Namtafuta baba yangu Melkioli Mayala, taarifa ya mwisho alihamia Uvinza, Kigoma

Picha ni muhimu sana wkt unamtafuta mtu,sio kila mtu atalifahamu jina
Utu uzima ukifika majina ya watu yanabadilika,pengine sasa anajulikana na jina la baba fulani,na ukumbuke vijana wengi ndio wapo kwenye social media ni rahisi alikiona picha akamjua na kupeleleza
Leta picha hata kama ya zamani
 
Poleni kwa majukumu yote ya kujenga Taifa.
Mimi ninaitwa Silivia naishi Uyole, Mbeya. Baba yangu alimuoa mama Igoma wakati akifanya kazi kama muuguzi wa afya hapo Igoma, Mbeya. Tulizaliwa mapacha mimi na Immanuel. Baba alitengana na mama tukiwa wadogo hivyo tumekua bila uwepo wake.

Mimi nimeolewa na nina watoto watatu na huyo Immanuel naye alioa na kupata watoto wawili lakini kwa bahati mbaya alifariki mwaka 2015 na akazikwa Mbeya na watoto wake ninawalea mimi.

Mama ambaye kwa kabila ni Mkinga alitupa taarifa hizi kuhusu baba na hakupenda tumjue kama ilivyo matokeo ya wapendanao wakigombana.

Simtafuti baba ili kupata urithi au chochote bali niweze kumjua na kuwajua ndugu zangu wengine kama mwanafamilia.
Taarifa ya mwisho ni kuwa baba alipohama Igoma alihamia Uvinza kiwanda cha chumvi mkoani Kigoma.

Kwa watanzania wenzangu wenye MAPENZI mema na wenye kumjua huyu Melkioli MAYALA mnisaidie kumpata baba yangu. Nimetumia uwanja huu mpana ili niweze kusaidika.

Asanteni.

0753772399

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina jamaa yangu Uvinza nimempigia simu anamfahamu baba yako amestaafu na yupo hai. Nimemwambia anitafutie namba yake ya simu nikiipata ntakutumia.
 
Baba yangu ni msukuma alifika mbeya igoma na kumuoa mama yangu aitwaye Lusia Binamu Swalo(mkinga)na kuzaa naye watoto wawili mapacha Silivia na Immanuel mwaka 1981.

Alifanya kazi ya uuguzi hospitali ya kiwira igoma baadaye akaondoka akaenda uvinza kiwanda cha chumvi akawa mtumishi huko.

Kiukweli tumekuwa bila kumjua baba na tukakua mimi wa kike nikaolewa na wa kiume kulwa(Immanuel) akaoa na kupata watoto wawili..Mimi nina watoto watatu.

Kwa bahati mbaya Kulwa alifariki mwaka 2015 na tukawa tumezika bila ya baba yetu MELKIOLI Mayala kujua.

Nina waomba watanzania wenzangu hasa mnaoweza kunisaidia kujua baba yangu alipo awe hai ama amekufa nione kaburi lake ama niwajue ndugu wengine wa baba.

Jamani nina kiu nimjue baba yangu popote alipo kwa kabila ni msukuma.

Mimi nipo mbeya uyole kwa mawasiliano namba zangu ni hizo hapo juu.

0753772399
0767264455 Mtafute huyu mtu na umuulizie kuhusu huyo Mayalla, pengine anaweza kukusaidia kumpata (kama ndio yeye)
 
Picha ni muhimu sana wkt unamtafuta mtu,sio kila mtu atalifahamu jina
Utu uzima ukifika majina ya watu yanabadilika,pengine sasa anajulikana na jina la baba fulani,na ukumbuke vijana wengi ndio wapo kwenye social media ni rahisi alikiona picha akamjua na kupeleleza
Leta picha hata kama ya zamani
Picha haipo mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom