Namshauri Malinzi ajiuzulu Urais wa TFF ili amalizane na Jamhuri

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,218
25,625
Nasema mwanzo mwanzoni kuwa mimi ni Mwanasheria na Wakili Msomi. Najua kuwa kutuhumiwa na kushtakiwa si kukutwa na hatia. Kila mshtakiwa si mwenye hatia hadi mahakama itamke hivyo. Mambo hayo,kama moja ya haki za msingi za binaadamu,nayajua na kuyaheshimu.

Rais wa TFF,Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu wake Mwesigwa wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya jinai mbalimbali yakiwemo ya kutakatisha fedha. Kabla ya hapo,Malinzi alikuwa moja ya waliochukua fomu za kugombea tena Urais wa TFF.

Ili kupunguza mzigo wa mambo na kukubali yaliyompata kimaisha,namshauri Jamal Malinzi ajiuzulu Urais wa TFF ili apate nafasi ya kumalizana na Jamhuri kwenye kesi yake ya jinai. Kuendelea kuwa Rais wa TFF akiwa mshtakiwa kunaweza kutafsirika kama kung'ang'ania kichaka chake cha 'kupiga dili'.

Kujiuzulu,pamoja na kupunguza mzigo,kutamfanya Malinzi awajibike ipasavyo kwa yaliyompata na kukubali kilichomkumba kimaisha. Hakuna haja ya Mshtakiwa kuendelea kuwa Rais wa TFF au hata kujadiliwa kama mgombea mtarajiwa wa Urais wa TFF. Apambane kwanza na jinai yake.Kujiuzulu,wakati mwingine,huilinda punje ya heshima iliyobaki!
 
Akijiuzuru ataishije????
 
Napinga vibaya sana , kwani walipomkamata walimpa option hiyo ?

Acheni mahakama iamue .
 
Masahihisho - hata kabla ya urais wa TFF , Malinzi hakuwahi kuwa Masikini .
Kwamba siku anatoka tumboni kwa mamaake alitoka na mapesa?anyway Utajiri au Umaskini wake hauna mahusiano na tabia za kipigaji...mwizi mwizi tu ht km anatoka familia ya kitajiri....
 
Nasema mwanzo mwanzoni kuwa mimi ni Mwanasheria na Wakili Msomi. Najua kuwa kutuhumiwa na kushtakiwa si kukutwa na hatia. Kila mshtakiwa si mwenye hatia hadi mahakama itamke hivyo. Mambo hayo,kama moja ya haki za msingi za binaadamu,nayajua na kuyaheshimu.

Rais wa TFF,Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu wake Mwesigwa wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya jinai mbalimbali yakiwemo ya kutakatisha fedha. Kabla ya hapo,Malinzi alikuwa moja ya waliochukua fomu za kugombea tena Urais wa TFF.

Ili kupunguza mzigo wa mambo na kukubali yaliyompata kimaisha,namshauri Jamal Malinzi ajiuzulu Urais wa TFF ili apate nafasi ya kumalizana na Jamhuri kwenye kesi yake ya jinai. Kuendelea kuwa Rais wa TFF akiwa mshtakiwa kunaweza kutafsirika kama kung'ang'ania kichaka chake cha 'kupiga dili'.

Kujiuzulu,pamoja na kupunguza mzigo,kutamfanya Malinzi awajibike ipasavyo kwa yaliyompata na kukubali kilichomkumba kimaisha. Hakuna haja ya Mshtakiwa kuendelea kuwa Rais wa TFF au hata kujadiliwa kama mgombea mtarajiwa wa Urais wa TFF. Apambane kwanza na jinai yake.Kujiuzulu,wakati mwingine,huilinda punje ya heshima iliyobaki!
Acha UZANDIKI kijana.
 
Tatizo la kupenda kupiga dili kaka ni kama ugonjwa, ila nahisi Malinzi hataki kung'oka akisubiri msaada wa FIFA, maana wapenzi wa soka wako tayari tufungiwe kuliko kuacha uozo pale TFF!
 
Nami namshauri aachie ngazi atashangaa mambo mengi kwenye ile kesi yatapungua nguvu!! Hata dhamana atapatiwa......akubali yaishe aachie ngazi FIFA hata wakija hawezi kumbadilishia ile charge sheet! Na kwa awamu hii wako tayari tufungiwe hata miaka 5 ila Ile kesi ipo pale pale!!!
 
Japo jamaa simkubali lakini njia waliotumia kumuondoa siyo sahihi mana ile imezoeleka kwa wanasiasa tu anawajibu wa kung'ang'ania mpaka FIFa waje wakate mzizi wa fitina
 
Back
Top Bottom