Namshukuru Mungu kununusuru na ajali mbaya sana ya kugogwa na lori

Lyatuu the Great

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
212
85
Namshukuru sana Mungu kwa kuniokoa na ajali mbaya sana ya gari kugongana na lori na halikusimama kabisa likakimbia. Hakika nimeuona upendo wa Mungu kwangu. Niko naendelea na Matibabu.ninasikitika sana baada ya ajali vibaka kama 9 wakavamia gari langu na kuanza kuiba vitu usiku huo betri,rejeta hadi matairi. Nashukuru kwa ushauri niliopewa na kaka yangu Bro. Ronald Lyatuu wa kukaa mbali na gari kwani wangeniua vibaka wale wangenikuta kwenye gari.
1475992542561.jpg
 
Pole sana mkuu! Mungu Azidi kushusha nguvu za uponyaji juu yako upate nafuu haraka. Gari na vingine vyote vinanunulika, Uhai na uzima wako ndio vitu pekee visivyoweza kununuliwa kwa pesa! Tunamshukuru Mungu kwa kuwa umesalimika na tunakuombea upone haraka!
 
Pole sana Mkuu
Mungu atakuponywa Haraka kwa uwezo wake.
Vi mini Camera muhim sana kwenye magari ila tunapuuzia.Maana vibaka na gari iliyofanya ajali vyote ungevinasa.Maana ile inafichwa
 
pole sana mkuu. hakika Bwana ni mwema na fadhira zake hazina mwisho. juhudi zikizokupatia hiyo gari zitakuwezesha upatikabaji wa vipuri vilivyoibiwa. nakutakia uponaji mwema na wa haraka. AMINA!
 
Back
Top Bottom