Nampongeza sana Mohamed Said : Nawalaumu Watanzania

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,508
23,709
Huyu mzee wa historia ni mtu asiyekata tamaa. Naangalia Jukwaa la Historia kwa siku sikosi kuona threads zake mpaka mbili au tatu.

Pamoja na vijana wengi kwa ujivuni wao wanaonekana kutochangia mada zake badala yake wanaenda kujazana mwenye jukwaa la MMU Mzee hajakata tamaa.

Nampongeza kwa kuwa pamoja na kubezwa wakati mwingine huwa hajazibiki badala yake huendelea kushuka mistari tu.huyu ni nyani mzee amekwepa mishale mingi.

Utakuta mzee wa watu kashuka madini ila walio comment 3. This isnt fair.watanzania acheni unafiki. Mnataka akifa ndo mje mseme alikuwa anatia madini sana.

Yaani uzi wa Zero Q unapata comments za kumwaga mpaka pages 200 au ile ya Kula tunda kimasikhara inafika pages 1000+ ila harakati za Mzee wangu said nobody gives a shit.

Mods muwe mnalazimisha watu wachangie mada zake.
😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Inavunja moyo sana.. kama mtu uko so fragile. Wanasema nzi hukimbilia taka
 
Ukisimamia unachokiamini wala mengine hayakupi shida. Mzee Mohamed Said ameamini katika historia aliyoichagua kwa kufanya tafiti ya historia hiyo, moyo wake umependa na kuwa na furaha bila kujalisha hadhira inapokeaje..

Ukifanya jambo kwa kutaka attention hutafanikiwa utakapokosa hiyo attention. Hilo jambo ni kinyume kwa Mzee Mohamed ndio maana tunamuona kila mara anaendelea kuchanja mbuga na mada zake.
 
Huyu mzee wa historia ni mtu asiyekata tamaa. Naangalia Jukwaa la Historia kwa siku sikosi kuona threads zake mpaka mbili au tatu.

Pamoja na vijana wengi kwa ujivuni wao wanaonekana kutochangia mada zake badala yake wanaenda kujazana mwenye jukwaa la MMU Mzee hajakata tamaa.

Nampongeza kwa kuwa pamoja na kubezwa wakati mwingine huwa hajazibiki badala yake huendelea kushuka mistari tu.huyu ni nyani mzee amekwepa mishale mingi.

Utakuta mzee wa watu kashuka madini ila walio comment 3. This isnt fair.watanzania acheni unafiki. Mnataka akifa ndo mje mseme alikuwa anatia madini sana.

Yaani uzi wa Zero Q unapata comments za kumwaga mpaka pages 200 au ile ya Kula tunda kimasikhara inafika pages 1000+ ila harakati za Mzee wangu said nobody gives a shit.

Mods muwe mnalazimisha watu wachangie mada zake.
Chizi...
Haya mambo yanataka subra.

Nilipoanza kuandika kurekebisha historia ya TANU kwanza nilikutana na ghadhabu za wasomaji na vitisho.

Mijadala ikawa inajaza na kuna mjadala ulivunja rekodi kwa kuenda miezi sita bila kusimama.

Mimi nikiwa peke yangu na watu wengine wachache.

Taratibu wasomaji wakatambua kuwa ninayoandika ndiyo ukweli wenyewe.

Mmoja mmoja wakakimbia ulingoni wakaniacha kwani hawana la kusema kwa kuwa kwenye ukweli uongo hujitenga.

JF ni moja ya sehemu moja katika nyingi zinapokwenda makala zangu kwa hiyo nina wasomaji wengi kiasi wanaponiandikia naelemewa.

Pili JF ndipo ilipo maktaba yangu kuu ukitoa blog yangu: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

Hapa ndipo ninapochomoa link kwa ajili ya rejea na makala zinarudi miaka 10 nyuma.

Nakushukuru sana kwa kujali.
 
Tatizo maudhui ya kidin din na kuponda serikal na kuiita ya mfumo wa din flan kisha kuonyesha din flan ndio ilipigania uhuru wa nchi hii..hii nadhan ni kero watu wasiopenda.
Au namchanganya huyu bwana?
Jang...
Hofu ya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kuwa Waislam ndiyo walikuwa mstari wa mbele imewaathir wengi.

Hawapendi hili jambo lielezwe lakini ndiyo ukweli wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Huwezi kuifuta historia.

Ukweli huu leo umekubalika kwa ushahidi madhubuti usio shaka.

Mwaka wa 1987 gazeti la Africa Events lilipochapa makala yangu "In Praise of Ancestors," (London) ikimtaja Abdulwahid Sykes kama muasisi wa TANU na kuitaja Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika kuwa moja ya taasisi zilizotoa viongozi na wanachama wa mwanzo wa TANU, toleo lote la gazeti lilikusanywa lisisomwe.

