Namtafuta baba mzazi Mr. Jumanne aliyekuwa dereva Chuo cha CBE Dodoma

batan

JF-Expert Member
Jan 15, 2016
417
364
Nimezaliwa miaka ya 80 mwishoni na sasa nna familia na watoto wawili na ni muajiriwa. Nakuja hapa kumtafuta mzee ambaye ni baba yangu ambaye sijawahi muona na majina yake niliambiwa jina lake moja tu kuwa anaitwa Jumanne. Mzee huyu alikuwa ni dereva katika chuo cha CBE Dodoma miaka ya 1986 hivi.

Natamani niweze tu kumfahamu kwani ni muda sasa nimeishi na mama bila kumfahamu yeye, sijui kilitokea nini kati yake na maza maana maza huwa haniambii kabisa kuhusu mzee na hilo jina tu nmelipata kwa baadhi ya ndugu zangu upande wa mama.

Tafadhari kama kuna mtu anakuwa na a,b,c zake za Mr. Jumanne hasa hasa kwa yeyote aliefanya naye kazi chuo cha CBE Dodoma miaka hyo ya 1986 naomba anitaarifu kwa dm.

Nitashukuru saana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mleta mada, kama mama yako alikulea mpaka hapo ulipofika kwanini unahangaika kumtafuta asiye kulea? Uje umkute ana matatizo lukuki uwanze kuyabeba.

Labda kama unataka kufahamu magonjwa ya kurithi kutoka kwenye ukoo wa Baba yako uanze kujilinda.
 
Mbona umemtaja kama Mzee na umeshasema hujawahi kumuona? huenda kwa miaka hiyo ya 80's alikuwa chalii tu na bado hajawa Mzee.
 
Mama yako alikuwa anaishi maeneo yapi Dodoma? Aliolewa au alikuwa kimada tu?Sisi wenyeji wa Dodoma tunaweza kukusaidia ukitupa mrejesho.
 
MZ.jpg
 
Mbona mzembe sana wewe jamaa unaandika bandiko hili upo wapi? Inamaa haujui Dodoma ilipo? Baba yako mzazi unakuja hapo kuomba msaada!! Umeniharibia shibe yangu ya mabumunda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
batan,
Si uende CBE dodoma katika kitengo cha masijala utapewa habari zake zoote? Umeishaambiwa alifanyakazi pale!
 
Pole sana mleta mada, kama mama yako alikulea mpaka hapo ulipofika kwanini unahangaika kumtafuta asiye kulea? Uje umkute ana matatizo lukuki uwanze kuyabeba.

Labda kama unataka kufahamu magonjwa ya kurithi kutoka kwenye ukoo wa Baba yako uanze kujilinda.


Mkuu vipi leo account yako imehakiwa Nini??

Baba Ni baba bhana Ni vema akamtafuta baba yake asikilize upande wa pili. Wanawake sometimes ndio chanzo Cha migogoro kwa kiburi halafu anakuja mjaza mtoto chuki isiyokua na msingi.

Wengine tunatamani hata tupate huo mzigo wakutunza baba lakini ndio hivyo, usimkatishe TAMAA.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom