Namshauri daktari aliyesimamishwa kazi na Waziri wa Afya huko Chunya, Mbeya, aingie sekta binafsi

Maslows

Senior Member
Jun 29, 2020
122
225
Nadhani kisa cha huyu doctor aliyesimamishwa kazi na Waziri Gwajima kwa sakata la ugonjwa ulioibuka huko Chunya, Mbeya kitampa jibu zuri sana kwa nini madaktari na wafanyakazi wengine wengi wanaamua kukimbia ajira za serikalini na kuingia private sector.

Ukweli ni kwamba katika awamu ya uongozi wa Magufuli, kufanya kazi serikalini, na hasa ukiwa na madaraka fulani imekuwa kero sana. Uongozi wa juu umesimamia zaidi kwenye siasa na kujipendekeza kwa Magufuli kuliko taaluma za kazi. Viongozi seikalini wamekuwa waoga wa kufanya maamuzi, na mara nyingine hata kuchukua msimamo kwamba ni bora kutofanya chochote kuliko kufanya kitu halafu Magufuli au waziri wakakutumbua.

Sasa kazi katika mazingira kama hayo inakuwa very stressful - kwanza mtu unakuwa na stress za kazi, na pili unakuwa na stress za kiongozi mwenye nidhamu ya woga anaegopa kufanya maamuzi au anaefanya maamuzi ili kujipendekeza au kujikosha kwa Magufuli asitumbuliwe yeye!

Kwa hiyo Magufuli anapaswa kuelewa kwamba kwa sasa kufanyia kazi serikali ni kujitafutia stress zisizo la lazima zinazoweza kukuaa kabla ya wakati wako, na kadiri unavyokuwa na madaraka ndivyo stress zinavyozidi.

Mfano mzuri ni huyu Waziri Gwajima, alivyokurupuka kumsimamisha kazi huyu daktari. Gwajima hakufanya hivyo kama taratibu za kazi, bali amefanya hivyo kumu-impress Magufuli - na ni wazi amefanya uamuzi mbaya na wa uonevu. Sasa huyu doctr akienda private sector, au madaktari wengine wakifanya hivyo kwa kuepuka hii mihemuko ya kisiasa kwenye taaluma mtawalaumu?
Aliyekwambia kuw hatarudishw ni Nani?
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,382
2,000
Kwa

Kifupi, kama umepewa madaraka na unakosa ujasiri wa kufanya maamuzi yenye tija kwa wananchi na Tz basi ni wazi hicho cheo hakikufai na hata ksbla ya kutumbuliwa ww jitumbue mwenyew! Wanaoshindwa kufanya maamuzi siyo kweli kuwa wanashindwa bali kinachotakiwa kutatuliwa kinakuwa hakina tija binafsi ya huyo kiongozi ndio maana anakipotezea! Kama kuna maamuzi hayo yanaambatana na fungu lake binafsi mbona wanatoaga maamuzi fasta! Kipindi cha awamu hii cha kwanza ktk kufanya maamuzi lazima kizangatie tija kwa wananchi maskini na nchi kwa ujumla! Ukitanguliza maslahi binafsi lazima yatakukuta makubwa! Ww na wenzio mnaolalama kila kukucha ni miongoni mwa watu mliozoea kutumia vyeo kupitishia maamuzi yasiyo na tija kwa taasisi, wananchi na nchi kwa ujumla bali maslahi binafsi! Awamu hii imewavuruga kwelikweli na hivyo kujikuta mnaganda wakati wa kufanya maamuzi yenye tija kwa jamii na siyo yenu binafsi!
Pole ndugu yangu. Bila shaka unaumwa. Waombe ndugu wakupeleke hospitali inayoshughulika na magonjwa ya afya ya akili ili kujiridhisha kama umzima au la! Dalili hazioneshi kama umzima.
 
Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,322
2,000
Pole ndugu yangu. Bila shaka unaumwa. Waombe ndugu wakupeleke hospitali inayoshughulika na magonjwa ya afya ya akili ili kujiridhisha kama umzima au la! Dalili hazioneshi kama umzima.
We jipeleke mwenyewe ndio kunakuhusu!
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
57,280
2,000
Nadhani kisa cha huyu doctor aliyesimamishwa kazi na Waziri Gwajima kwa sakata la ugonjwa ulioibuka huko Chunya, Mbeya kitampa jibu zuri sana kwa nini madaktari na wafanyakazi wengine wengi wanaamua kukimbia ajira za serikalini na kuingia private sector.

Ukweli ni kwamba katika awamu ya uongozi wa Magufuli, kufanya kazi serikalini, na hasa ukiwa na madaraka fulani imekuwa kero sana. Uongozi wa juu umesimamia zaidi kwenye siasa na kujipendekeza kwa Magufuli kuliko taaluma za kazi. Viongozi seikalini wamekuwa waoga wa kufanya maamuzi, na mara nyingine hata kuchukua msimamo kwamba ni bora kutofanya chochote kuliko kufanya kitu halafu Magufuli au waziri wakakutumbua.