Leo baada ya miaka 30 tunajadili haya bila hofu na kitabu nilichoandika kuhusu historia hii kipo sokoni tunakwenda toleo la nne.

Screenshot_20200622-180240.jpg
 
Ukisimamia unachokiamini wala mengine hayakupi shida. Mzee Mohamed Said ameamini katika historia aliyoichagua kwa kufanya tafiti ya historia hiyo, moyo wake umependa na kuwa na furaha bila kujalisha hadhira inapokeaje..

Ukifanya jambo kwa kutaka attention hutafanikiwa utakapokosa hiyo attention. Hilo jambo ni kinyume kwa Mzee Mohamed ndio maana tunamuona kila mara anaendelea kuchanja mbuga na mada zake.
Mwifa,
Ahsante sana.
 
Nimemuuliza maswali kwenye marejeo yake ya vitabu vipya vya Nyerere.

Itafaa kama pia ataweza kufanya documentary kuwatafuta wazee wa zamani waliobaki waweke mambo kwenye oral history.
Kiranga,
Waliobakia ambao mimi nawajua wanaweza kuhadithia historia ya uhuru wa Tanganyika kwa namna ninayoieleza mimi ni wachache - Abbas Sykes, Aisha "Daisy" Sykes, Bi. Zainab Ally Sykes, Bilal Rehani Waikela na Mama Maria Nyerere.

Katika hawa mwenye umri mdogo ni bint yake Abdul Sykes ambae kamuona Mwalimu Nyerere siku ya kwanza amefika nyumbani kwa baba yake mwaka wa 1952.

Mama Maria na Mwalimu wakimjua Daisy toka utoto wake.
 
Jang...
Hofu ya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kuwa Waislam ndiyo walikuwa mstari wa mbele imewaathir wengi.

Hawapendi hili jambo lielezwe lakini ndiyo ukweli wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Huwezi kuifuta historia.

Ukweli huu leo umekubalika kwa ushahidi madhubuti usio shaka.

Mwaka wa 1987 gazeti la Africa Events lilipochapa makala yangu "In Praise of Ancestors," (London) ikimtaja Abdulwahid Sykes kama muasisi wa TANU na kuitaja Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika kuwa moja ya taasisi zilizotoa viongozi na wanachama wa mwanzo wa TANU, toleo lote la gazeti lilikusanywa lisisomwe.

Leo baada ya miaka 30 tunajadili haya bila hofu na kitabu nilichoandika kuhusu historia hii kipo sokoni tunakwenda toleo la nne.

View attachment 1486527
And what is your motive behind all this? Why concerntrating so much on religious issues kuliko hata uhuru wenyewe?
 
Chukua muda usome kitabu cha Abdul Sykes (1998)utaona hakuna dini kama imani ila nimeeleza jinsi Waislam walivyopambana na ukoloni.

Kuhusu uhuru wenyewe nimeeleza toka siku unafanyika mkutano kumjadili Nyerere nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio Ukerewe 1953.

Waliokuwapo ni Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hiki ndicho kikao kilichomtia Nyerere kwenye uongozi wa TAA 1953 na 1954 TANU ikaundwa.

Historia ya Nyerere ndivyo ilivyoanza na kitabu kimeeleza hadi "uhuru wenyewe" ulipopatikana mwaka wa 1961.

Wewe naamini historia uliyosoma ni ile ni Nyerere ndiye aliyeasisi TANU historia ambayo imewafuta wazalendo wengi sana.

Umeniuliza nini kilichonifanya kuandika.
Nadhani jibu umelipata.
 
Jang...
Chukua muda usome kitabu cha Abdul Sykes (1998)utaona hakuna dini kama imani ila nimeeleza jinsi Waislam walivyopambana na ukoloni.

Kuhusu uhuru wenyewe nimeeleza toka siku unafanyika mkutano kumjadili Nyerere nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio Ukerewe 1953.

Waliokuwapo ni Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hiki ndicho kikao kilichomtia Nyerere kwenye uongozi wa TAA 1953 na 1954 TANU ikaundwa.

Historia ya Nyerere ndivyo ilivyoanza na kitabu imeeleza hadi "uhuru wenyewe" ulipopatikana mwaka wa 1961.

Wewe naamini historia uliyosoma ni ile ni Nyerere ndiye aliyeasisi TANU historia ambayo imewafuta wazalendo wengi sana.

Umeniuliza nini kilichonifanya kuandika.
Nadhani jibu umelipata.
Nimekuelewa mkuu.kama lengo ni jema basi sawa cheers.
 
