Namsaidia vipi mtu mwenye tatizo la Obsessive Compulsive Disorder (OCD)?

LadyRed

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
9,647
2,000
Aendelee na therapy kwa Daktari wa Magonjwa ya Akili....like kumuona daktari na kumueleza jinsi anavyojiskia hadi aone hali yake imetengamaa

Tiba namba moja kwa mambo ya Akili ni kuwa 'aware' kuwa unapitia hali fulani...hio awareness itakusaidia kuchagua ur 'reaction'/behaviour...

Bora uumwe vingine lakini sio 'engine' ya mwili
 
Am mackdy

Member
May 9, 2020
30
95
Naombeni kuuliza OCD husababishwa na kuishi sehemu zenye sheria Kali sana kama shule za boarding!? Kwn akili inakuwa inadhohofika
 
Am mackdy

Member
May 9, 2020
30
95
Kuna Hali mara mara unakuta unahisi kama kwenye kucha Kuna uchafu ivyo unakuwa mara kwa mara unajibinya juu kucha au ndani ya kucha au unakuta tuu unahisi kufanya mara kwa mara , ivyo nauliza ni kawaida kufanya au!?? sababu tangia nianze kusikia kuhusu OCD kuna hali zingine napata sasa sijui ni kawaida
 
Am mackdy

Member
May 9, 2020
30
95
Mkuu asante kwa kurahisisha kazi nilitaka kuanzisha uzi juu ya OCD, kiukweli wahanga tupo japo kwa level tofauti kwa upande wangu sijafikia extreem level kabisa ila nimeanza kutafakari mambo nilioyapitia na reaction zangu huko zamani i can relate kuwa hili jambo nipo nalo zamani bila kujua mpaka pale nilipoanza kusoma na kufahamu juu ya OCD,Nadhani tunaweza kulipuuzia lakini halina mwisho mwema kabisa.
Vipi ndugu upande wako upo vipi au ntaweza pata mawasiliano yako
 
Mackdymacswagz

New Member
Sep 10, 2019
2
20
Jamani mada basi juu ya hii thread wahanga tupo wengi eety ,mimi mwenyewe nmebidi nipostpone kwa muda masomo ya chuo niwezefanya kwnz matibabu, naomba kuuliza je ni bima ya bei gani inaweza fanya matibabu ya mental health.
 
Am mackdy

Member
May 9, 2020
30
95
Habari za asubuhi wadau,

Nina rafiki yangu anasumbuliwa na tatizo ambalo mwanzo lilianza kama utani.

Yaani tulipokuwa tunasoma naye alikuwa ananiambia kila nikijibu mitihani nakuwa sijiamini hasa hesabu yaani hata 2+8 jibu ni kumi, ila yeye anaweza kukaa hata dakika tano anakuwa kama anajiuliza hivi jibu hili ni kweli? Na mara nyingi alikuwa hamalizi mtihani.

Baadae akawa akitaka kulala anajiuliza nimefunga mlango kweli yaani anaweza kurudi hata mara tatu kuhakikisha. Alipoenda chuo kusomea Udaktari hali ikazidi anakuwa na mawazo.

Mara anajihisi amemtukana Mungu anaogopa adhabu ya Mungu. Hali hiyo ikamsumbua kiasi cha kuahirisha masomo slipopelekwa hospital hizi za kawaida walisema hawaoni tatizo eti mtu lazima uwaze.

Tukaona twende kwenye hospitali za watu wenye matatizo ya akili tukakutana na dokta akasema huo ni ugonjwa unaoitwa OCD.

Wakatupa dawa na maelekezo mengine ila kwa sasa karudi chuo lakini naona kama tatizo bado lipo kwani bado nikiongea naye ananiambia kuwa anatumia nguvu kubwa sana kwenye kujisomea mawazo yanakuwa mengi.

