu ya A GOOD MAN IS HARD TO FIND au WHY DID I GET MARRIED?? . . . hizo movies zimenitoa machozi balaa
 
Kwani wewe wa wapi??? Nadhani wewe ndo UMECHANGANYIKIWA kuleta mdogo wako hapa umtafutie mchumba . . . kama ubongo wa wanaume mgumu kuelewa ungesema unamtafutia mwanaume?? Wewe si ndo unamleta hapa mdogo wako azoe yeyote tu?!! Angalia . . .

Kwani humu ndani hawezi kuchagua. Unazani watu wote humu ndani akili zao kama zako za kuunga unga?
 
Nazani akiolewa atashauriwa na mumewe wafanyaje maishani. Mie nimemshauri asome anasema hawezi, kuna wasichana wengine walio lelewa mazingira ya kuolewa, shule hawaioni muhim sister. Na akipata matatizo ktk ndoa mtamsaidia, sito muhacha motoni aise

Hebu tuwasiliane mm naweza kuwa msaada mkubwa sana kwa mdogo wako
 
Pengine alitegemea alimleta hapa ndo atapata soko kwa wingi . . . yaani hajui anachofanya kinaweza kutafsiliwa kama kumuuza mtu, hasa anaposema "Yeye kaniambia tu nimsaidie kimaisha, ila mie ndio nimefikiria labda ni bora tu aolewe" Yaan kwa akili yake anaamini njia moja wapo kumsaidia mdogo wake ni kumtafutia mwanaume ????!!!! Na hapo ktk kauli yake utagundua hata mhusika mwenyewe hajui kama anatafutiwa mwanaume????!!!!

Ndio hivo hivo, sasa wewe inakumaa kitu gani? Ukijua unachokifanya wewe mwenyewe maishani mwako inatosha. Hurumia dada zako wanao pigwa uko na kunyanya sika, ila yawenzio yavue na yaache kama yalivo, hayakuhusu..
 
Kwa maelezo yake wala sishauri amchukue huyo binti, anaweza mgeuza mtaji. Sikuwa nikijua kama kuna wanawake wenye akili mgando kiasi hicho mpaka leo. Hivi anadhani huyo mdogo wake ni mlemavu wa akili hata aweze kukataa hao wanaume wengine? Na je alimwambia amtafutie mume? Tena hata Mama yake tayari hamwamini. Eti anashindwa kumfungulia hata salon!!! kweli unaishi huko ulipo na kumpa ndugu yako mtaji wa salon ni tabu, school fees utaweza? Mshauri aje kwangu anitunzie watot nitamsaidia kuliko wewe.

Mie nazani wewe mwenyewe ndio mlemavu wa akili. Na wewe mwenyewe ndio una fikra za kugeuza watu mitaji. Maana hata hauelewi inavo onesha, kwani nimesema siwezi kumpa mtaji wa salon? Au nimesema siwezi kumlipia shule?
 
Mtafutie shule nduguyo...mchumba atajitafutia mwenyewe muda muafaka ukifika...
 
Back
Top Bottom