Namtafuta baba yangu Melkioli Mayala, taarifa ya mwisho alihamia Uvinza, Kigoma

0767264455 Mtafute huyu mtu na umuulizie kuhusu huyo Mayalla, pengine anaweza kukusaidia kumpata (kama ndio yeye)
Niliongea naye akaniambia vizuri na kunihakikishia kuwa yupo uvinza ila ameshastaafu kazi ya udaktari.
Amesema yupo hai na leo ijumaa jioni angetuunganisha naye ili wawasiliane na mwanaye kwa bahati mbaya amechelewa kutoka kazini.

Soon mambo yatakuwa safi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau msihofu nipo ndani ya kiwanda hapa uvinza kesho by saa 4 nitakuja na jibu lililonyooka au usiku huu nitawapa jibu maana hapa nimelala ila msihofu cha muhimu kuche
 
Baba yangu ni msukuma alifika Mbeya Igoma na kumuoa mama yangu aitwaye Lusia Binamu Swalo (mkinga) na kuzaa naye watoto wawili mapacha Silivia na Immanuel mwaka 1981

Alifanya kazi ya uuguzi hospitali ya Kiwira Igoma baadaye akaondoka akaenda Uvinza kiwanda cha chumvi akawa mtumishi huko

Kiukweli tumekuwa bila kumjua baba na tukakua mimi wa kike nikaolewa na wa kiume kulwa(Immanuel) akaoa na kupata watoto wawili. Mimi nina watoto watatu.

Kwa bahati mbaya Kulwa alifariki mwaka 2015 na tukawa tumezika bila ya baba yetu MELKIOLI Mayala kujua.

Nina waomba watanzania wenzangu hasa mnaoweza kunisaidia kujua baba yangu alipo awe hai ama amekufa nione kaburi lake ama niwajue ndugu wengine wa baba.

Jamani nina kiu nimjue baba yangu popote alipo kwa kabila ni msukuma.

Mimi nipo Mbeya Uyole kwa mawasiliano namba zangu ni hizo hapo juu.

0753772399
Mzee Melkiory yupo hai buheri wa afya yupo hapa uvinza mtaa wa nyambutwe ana mke na watoto napo huku ana mapacha kwa taarifa za Intel na amestaafu ila yupo salama kwa mawasiliano zaidi PM nikuunge na mjukuu wake maana ni jirani yangu njia ya kwenda kibaruani
 
Huo ubin (Njaa/Mayala) ni common mno usukumani pengine kila kijiji hilo jina lipo Shinyanga,Geita.

Lingekuwa jina walau unique la ukoo ingekuwa rahisi hata kuunganisha dots kwa kutumia jina tu.
 
Naipongeza jf na wanajamii forum wote.

Nami nitamtafuta ndugu yangu muda sio mrefu
Ngoja mimi.
Kuna mama mmoja daima anatamani kumpata mzazi mwenzake.
Mazingira yako hivi: Akiwa mfanyakazi kazi za ndani Iringa mjini miaka ya 2000 hadi 2001, alipata ujauzito kwa kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Clement.
Kijana huyo naye alikuwa wa kuja tu hapo mjini.

Alipopata taarifa za binti kuwa mjamzito, alihama mji kwenda Makambako na baadaye Dsm.

Akiwa Makambako alifahamishwa kuhusu kuzaliwa kwa watoto lakini hakufuatilia. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa rafiki yake ambaye sitamtaja jina.

Nimeandika kumsaidia huyu mama maana watoto wanamsumbua kutaka kumfahamu baba yao. Watoto ni wakubwa sasa na wamehitimu kidato cha nne. Wanatafuta future yao wakiwa na mama tu. Ni mapacha wa kiume.

Clement yasemekana ni mhehe wa maeneo ya kuelekea Idodi huko Iringa. Na kwa maelezo ya huyu mama, watoto wanafanana na baba yao.

Ombi: Kwa anaemfahamu Clement wa mazingira haya niliyoeleza au kama yuko humo, tafadhal wasiliana na nami ili nikuunganishe na huyo mama na wanao.

Lakini pia kuwa na utu na huruma kwani unafahamu uwepo wa wanao lakini hujajishughulisha kuwatafuta licha ya teknolojia kuwa msaada kwa sasa.

Simu 0755274552
 
Mkuu ungefungua uzi mpya nadhani ingeleta urahisi zaidi kumpata kuliko kupost ndani ya uzi huu.

Mtu hadi aone comment yako si rahisi na uzi huu tayari una updates kwenye page ya kwanza, kwa hiyo mtu akifungua anaishia kusoma zile updates tu.
 
Mrejesho.
Hadi sasa tumefanikiwa kumpata mtu wa karibu kabisa na Mzee Mayala ambaye muda mwingi wapo wote.Huyo baba ameomba tumpe muda kidogo kuna mambo ayaweke sawa kisha atatuunganisha naye wawasiliane na mwanaye.

Kwa ufupi jf imesaidia mno ni jukwaa lisiloshindwa jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ungefungua uzi mpya nadhani ingeleta urahisi zaidi kumpata kuliko kupost ndani ya uzi huu.

Mtu hadi aone comment yako si rahisi na uzi huu tayari una updates kwenye page ya kwanza, kwa hiyo mtu akifungua anaishia kusoma zile updates tu.
Asante kwa ushauri
 
Niwashuru wana jf wote.
Shukrani za dhati kwa mkuu Chief na kinusikwetu kwa msaada wenu.
Silivia leo ameweza kuongea na baba yake Mzee Mayala na hakika kwa niaba yake nasema Mbarikiwe nyote.
Pia nimshukuru member mmoja aliyenishauri nilete jukwaa la hoja mchanganyiko kutoka lile la mapenzi hakika Mungu ambariki pia.
Sasa wote wamejawa na furaha tele.
Mimi nilitumika kama msaada tu kumsaidia afikie hatua hii ya leo.Mzee Mayalla yupo Uvinza na amestaafu. Nawashukuruni mno.

Asanteni.

Ubarikiwe pia kwa kumsaidia huyo ndugu
 
Mungu ni mwema
 
Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya kifo cha Mzee Mayala kutoka kwa binti yake ambaye amefiwa na huyo baba mzazi.

Ninlazimika kusema hapa kwa kuwa msaada wa jukwaa hili hadi watu hawa kuonana ulianzia hapa. Jukwaa hili limekuwa chanzo cha tabasamu lao hadi anafikwa na umauti.

Mungu azidi kuwabariki kwa ushirikiano mkuu kwa familia hii bado anazidi kuwashukuru mno.
Mbarikiwe mno wote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom