Namshukuru Mungu kwa kuniepusha na kifo

shaks001

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2014
Messages
1,250
Points
2,000

shaks001

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2014
1,250 2,000
Tunapoamka asubuhi hatujui kitakachokuja kutokea mbele yetu mpaka tutakapooenda vitandani mwetu usiku!Kikubwa tunatakiwa tuweke mambo yetu sawa na Mungu kila sekunde maana hatujui sekunde ipi utapata majanga.

Jana jioni mida ya saa 1 nikiwa na rafiki yangu kwenye gari ndogo tulipatwa na ajali mbaya sana barabara ya kongowe-Kivukoni.Yaani ajali inapotokea huwezi kuamini hali inayotokea kwa kipindi kile maana unaona kabisa mtoa roho huyu hapa.

Jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba sote wawili tulitoka salama lakini gari zote tatu zilikuwa hazifai.Maana ajali ilisababishwa na dereva mlevi mmoja ambaye aligonga gari mbili kwa pamoja.

Napenda kuwashauri ndugu zangu tuwe na utamaduni wa kufunga mikanda kwani ina msaada mkubwa sana inapotokea ajali,bila mikanda hata zile air bags zingekuwa ni hatari sana kwa maisha yetu maana zote mbili zilifyatuka.

Nakushukuru Mungu kwa ulinzi wako!Jioni njema.
 

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Messages
5,782
Points
2,000

dmkali

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2014
5,782 2,000
POLE SANA; KUMBE NDO WEWE, JANA SAA MOJA NA NUSU NILIPITA MAENEO HAYO PANAITWA KWA PIUSI WATU WAMEPASUANA; POLE SANA; NILIMUONA TRAFIKI ANAPIMA PIMA VIPI ILIKUWAJE? SIKUWEZA KUSIMAMA MAANA USALAMA ULIKUWA MDOGO PAMEKAA VIBAYA.
 

shaks001

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2014
Messages
1,250
Points
2,000

shaks001

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2014
1,250 2,000
Ajali mbaya sana! halafu mmepona? ungesema tu ajali.

Pole sana mkuu.
Kila mmoja mkuu anaweza kuelezea ubaya wa ajali kwa kadri ya jinsi ilivyomkuta.Yes,nasema ni mbaya sana maana sikuhadithiwa,nimeona ni muujiza kutoka nilivyotoka japokuwa maumivu ya ndani yapo lkn bado naona kama sijaumia kwa aina ile ya ajali.
 

shaks001

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2014
Messages
1,250
Points
2,000

shaks001

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2014
1,250 2,000
POLE SANA; KUMBE NDO WEWE, JANA SAA MOJA NA NUSU NILIPITA MAENEO HAYO PANAITWA KWA PIUSI WATU WAMEPASUANA; POLE SANA; NILIMUONA TRAFIKI ANAPIMA PIMA VIPI ILIKUWAJE? SIKUWEZA KUSIMAMA MAANA USALAMA ULIKUWA MDOGO PAMEKAA VIBAYA.
Ndio mkuu!ilikuwa sisi.Na kweli usalama pale ni mdogo maana muda mfupi tu tulikuta tushaibiwa baadhi ya vitu.
 

Forum statistics

Threads 1,392,181
Members 528,565
Posts 34,100,876
Top