mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Yusufu(Mtu wa Mungu) alitoa maono ya njaa. Kaisali/Mwanasiasa(Farao enzi hizo) akaagiza kujengwa maghala yenye uwezo wa kutunza chakula miaka saba wakati Misri nzima itakapokumbwa na njaa.
Binafsi sijaiona njaa Tanzania ila nikipita mabarabarani ninaiona ardhi sehemu kubwa ikiwa na Mazao Dhaifu.Upungufu wa chakula baadhi ya maeneo sio habari maana ni toka uhuru na Yawezekana tukaja na njia mpya sio ileile ya kila siku kugawa chakula.
Kazi ya Kaisali sio Kugawa Chakula wakati njaa halisi haijafika au Kumuomba Mungu Mvua Inyeshe, Bali ni kuleta mipango yenye uhalisia jinsi ya kukabiliana na Njaa ijayo kama kweli ipo.
Ninawashangaa wote wanaoshabikia kauli ya kugawa chakula kama kilele cha ubunifu wa Mwanasiasa.