Umeeleza vizuri sana, na vizuri umeiona changamoto ya aina ya Wanachama tuliomo humu JF...wengi wetu humu ni Mashabiki wa nyuzi za aina fulani fulani tu.

Mzee Saidi ni Mtu anayejaribu kusukuma ajenda zake...nampongeza kwa bidii aliyonayo ingawa hiyo ni hatari sana iwapo maandiko yake yatakuwa yanafika moja kwa moja kwenye vichwa vya watu hawa wa hizo mada za "umewahi kula tunda kimasihara" bila kukutana na Wabobezi wengine wanaoweza kusahihisha panapopotoshwa.

Kupungua kwa Wafuatiliaji wa nyuzi zake huenda ni baada ya Watu kupata picha halisi ya mlengo wa Mzee Said.

Mzee amekuwa akiendekeza misimamo yake na kupingana na wengine wote wanaojaribu kusahihisha maelezo yake...anaamini kwamba anachofahamu, kuandika au kusikia yeye basi ndio mwisho.

Pia Mzee amekuwa hatoi majibu kabisa au kutoa majibu hafifu au kuishia kumlaumu Mtu anayehoji au kuja na maelezo tofauti kwa jambo alilolielezea yeye.

Wakati mwingine anakinzana hata na Watu wale wale anaowataja yeye au kuwatumia kwenye rejea zake.

Jambo la msingi ni kuwa unaposoma makala za Mzee Said jaribu kutafakari na ukiweza tafuta vyanzo vingine ili uweze kuunganisha dots...si vyote anavyosema ni vya kweli ingawa vipo baadhi ni sahihi.
 
And what is your motive behind all this? Why concerntrating so much on religious issues kuliko hata uhuru wenyewe?
Bahati mbaya au nzuri Mzee Said ni rahisi kufahamika kwa wengi tofauti na wengi tunaochangia humu kwa majina fake.

Ila kiukweli kuna wakati analazimisha hoja basi unaamua tu kuondoka ili kutunza heshima ya Mtu anayeweza kuwa kama Mzazi wako...hivyo Mtu kusoma na kukaa kimya haimaanishi kuwa amekubaliana na hoja zake bali ni kuepusha tu ubishani na Mtu mwenye misimamo yake.
 
May Day,
Hivi kabla ya kitabu cha Abdul Sykes nani alikuwa anaijua historia hii?

Mimi sijamlazimisha mtu kuniamini uko huru kukataa yote yaliyomo kwenye kitabu changu ukabaki na "ukweli,"" katika kitabu cha historia ya TANU kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni.

Wala mimi sijamzuia mtu yeyote kuandika historia ya TANU.

Wala mimi siwezi kuwa na ujinga wa kuamini najua kila kitu.

Ninachokuambieni siku zote ni kuwa mimi nimeijua historia ya TANU na historia ya Nyerere kwa kiwango hiki kwa sababu historia ya TANU ni sehemu ya historia ya wazee wangu na hivyo ndivyo ilivyo kwa Nyerere kule kusuhubiana na wazee wangu na yeye kawa sehemu katika histori yao.

Mimi sina uwezo wa kulazimisha chichote zaidi ya kueleza nikijuacho na watu wakasoma.

Ukomo wa uwezo wangu unaishia hapo.
 
Bahati mbaya au nzuri Mzee Said ni rahisi kufahamika kwa wengi tofauti na wengi tunaochangia humu kwa majina fake.

Ila kiukweli kuna wakati analazimisha hoja basi unaamua tu kuondoka ili kutunza heshima ya Mtu anayeweza kuwa kama Mzazi wako...hivyo Mtu kusoma na kukaa kimya haimaanishi kuwa amekubaliana na hoja zake bali ni kuepusha tu ubishani na Mtu mwenye misimamo yake.
Hata historia official ilikuwa ya uwongo
Ndo maana wale waliomeza historia ya uwongo
Wanakataa historia hii ya ukweli hata kama ime base zaidi Kwa waislam..

Mzee Said anaweza andika historia ya Paul Rupia vizuri kuliko wengine naamini
Lakini hajataka sababu hata hao kina Sykes historia Yao ilikuwa inafutwa kimyakimya
 
Mohamedi Saudi Mzee alieamua kuandika histori ya taifa hili kwa mrengo wa kidini ambao anaamini ni usahihi zaidi. Pengine anakosea na pengine anapatia. Lakini hata waandika magazeti Kama hao waliotajwa hapo bila shaka walikuwa wakoloni waliokimbizwa. Na bila shaka lengo lao kulikuwa moja tu kututenganisha watanganyika
 
Back
Top Bottom