Labda mnisaidie njia za kumsaidia.
Naomba uniconnect na huyo rafiki yako
 
Cathy Diwani

Senior Member
Feb 13, 2016
111
250
Tatizo la akili ni gumu sana.

mimi binafsi nina Anxiety disorder tena wakati mwingine napatwa na Panic attack hii ikikukuta mkuu unaandika wosia maana unahisi kama unakufa unaweza kuanza kukimbia tu bila sababu watu wakakushangaa/au unatetemeka yani unakua kama umepandwa na pepo , Akili yako mwenyewe inaweza kukuchezea ukaiona dunia Chungu sana.

Mkuu kwanza Rafiki yako lazima ajue kuwa hayuko pekeyake kila mtu ana matatizo ya akili ila yanazidiana tu. kila anapopatwa na jambo Inabidi Arelax kurelax ni dawa kubwa, japo kurelax ukiwa katika aina yoyote ya Disorder ni jambo gumu kama kushinda vita
Mkuu natamani nikuone unisaidie kama umeweza kuishinda hii hali. Mimi ni mhanga wa anxiety disorder
 
concordile 101

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
1,334

Mimi nina kama lako ila kwangu imeongezka nakuwa natetema sana halafu nina woga sana. Yaan hii imenipelekea kuwa nawakimbia watu. Kazini namuogopa karibia kila mtu hata wale ambao tuko level moja. Kutokana na kutojiamini nimekuwa muongo sana hasa pale napohisi nimekosea lazima nitadanganyq tu
 
Vi rendra

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
3,051
2,000
Mkuu natamani nikuone unisaidie kama umeweza kuishinda hii hali. Mimi ni mhanga wa anxiety disorder
Pole, mimi inakaaga inanirudia ila niko kwenye process ya kuimaliza kabisa... Kwakua unasumbuliwa na hii hali niko tayari kukuona maana najua jinsi gani inavyodrain energy ya mtu ... usijali sana healing ni process kinachotakiwa usikate tamaa

Imenisumbua sana tangu mwezi wa 7 mwishoni mpaka leo, imenilazima kuachana na mitandao ya kijamii na marafiki , maana nilikuja kugundua nikiwaona watu wana furaha najilaumu kwanini mm nakua hivi kwahiyo nikaona chochote kinachomaliza energy yangu naachana nacho.... process ni nyingi ila
nmepata ahueni sana na hata jf nmefikiria kuifuta sema tu kuna jambo langu limenikwamisha..

Karibu sana kipenzi niko available anytime unapohitaji tumaini.
 
Vi rendra

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
3,051
2,000
Mimi nina kama lako ila kwangu imeongezka nakuwa natetema sana halafu nina woga sana. Yaan hii imenipelekea kuwa nawakimbia watu. Kazini namuogopa karibia kila mtu hata wale ambao tuko level moja. Kutokana na kutojiamini nimekuwa muongo sana hasa pale napohisi nimekosea lazima nitadanganyq tu
Ni kawaida ya anxiety mpenzi... unachokiogopa huwa kinakutawala!
Hata mimi nmeshaga tetemeka sana kama nmepandwa na pepo, nmeshaliaga sana... nmesha ogopa watu na mengine makubwa kuliko unavyodhani ila niko kwakua kabla hujafa tumaini lipo na amani ipo pia ..
usijali utakua sawa kabisa
 
TZ-1

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
758
1,000
Huyo ugonjwa wa OCD hatakiw kusomea udaktari , huo ni saw saw na battle confusions . Mwambie aache hyo coz
Asije choma sindano wagonjw mara2 mbili na kuwa over doz sambamb na mambo mngn kwakuw swala la afya ni sensitive
 
