Namshauri Rais kuvunja Baraza badala ya kutengua mmoja mmoja

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Wakuu habari zenu nataka kwanza kuanza hapa.

Je, ni sahihi kumukosoa Rais? Kama ni sahihi nianze kwa kumkosoa mama Samia kwa machache, najua kila mtu anaona kazi anayo fanya Rais wetu. Kiukweli mama anapiga kazi vizuri sana.

Lakini hakuna aliye mkamilifu mimi nashauri mama awe na msimamo siyo anachofanya, mimi nakosoa taratibu aliyofuata ya kutovunja baraza halafu anatengua mmoja mmoja.

Najua humu kuna watu walio karibu na mama, mwambieni mama afuate katiba; huyo ni Rais mpya na wa awamu nyingine kwahiyo inapaswa avunje baraza harafu ndio ateuwe upya. Mama fuata katiba japo unayofanya ni mazuri.

Team zote naomba mje kutia neno au kukosoa.
 
Sheikh Ponda anataka kumuona Mama kuhusu Ile Issue ya Mashekhe waliolundikwa jela na Hayati Mwenda

Mbona viherehere wa CCM wanamuwekea kauzibe
 
Inatakiwa mama afanye hivyo
Wacha upumbavu unajua gharama ya kuvunja Baraza na kuteua wapya? She has chosen continuity over power ego! Deal with that! Kwani uchaguzi umeitishwa mpaka atengue na kuunda Baraza jipya? Kifungu kipi hicho cha Katiba kinaelekeza unachosema hebu leta evidence?
 
Tena ni Baraka na Thawabu kubwa kumkosoa Raisi

Na Maraisi wasikivu ndio huongoza vizuri
Njia bora ya kumkosoa,ni kumshauri

Na ikiwa atakataa au kutosikiliza ushauri,kisha kwa bahati mbaya,akateleza katika maamuzi yake

Haifai kumtusi wala kumbeza
Bado tunayo nafasi ya kumshauri na kumuombea mafanikio
 
Wacha upumbavu unajua gharama ya kuvunja Baraza na kuteua wapya? She has chosen continuity over power ego! Deal with that! Kwani uchaguzi umeitishwa mpaka atengue na kuunda Baraza jipya? Kifungu kipi hicho cha Katiba kinaelekeza unachosema hebu leta evidence?
Hahahaha nimecheka kwa sauti kwahiyo unapinga huku hufahamu
 
Hahahaha nimecheka kwa sauti kwahiyo unapinga huku hufahamu
Leta evidence tukufafanulie! Baraza la Mawziri ikiwemo Bunge linavunjwa Mhula ukiisha na pale Bunge linapokosa imani kwa Rais kwa vile Mawaziri hutokana na Wabunge kwa hiyo Bunge likivunjwa na Baraza la Mawziri huvunjwa ! Haya leta evidence pale anapofariki Rais ni lazma Baraza la Mawaziri livunjwe wakati Mgombea Mwenza au Makamo wa Rais ameomba na kupigiwa kura pamoja!
 
Back
Top Bottom