Namtafutia mchumba mdogo wangu wa miaka 22 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namtafutia mchumba mdogo wangu wa miaka 22

Discussion in 'Love Connect' started by Somoe, Dec 18, 2010.

 1. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Habari za maisha walimwengu.

  Mie ni dada nimeolewa, na nina watoto. Nina swali. Nina mdogo wangu wa miaka 22, ninahisi ni bikra, ila sina uhakika. Kazi yake ni kupika tu home kwa mama. Wachumba wote waliotokea kawakataa.Kaniambia hataki kuolewa, anaogopa HIV. Kaniambia nikamchukue aje kuishi nami Ulaya, mie naweza kwenda kumchukua kama au pair lakini namuogopa mama kunikatalia.

  Anasema hapa Ulaya ni ufataki tu, na ushenzi, aasije mwanae kuharibika. Nimefikiria kumtafutia mchumba, sasa sijui nimtafutie wa kizungu? Maana waislam wa iswaili kupatikana ulaya sio raisi nafikiri. Siwezi hata kumfungulia salon Tz, au biashara zingine maana mama hataki mwanawe anze biashara haram anasema.

  Naombeni ushauri nifanyeje kwa hili, nae kaniomba nimsaidie
   
 2. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tuanze kwanza kwa kujibu maswali haya kabla sijatoa ushauri:

  1. Hapo kwenye red: kwani mama mpaka aseme hivyo wewe umeharibika kwa kuja ulaya?

  2. Au mama kaona uwepo wako ulaya hauna manufaa yoyote?

  3. Huyo mdogo wako ameenda shule kidogo?

  4. Akija ulaya unaweza kumwendeleza kimasomo?

  Pamoja na kujibu maswali haya, kwa kuanzia mie nafikiri ni vema ukafikiria kumjengea uwezo mdogo wako kuliko kufikiri kumtafutia mume. Miaka 22 bado mdogo, anaweza kuendelezwa hasa kielimu na hata baadae akiolewa na huyo mzungu unayemfikiria hata nyanyasika sana. Wakina dada wengi wanaoolewa ulaya wakiwa hawana mbele wala nyuma huwa wanaishia kuwa watumwa wa ngono.
   
 3. Attinda78

  Attinda78 Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi natafuta mchumba lakini awe muislamu mwenye itikadi kali kama mimi, ila naona 22 ni mdogo, lakini inategemea how mature someone is kiakili so lets communicate. :eek:,

  ila mahari bana isiwe kuuuubwa,:bump: na harusi ya kiislamu hakuna mdundiko wala muziki.
   
 4. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo we dada yangu umeona kumtafutia mchumba mdogo wako ndo solution? Pengine alivyowakataa hao wachumba anaona umri bado mdogo, after all kumtafutia mtu mchumba kumepitwa na wakati ilikuwa ni enzi zile za mwalimu, unaweza kumpata huyo mchumba lakini wakijapata matatizo maishani mwao utalaumiwa milele, mdogo wako atakuwa akisema isingekuwa dada nisingeolewa na huyu mwanamume na kinyume chake! Nakushauri mwendeleze mdogo wako awe na kitu cha kufanya, hata shule au kozi waweza kumpeleka akapata ujuzi!

  napenda kuuliza huyo mdogo wako ana elimu gani?
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kwa nini usimchukue ukamuendeleza kielimu kwanza huko kisha akajitafutia mwenyewe mchumba kama atataka?

  Miaka 22 ni mtu mzima na anatakiwa aweze kujiamulia mambo yake au hataweza hata huko kwa mume
   
 6. Baiskeli

  Baiskeli JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  naomba aolewe na kaka yangu. yeye ni mwanadini mzuri. itakuwa vzuri kama utaweka picha yake.
   
 7. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  duuuhhh kwakweli
  sasa si unaweza kumtafutia mchumba halafu mama akatae ??/
  maana kila kitu hapo juu ni mama hataki ...
  kwanini huyo binti asichague anataka nini maishai mwake ?
  mama amsaidie tu kimawazo na pale anapohitaji msaada zaidi..
  lakini huyo bint aa make her own decision...
  coz at the end of the day this is her life...
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  We somoe, huyo ndio yule mdogo wako uliyesema mtukutu unamtaftia shule ya boarding leo unamtaftia mchumba!
  Hebu jifikirie mara mbili mbili.
   
 9. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Deodat,

  1) Mie sijaribika. Ila hata mimi nilipokuwa nakuja ulaya mama alikuwa na wasiwasi pia. Ila amefurahi aliponiona nipo wa kawaida kama zamani sijambadilika kuja ulaya.

  2) Ana mafanikio sana tu, na anamshukuru Mungu.

  3) Hajaenda shule na hapendi shule

  4) Labda akija ulaya anaweza kujiona mpumbavu na kujiendeleza kimasomo. Mbona wengi tu wameolewa wakiwa na miaka 19 tu, sasa miaka 22 kuna tatizo gani? Kama hataki kujiendeleza kwa sasa mtu utafanyaje? Labda akishaolewa na kuzaa ndio ataona school ni muhim maishani, na ataanza shule upya..
   