Cathy Diwani

Senior Member
Feb 13, 2016
111
250
Ni kawaida ya anxiety mpenzi... unachokiogopa huwa kinakutawala!
Hata mimi nmeshaga tetemeka sana kama nmepandwa na pepo, nmeshaliaga sana... nmesha ogopa watu na mengine makubwa kuliko unavyodhani ila niko kwakua kabla hujafa tumaini lipo na amani ipo pia ..
usijali utakua sawa kabisa
Mimi huu ni mwaka wa tatu. Nililazimika kuacha masomo kwa ajili ya tatizo hili, niliogopa kusafiri, niliogopa kujumuika na watu, niliogopa kula, muda wote nahisi kama nakufa dakika chache zijazo.... Mwanzo nilijua nimepata heart attack, mpaka nikakimbizwa hospital na ambulance.... Zile dalili nilikuwa nazo ndio madaktari wakasema ni panic attacks, nikaanzishwa dose za anti depressants... Nikimaliza dose baada ya muda nikipitia changamoto yeyote tatizo linarudi.

Mpaka nimeamua kukaa mbali na familia yangu maana kuna sehemu wanachangia huku wakinisimanga kuwa matatizo nimejitakia mwenyewe
 
Jamani Pole Cathy hili swala linaweza kwisha kabisa..ila ni process
 
Mine eyes

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
5,807
2,000
Mimi huu ni mwaka wa tatu. Nililazimika kuacha masomo kwa ajili ya tatizo hili, niliogopa kusafiri, niliogopa kujumuika na watu, niliogopa kula, muda wote nahisi kama nakufa dakika chache zijazo.... Mwanzo nilijua nimepata heart attack, mpaka nikakimbizwa hospital na ambulance.... Zile dalili nilikuwa nazo ndio madaktari wakasema ni panic attacks, nikaanzishwa dose za anti depressants... Nikimaliza dose baada ya muda nikipitia changamoto yeyote tatizo linarudi.

Mpaka nimeamua kukaa mbali na familia yangu maana kuna sehemu wanachangia huku wakinisimanga kuwa matatizo nimejitakia mwenyewe
Pole sana..

Hili tatizo linahitaji utulivu mno na kutiwa

moyo..sasa familia zetu hizi wengi

hawama uelewa huo... Nimeona wengi

wanaishi vibaya sana ...ni kama

wanatengwa!

Jitahidi ujifunze kujituliza kwa kuongea na

nafsi yako kimya kimya.. na kujipa moyo.

Fanya na kuangalia vitu vinavyo

kufurahisha...jiamini .. ...angalia pia na tiba

mbadala..zinasaidia..
 
bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,907
2,000
Nilisoma soma Jf /Google nikagundua kuwa nna hilo tatizo, sijawahi kutumia dawa yoyote nahangaikaga mpaka nakua sawa,
Tiba hasa ni kutojiweka karibu na vitu vinavyokutia woga pamoja na hizi mada unazochangia,Kwakua imeshakua trauma hata vitabu vinavyoelezea badala vikupunguze ndio vinazidisha.
Uwe na furaha mda mwingi
Chukulia poa usichukulie kama tatizo kuubwa.
Huwezi kuhakikisha kwamba ni ugonjwa huo kwa kusoma tu, ni lazima ukamwone daktari halafu akuambie kama ni kweli au la. Wao wanakuwa na vipimo au masuali yao wanayokuuliza halafu ndiyo wanakwambia kwamba uko sawa au la.

Ni sawa na ku'google' symptoms:
 
Vi rendra

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
3,051
2,000
Pole sana..

Hili tatizo linahitaji utulivu mno na kutiwa

moyo..sasa familia zetu hizi wengi

hawama uelewa huo... Nimeona wengi

wanaishi vibaya sana ...ni kama

wanatengwa!

Jitahidi ujifunze kujituliza kwa kuongea na

nafsi yako kimya kimya.. na kujipa moyo.

Fanya na kuangalia vitu vinavyo

kufurahisha...jiamini .. ...angalia pia na tiba

mbadala..zinasaidia..
familia zetu changamoto sana zinazidisha matatizo mno, unaweza jikuta unamchukia kila mtu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom