Namtafuta baba yangu Melkioli Mayala, taarifa ya mwisho alihamia Uvinza, Kigoma

Miaka yote ulikuwa wapi?

Mpka leo hii umemkumbuka baba?

Ni kwanini mama yenu tangu mkiwa watoto hakuwaonesha baba yenu yupo wapiiiiiii??

Nadhani sehemu pekee ya kuanzia mkomalie mama akuoneshe baba yupo wapiiii
 
Baba kama alikuacha bila kuona kuna muhimu akutafute huyo ni baba sasa, unamtafuta wakati yeye hakutafuti mpotezee tu hana issue
Mambo haya wakati mwingine ni mkanganyiko tupu.

Baba alaumiwe kama aliondoka huku akijua kuwa kaacha watoto kule huyoo akasepa makusudi. Wakati mwingine mabaharia hawa anakwenda sehemu kikazi kwa muda mfupi anakula tunda kimasikhara huko anaondoka hata bila kujua kama kaacha mbegu. Ndiyo baadaye mtu anaibuka anamtafuta babake mnabaki kushangaa.

Ila hata mimi. I have zero respect kwa mwanaume anayetandika mimba halafu anakimbia majukumu makusudi. Huko mbele ya safari mtoto kakua eti ndiyo anadai heshima na privilege za kibaba. No way...

Inaonekana binadamu tuna tamaa sana ya kujua chanzo chetu na ndugu zetu wa damu kama wapo . Huwa nawaona hapa katika Maury mtu ana miaka 50 na ana kila kitu lakini bado anamsaka baba yake. Kujitafuta.
 
Ndio mwanangu nimefurahi kusikia upo dotto, mimi mwenyewe Baba yako nipo uyole hapa nakula mtungi karibu na ofisi za tulia trust nitakutafuta mwanangu
Jinga moja limekosa cha kuchangia.

Pole Sana dada yangu, taarifa za baba yako utazipata tu jf ni uwanja mkubwa Sana.Mungu akutimizia ndoto yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni kwa majukumu yote ya kujenga Taifa.
Mimi ninaitwa Silivia naishi Uyole, Mbeya. Baba yangu alimuoa mama Igoma wakati akifanya kazi kama muuguzi wa afya hapo Igoma, Mbeya. Tulizaliwa mapacha mimi na Immanuel. Baba alitengana na mama tukiwa wadogo hivyo tumekua bila uwepo wake.

Mimi nimeolewa na nina watoto watatu na huyo Immanuel naye alioa na kupata watoto wawili lakini kwa bahati mbaya alifariki mwaka 2015 na akazikwa Mbeya na watoto wake ninawalea mimi.

Mama ambaye kwa kabila ni Mkinga alitupa taarifa hizi kuhusu baba na hakupenda tumjue kama ilivyo matokeo ya wapendanao wakigombana.

Simtafuti baba ili kupata urithi au chochote bali niweze kumjua na kuwajua ndugu zangu wengine kama mwanafamilia.
Taarifa ya mwisho ni kuwa baba alipohama Igoma alihamia Uvinza kiwanda cha chumvi mkoani Kigoma.

Kwa watanzania wenzangu wenye MAPENZI mema na wenye kumjua huyu Melkioli MAYALA mnisaidie kumpata baba yangu. Nimetumia uwanja huu mpana ili niweze kusaidika.

Asanteni.

0753772399

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni kwamajukumu yote ya kujenga Taifa.
Mimi ninaitwa Silivia naishi uyole mbeya.Baba yangu alimuoa mama igoma wakati akifanya kazi kama muuguzi wa afya hapo igoma mbeya.
Tulizaliwa mapacha mimi na Immanuel. Baba alitengana na mama tukiwa wadogo hivyo tumekua bila uwepo wake.

Mimi nimeolewa na nina watoto watatu na huyo Immanuel naye alioa na kupata watoto wawili lakini kwa bahati mbaya alifariki mwaka 2015 na akazikwa mbeya na watoto wake ninawalea mimi.

Mama ambaye kwa kabila ni mkinga alitupa taarifa hizi kuhusu baba na hakupenda tumjue kama ilivyo matokeo ya wapendanao wakigombana.
Simtafuti baba ili kupata urithi au chochote bali niweze kumjua na kuwajua ndugu zangu wengine kama mwanafamilia.
Taarifa ya mwisho ni kuwa baba alipohama Igoma alihamia uvinza kiwanda cha chumvi mkoani kigoma.

Kwa watanzania wenzangu wenye MAPENZI mema na wenye kumjua huyu Melkioli MAYALA mnisaidie kumpata baba yangu.Nimetumia uwanja huu mpana ili niweze kusaidika.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
jaribu kwenda NIDA, nenda kwenye mitandao ya simu, nenda TRA, hayo ni maeneo yanayohifadhi taarifa za watu. NIDa wao ndio wanaatarifa nyingi.

Nida wakipata jina lake watatafuta kama ana kadi ya taifa basi itaonesha hadi alipojiandikishia, pia mitandao ya simu, pia TRA kama ana leseni yoyote iwe ya gari au biashara badi TRA wana taarifa zake hasa taarifa za mji anaoishi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom