Nampongeza Rasi kwa kufunguka........ Tupo palepale ..Liwalo na Liwe!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nampongeza Rasi kwa kufunguka........ Tupo palepale ..Liwalo na Liwe!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, Jul 2, 2012.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Napenda haki,ila haki bila wajibu sio sahihi!! aidha ukitaka uheshimiwe lazima ujiheshimu. kwa muda sasa nimeanza kumuelewa Rais Jakaya Kikwete kuwa ni mtu Mstahimilivu na muungwana ambaye nimeshuhudia mara nyingi akichelea kutoa maamuzi ili kudhihirisha Umakini wake! Kwa tabia ya waafrika hasa viongozi wa kiafrika sio wengi wenye staha, wengi huamua maamuzi ya kidikteta na kufedhehesha.

  Kauli ya Rais aliyoitoa jana kupitia vyombo vya habari ninaiunga mkono kwa asilimia mia, sitaki kuamini kuwa serikali hii inauwezo huo wa kulipa Daktari waliyemsomesha bure milioni tatu na nusu, haiwezekani!!

  Kauli ya Rais niya uwazi na ukweli!! Anayeona mshahara wa lakitisa ni mdogo aende popote akaajiriwe, huo sio ushauri mbaya.! Tatizo lililopo ni kuwa madaktari wengi ni watoto wa vigogo maana inaeleweka wazi kuwa shule zinazofundisha masomo ya sayasi na zenye ufaulu mzuri ni zile za kulipia ambazo watoto wa shule za kata hawawezi kuwa madaktari. Kwa mantiki hii, hakuna haja ya kusumbuana, Hospitali za Binafsi zipo nyingi, kilichopo hao wanaodhani mshahara ni mdogo waende tu kwa amani, kuliko kuwachochea madaktari wenye moyo na kazi kugoma na kuumiza wagonjwa.

  Kama madaktari wanadhani taaluma yao ni bora sana, basi waende wakajitafutie sehemu stahiki. Stop migomo, vivyo hivyo kwa walimu, kama wanadhani kazi ya ualimuhailipi hakuna haja ya kusumbua serikali shule za binafsi zipo nyingi japo usalama wa kazi ni mdogo dawa si kugoma dawa ni kuondoka!!!!
   
 2. M

  Mukalabamu Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  anakupumulia nini?
   
 3. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kweli ni Rasi.Haya umesikika, hongera
   
 4. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  majibu mepesi sana!!
   
 5. A

  Anold JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Inaonyesha ndiyo kazi yako hiyo. Kama ni mmojawao waliogoma wee chapa lapa tu mnajua milioni tatu nyie? mmezoea eeh? Hii ni Afrika! Hata hizo tisa ni nyingi angepiga panga!!!!
   
 6. K

  Kingengame Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nakuunga mkono:

  Ni uwamuzi wa Busara, uliojaa upendo, huruma na msamaha kwa vijana wake Madaktari. Rahisi ametanguliza maslahi ya sisi tulio wengi kuliko kundi moja tu la watumishi. Hotuba ya Raisi imewahabarisha watanzania juu ya sakata hili kwa ujumla wake. Watanzania tumeyaelewa mahitaji ya msingi ya madaktari wetu na wala hatuyapuuzi, tumeuona uwezo na dhamira ya Serikali kuya-address hata kama kwa awamu. Sasa wito wangu kwa Madaktari ni kwamba muitumie nafasi hii kurudi kazini tupunguze vifo visivyo vya lazima wakati serikali ikilishughulikia suala la mafao ya wafanyakazi kwa ujumla wake. Mrejeshe mahusiano yenu mazuri yale ya awali kati yenu na wagonjwa/ wananchi. Madaktari na baadhi ya wananchi msiendelee kudanganywa na wanaharakati/ Wanasiasa hapa Dar es Salaam. Wananchi walio wengi nchini hususan wale waliopoteza ndugu zao kwa kukosa matibabu, wana hasira na watumishi wa sekta ya afya. Wanaharakati hawakufanikiwa kuwashawishi watu wote kuwa serikali ndio iliowauwa. Mgonjwa akija hospitali anamuona Daktari na sio kiongozi wa serilkali. Wananchi wanajua sasa dhamira na mchango wa serikali yao katika kuboresha hali ya huduma zetu za tiba; na mifano wanayo. Waliziona picha za Dr. Ulimboka akiwa ICU, wapo wanaosema miaka 10 iliyopita ICU haikuwa vile. Sasa hivi wananchi wanaeweza kuandamana dhidi yenu mkiendelea kuwa na shingo ngumu. Nawaomba msiwaamshe wananchi waliolala wasije wakafanya tathmini yao na kuwasha hasira ya uma dhidi yenu. Halafu msiwadanganye watanzania kuwa nyie mnataka zaidi kuboreshwa kwa mazingira ya kazi kuliko mishara yenu. Wananchi sikuhizi wanaelewa sana. Na huwezi kirahisi tu kuwa-blind kwa kelele za wanaharakati au wanasiasa. Hata hivyo: Mheshimiwa Raisi amewarahisishia wale ambao hawako tayari, waacha wenyewe, hivyo basi hatutegemei tena kuona huduma zikisimama. Ndugu zetu madaktari; sisi wananchi tunawependa mno, ninyi ndi mawakili wetu kwa mwenyezi Mungu, mnatutetea kila tunapokata rufaa ya kifo kwa kututibu. Maana baadhi ya magonjwa bila tiba ya haraka mtu hufa. Mnapotutibu ndio mnatukatia rufaa tusife. Tusaidieni. Na ndio maana serikali inaendelea kusomesha madaktari bure ili tuwe nao wengi watuponye.

  Kila la kheri Madaktari.

   
 7. Leftist

  Leftist Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nanukuu kauli yako... ''Tatizo lililopo ni kuwa madaktari wengi ni watoto wa vigogo maana inaeleweka wazi kuwa shule zinazofundisha masomo ya sayasi na zenye ufaulu mzuri ni zile za kulipia ambazo watoto wa shule za kata hawawezi kuwa madaktari.'' We ni muongo tena muongo wa kutupa. Mi ni medical student, chuo fulani cha serikali hapa nchini, asilimia kubwa tulio hapa ni watoto wa masikini. Acha kudanganya watu kama hauna data. :A S-baby::A S-baby:
   
 8. B

  Boniface m Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Mmh,maneno kama hayo si ya kiungwana kwa kiongozi,anatakiwa kutatua tatizo na wala c kusema muende kokote,ukweli ni kwamba nchi hi ina pesa ya kutosha kdogo kama tukigawana vizuri,shida hatugawani vzuri inabid viwango vya mishahara vipitiwe upya,mfano mshahara wa mwalimu wa certificate,marambili anapata mwanasheria mwenye certificate,zaid ya mara mbili anapata daktari,tofauti ni kubwasana kwakweli,halaf unasema huna wakati watu wanaiba mabilioni,wanaweka nje,wanyama wanabebwa hakuna aliyekamatwa inaingia akilini kweli?!
   
 9. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huna habari kuwa huyo unaemsifu na genge lake wameficha shilingi trilloni Tatu huko ughaibuni? Halafu jamaa kila kukicha anakwea pipa kwenda kutembeza bakuli; hiyo ni akili kweli?
   
 10. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Anampumulia kisogoni huyo
   
 11. D

  DAVIES JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 513
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Unapoongea kitu we schwazzenegar whatever unauhakika wanasomeshwa bure au unaongea tu hebu kakope pesa popote pale uone kama hutairudisha hivyo msitake kuudanganya uma eti mnasoma bure mikopo yote ile hulpwa kwa utaratibu maalumu kuna cha bure siku hiz?
   
 12. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ni kweli bwana,Andrew Chenge aliyehusika kwenye rushwa ya radar ni mtu mzuri.Alisomeshwa na serikali nje ya nchi wala hagomi na akiingiza hasara serikali kama bilion kadhaa yeye husema vijisenti tu...kidumu chama cha mapinduzi. Madaktari wana makosa kwa sababu serikali inawakopesha asilimia mia moja kudhamini mafunzo yao vyuoni,lakini wakipata kazi hawarudishi fedha serikalini wala kodi hawalipi...zidumu fikra za mwenyekiti! Kwa hiyo madaktari wanamakosa sana kuliko ufisadi wa EPA,RICHMOND,RADAR,MEREMETA,MISHAHARA HEWA n.k Hizo propaganda za mwaka 1970,serikali ya magamba ni wapotoshaji wakubwa!
   
 13. mtzedi

  mtzedi JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,364
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  KAJIBU HIVYO KWA VILE YEYE NA WENZIE WAPENDA POSHO,KUWEKA PESA ZETU USWISI WAKIUGUA WANAKWEA PIPA KWENDA UGHAIBUNI TABU KWETU WANANCHI WA KAWAIDA TUNAOBAHATISHA MAISHA :flypig:
   
 14. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  mi uwa nikiona shughuli ninayofanya ainiingizii kipato vile napenda natafuta shuguli nyingine uwa sigomi
   
 15. mapanga3

  mapanga3 JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 666
  Likes Received: 562
  Trophy Points: 180
  MATOPE MATUPU! Poor wewe!!
   
 16. L

  Lakuchumpa Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dhaifu. Wewe na unaemuunga mkono. Nani kakufanya ujue ku2mia jf, mwalm. Then zungumzia na Mps. Dhaifu
   
Loading...