Namtafuta dada yangu toka nchini Uganda.

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
Tafadhali sana naombeni msaada wenu wa jinsi gani au nifanyeje
namtafuta dada yangu anaitwa
Ghati Josephati Magoiga,sijawahi onana nae
tuliambiwa na baba kuwa tuna
dada yetu anaishi Nchini Uganda alizaliwa
mnamo mwaka 1982 nyumbani kwao
alipozaliwa panaitwa Bujiku.Sikuweza kusikia
mimi ila niliambiwa mwaka 2007
aliwahi kutoa taarifa redio free africa kuwa
anamtafuta baba yake ambaye ambaye anaitwa Josephat Magoiga alikuwa mwanajeshi toka Tanzania alishiriki vita ya kumng'oa Iddi Amini ambaye
hajawahi kumuona maana aliondoka
Uganda tokea kipindi cha vita vya Kagera mama mama
yake aliachwa akiwa na
ujauzito wake na alipozaliwa tu mwaka 1982
mama yake alimtumia baba barua
ya kumtaka ampatie jina la kumuita mtoto huyo
aliyezaliwa na baba aliijibu
barua kwa kumtumia jina kuwa aitwe Ghati
Josephati tokea hapo walipotezana mawasiliano hadi hivi sasa,tokea alipotoa taarifa ile mwaka 2007 kupitia RFA kuwa anamtafuta baba yake.
alijitambulisha kuwa anafanya kazi kwenye
ubalozi wa Sweden nchini Uganda.Kwa bahati mbaya mimi binafsi sikuipata taarifa hiyo redioni ila niliambiwa na baba ambaye nae aliambiwa kuwa anatafutwa.Sasa sijui hata nianzie wapi naombeni mwongozo wenu.
 
Nami namtafuta Arafati Tengeneza.
Mara ya mwisho tumeachana nilipokwenda kumsalimu ChiboSeco (Chidya Boys Sec School-Masasi.)

Hayuko Facebook wala wapi.
 
Sasa kama yupo ubalozi wa sweden uganda si hatua ya kwanza ukaulize au uwatumie mail ubalozi kuulizia mkuu??
 
Sasa kama yupo ubalozi wa sweden uganda si hatua ya kwanza ukaulize au uwatumie mail ubalozi kuulizia mkuu??

Nimekwishaituma email leo,ila hofu yangu kubwa ni yawezakuwa pale ubalozini huenda hajalitumia jina hilo alilolitoa baba pia najitahidi kutafuta mawasiliano ya redio free africa hasa kipindi kile cha kutafutana ili kama watakuwa na kumbukumbu zake atakazokuwa aliziacha ila bado sijafanikiwa.Kwa yeyote atakayekuwa na mawasiliano ya redio free kwenye kipindi cha kutafutana anisaidie.
 
unajua ubaloz wakipata email wata punch notboard so hata kama hajatmia jna ilo atajijua thn wil chk u back.utampata tu
 
unajua ubaloz wakipata email wata punch notsboard so hata kama hajatmia jna ilo atajijua thn wil chk u back.utampata tu
 
ndugu mtafuta ndugu... kama kwenye mitandao ya kijamii haipo, na kama mlipata picha yake au chochote kinachowaunganisha ninyi na nduguyenu wa Uganda pengine mngefanya utafiti wa kijiji au mji alipokuwa akiishi mama mama huyo alipokutana na baba yako and then mfuatilie..hii ina maana kutoa muda kabisa wa kusafiri kwenda huko au Kuandika tangazo kwenye magazeti yanayosomwa kwenye eneo mnalodhani huyo ndugu yenu yupo.. kwa juhudi hizi mnaweza kupata dodoso zitakazopelekea kkutana na ndudu yenu. Kila la heri.. Mimi nilimpata motto wa kaka yangu kwenye facebook na ilikuwa ni bahati kwa sababu pamoja na majina lakini inmachukua uaminifu mpaka mtu ulipepotezana naye kuamini kwamba "wewe ndio ndugu na si tapeli" .. Kila la heri na endelea kutujuza hapa jamvini.
 
Asante
 
Back
Top Bottom