Sasa kazi katika mazingira kama hayo inakuwa very stressful - kwanza mtu unakuwa na stress za kazi, na pili unakuwa na stress za kiongozi mwenye nidhamu ya woga anaegopa kufanya maamuzi au anaefanya maamuzi ili kujipendekeza au kujikosha kwa Magufuli asitumbuliwe yeye!

Kwa hiyo Magufuli anapaswa kuelewa kwamba kwa sasa kufanyia kazi serikali ni kujitafutia stress zisizo la lazima zinazoweza kukuaa kabla ya wakati wako, na kadiri unavyokuwa na madaraka ndivyo stress zinavyozidi.

Mfano mzuri ni huyu Waziri Gwajima, alivyokurupuka kumsimamisha kazi huyu daktari. Gwajima hakufanya hivyo kama taratibu za kazi, bali amefanya hivyo kumu-impress Magufuli - na ni wazi amefanya uamuzi mbaya na wa uonevu. Sasa huyu doctr akienda private sector, au madaktari wengine wakifanya hivyo kwa kuepuka hii mihemuko ya kisiasa kwenye taaluma mtawalaumu?
Hata Coronavirus Covid-19 ilivyoanza kutokea China, madaktari walitahadharisha, serikali ya China ikawa inaficha ukweli.

Mpaka ilipokubali, tatizo lilikuwa kubwa sana.

Hatujifunzi
 
Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
8,542
2,000
... ukisoma vizuri ile press release ya Wizara ya Afya hila zote zimewekwa kuhakikisha yule Dr hachomoi. Ina kipengele kinasema "... na hata kama ni kweli kungekuwa na ugonjwa, mwenye mamlaka ya kutangaza ni waziri wa afya ...".

Hapa always hata "akipangua" vipengele vingine vyote, hiki cha "kutangaza" hachomoi unless airidhishe mamlaka ya nidhamu kwamba "hakutangaza".
Acha kuimba kisungura hapa

Mojawapo ya majukumu ya Mganga mkuu Wilaya ni kuwa msemaji wa masuala yote ya afya ndani ya eneo lake la utawala.

Waziri yeye hupelekewa taarifà.

Kama ni janga linalokumba eneo la zaidi ya wilaya au mikoa tofauti hapo ndipo Waziri na Katibu Mkuu Wizara wanahusika.

Naona unaanza kuimba wimbo wa kuhalalisha ushetani kwenye hili sakata la kipuuzi la kumsimamisha Mganga wa Wilaya
 
Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
8,542
2,000
... kosa ambalo Dr yule hatachomoa ni kujitwalia mamlaka ya "kutangaza" huku akijua mamlaka hayo ni ya waziri wa afya peke yake au kwa atakayemkaimisha kwa niaba yake. Mnakumbuka ya Dr. Mwele Malecela na zika? Analiwa kichwa yule.
Kea hiyo janga likitokea nyumbani kwangu mwenye mamlaka ya kulisemea ni kiongozi wangu wa Mtaa?

Acha utoto
 
Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
8,542
2,000
... yote hayo yanweza kuwa sahihi ila ... kosa ambalo Dr yule hatachomoa ni kujitwalia mamlaka ya "kutangaza" huku akijua mamlaka hayo ni ya waziri wa afya peke yake au kwa atakayemkaimisha kwa niaba yake. Mnakumbuka ya Dr. Mwele Malecela na zika? Analiwa kichwa yule.
Dokta Mwele alijitwalia mamlaka ya kuisemea nchi na haihusiani na issue kama ya mganga wa wilaya.

Mzee naona umeamua kulazimishia saikolojia ya kishetani sasa
 
Faru Tobbi

Member
Oct 29, 2018
60
125
Acha kuimba kisungura hapa

Mojawapo ya majukumu ya Mganga mkuu Wilaya ni kuwa msemaji wa masuala yote ya afya ndani ya eneo lake la utawala.

Waziri yeye hupelekewa taarifà.

Kama ni janga linalokumba eneo la zaidi ya wilaya au mikoa tofauti hapo ndipo Waziri na Katibu Mkuu Wizara wanahusika.

Naona unaanza kuimba wimbo wa kuhalalisha ushetani kwenye hili sakata la kipuuzi la kumsimamisha Mganga wa Wilaya
Napinga na wewe kidogo kwenye swala la kutangaza magonjwa ya mlipuko utaratibu Ni tofauti mganga mkuu haruhusiwi, Sheria inasema waziri wa afya, mganga mkuu wa serikali, au mtu atakaye teuliwa na waziri wa afya. Kwa uelewa zaidi kasome public health act ya 2009
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom