Namtafuta baba yangu mzazi mzee Jovin Machumu

mkata-mkaa

JF-Expert Member
Nov 16, 2016
296
181
Wakuu habari zenu,

Namtafuta mzee wangu. Mama na mzee waligombana kipindi mimi nazaliwa kwa hiyo mzee aliondoka na mama akakata kabisa mawasiliano naye.

Ni miaka zaidi ya 25 imepita, mimi simfahamu mzee hata kwa picha, baada ya mahojiano na mama akanipa maelezo yafuatayo
- Jina lake ni Jovin Machumu
-Mara ya mwisho mama alisikia anaishi Shinyanga na alikuwa anafanya kazi Tanzania National Miling
-kabila lake ni Muhaya
- Hawafahamu kabisa ndugu wa mzee

Kwa yeyote ambaye anamjua mtu ambaye alifanya kazi national milling Shinyanga naomba aniunganishe. Sina maelezo mengine zaidi ya hayo kwa hiyo naomba msaada wenu wakuu. Mwenye nia ya kunisaidia anitumie meseji pm.


update :

bado sijafanikiwa
 
Kwa hiyo ya kufanya kazi national milling ilikuwa lini kwa mara mwisho? Maana NMC zilikufa siku nyingi sana. Yale ma-godown pale SHY huwa yanakodishwa kwa watu kwa ajili ya kutunzia mizigo, sasa sidhani kama utapata mtu wa kukuelekeza pale!
 
  • Thanks
Reactions: A85
Jaribu kuulizia mtu anayejua waliokuwa wafanyakazi wa NMc shinyanga ndio pa kuanzia
 
Kwa hiyo ya kufanya kazi national milling ilikuwa lini kwa mara mwisho? Maana NMC zilikufa siku nyingi sana. Yale ma-godown pale SHY huwa yanakodishwa kwa watu kwa ajili ya kutunzia mizigo, sasa sidhani kama utapata mtu wa kukuelekeza pale!
Mkuu apo nashindwa kujua mara mwisho kufanya kazi ili kuwa ili kuwa mwaka gan mana ata mama hajui
 
Boss nashukuru kwa kuumulizia mzee wako Nami nitajaribu kusaidia kuulizia kwa wafanyakazi wa zamani wa national milling na wagita?
 
Kama alikuzila na hakukujali mpaka umekuwa mtu mzima kuna haja gani ya kumtafuta

Mkuu kuna masuala ya matambiko mambo ukiona hayaendi vizuri unaambiwa nenda kwa wazee wakuteeme mate,sasa pata picha Mzee wako humjui,Ndugu zake huwajui hilo tambiko litawezekana kweli.
 
Back
Top Bottom