shaks001
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 1,246
- 1,070
Tunapoamka asubuhi hatujui kitakachokuja kutokea mbele yetu mpaka tutakapooenda vitandani mwetu usiku!Kikubwa tunatakiwa tuweke mambo yetu sawa na Mungu kila sekunde maana hatujui sekunde ipi utapata majanga.
Jana jioni mida ya saa 1 nikiwa na rafiki yangu kwenye gari ndogo tulipatwa na ajali mbaya sana barabara ya kongowe-Kivukoni.Yaani ajali inapotokea huwezi kuamini hali inayotokea kwa kipindi kile maana unaona kabisa mtoa roho huyu hapa.
Jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba sote wawili tulitoka salama lakini gari zote tatu zilikuwa hazifai.Maana ajali ilisababishwa na dereva mlevi mmoja ambaye aligonga gari mbili kwa pamoja.
Napenda kuwashauri ndugu zangu tuwe na utamaduni wa kufunga mikanda kwani ina msaada mkubwa sana inapotokea ajali,bila mikanda hata zile air bags zingekuwa ni hatari sana kwa maisha yetu maana zote mbili zilifyatuka.
Nakushukuru Mungu kwa ulinzi wako!Jioni njema.