 10. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Sie, yule sie wa kuolewa kabisa, angepiga mume wenyewe mashuti.... yule anapenda shule na ugomvi tu sio ndoa:redfaces:
   
 11. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Nazani akiolewa atashauriwa na mumewe wafanyaje maishani. Mie nimemshauri asome anasema hawezi, kuna wasichana wengine walio lelewa mazingira ya kuolewa, shule hawaioni muhim sister. Na akipata matatizo ktk ndoa mtamsaidia, sito muhacha motoni aise
   
 12. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Mahari sio issue, muhim wewe tu udumu nae maishani. Yeye katoka kwenye uislam haswa, ila hapendi wazee, kwaiyo usizidi miaka 30. Akili kichwani zimo za kumpikia mumewe na kulea watoto. Na ni mpole sana, unaweza kumuonea akaka kimya anameza mate tu,, wajanja na wauni hatowezana nao kabisa. Inabidi awe na mume mpole kama yeye mwenyewe
   
 13. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mie naona, kama hataki shule kuna kazi za mikono kama kushona na mambo ya uzuri na mengine mengi, ambayo yatamsaidia kujitegemea but kuolewa at that age sio solution
   
 14. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa maelezo yanakwenda yana rudi. Wachumba wote kawakataa, hataki kuolewa, halafu tena unasema umtafutie mchumba????? Sounds weird!!!! Kama hajaitunda hii habari basi kaitoa sehemu kaileta hapa, na kakosea kujieleza. UTAMTAFUTIAJE MCHUMBA MTU AMBAYE AMESHAKATAA HATAKI?? AU UNATAKA KUMLAZIMISHA KWA MABAVU???? Eti hapendi kabisa shule, na wala hajawahi kusoma??? Mtu gani sasa huyo??

  Halafu unadai umfungulie biashara ????? Hata biashara ya karanga itahitaji mtu ajue kusoma na kuandika ili apige hesabu na kuandika kumbukumbu za biashara vizuri, sasa huyo kilaza ataanzaje???? Na ukaona dawa ni kumtafutia mwanaume wa kumshughulikia??? Kweli unampenda mdogo ako wewe??? Huoni hata aibu kuwa kuwadi wa mdogo wako?? Au unamtafutia dume la kumpachika mimba???

  Mi naona hii imetungwa tu, maelezo yake hayaonyeshi kama ni kitu halisi.
   
 15. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  We kaka vipi? Ndio sasa wachumba wote kawakataa, kawaona hawamfai, umenipata hapo? mbona wagumu kuelewa nyie? Je kwani mtu hauwezi kukataa hiki kama haukitaki na ukatafuta kingine? Mbona nyie waswaili wengine hamna kitu kuelewa kichwani mwenu.

  Yaani kumuunderstand kwanini kakataa hiki na anataka kingineiiii. sawa???? Hata nguo unaweza kuziacha hizi ukaenda kununua zile, ni upendeleo wa mtu.

  Hapo sasa kama akili zako timamu utaelewa bila kuelezwa kama, hizi hakuzitaka anazitaka zile. Labda nyie wanaume hamchagui mnachukua mnachokipata, au sio? Mchumba akitokea yeyote ule, mnazoa tu ka? mnachekesha sana. Au nyie wanaume ubongo wenu mgumu kuelewa?

  Vile vile elewa mdogo wangu hajaniambia nimsaidie kutafuta mchumba, hapa naona wewe mwenyewe umechanganya mambo. Yeye kaniambia tu nimsaidie kimaisha, ila mie ndio nimefikiria labda ni bora tu aolewe, maana mie siwezi kumsaidia daima. Sababu hata mie nilipo ona maisha siyawezi peke yangu nikamua kuolewa ili nisaidiane kimawazo na mwenzangu.

  Uislam ukuwadi ndio jadi yetu,, sio uislam tu hata wazazi utafutia watoto wao wachumba hivi ulikuwa haujui eh? mbona watu wengi tu wanaolewa ki hivi na wanadumu daima.
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo anataka/unataka aolewe ili apewe maisha??Kwenye ulimwengu huu wa sasa??Kaaazi kweli kweli!
   
 17. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #17
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Juu ya elimu, naona wewe kaka haujui na wala haujaelimika kimaisha. Mie mwenyewe binafsi mimemaliza chuo kikuu. Na nina majamaa wengi tu walishia darasa la tatu, walikimbia mtiani wa darasa la nne, na sasa ni matajiri sana, we kaka vipi? unazani kusoma ndio kuwa na juhudi au kuongezeka akili? hahahha, ebu mi nicheke kwanza. Na nina marafiki kibao wamemaliza chuo mpaka PHD wapo wapo tu hawana A wala B. Eti hata biashara ya karanga inaitaji ajue kusoma na kuandika, mwee? Mie niliona wauza karanga wengi hawajui kusoma na wala kuandika ila kumbukumbu walikuwa nazo,,,
   
 18. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #18
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Yes, sababu mungu kaumba kike na kiume, ili wapeane maisha. Sio apewe tu na atoe maisha pia. Kwani ulimwengu huu unanini?
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sio wakutegemea ni wa kutegemeana!!
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli kweli ila somoe jitahidi labda utafanikiwa kumpata huyo mwanaume kwa ajili ya mdogo wako
   
Loading...