Nampongeza Rais wa Tanzania kwa kuondoa watumishi wenye vyeti feki

Apparatus

Member
Dec 16, 2016
95
94
Kwako Mh. Rais wa Tanzania DR. John Magufuli,

Popote ulipo unapoendelea na dhamira yako ya kuijenga Tanzania mpya ninakusalimu.

Baada ya salamu hizo pia ninakupongeza kwa kuendelea na zoezi endelevu la kuwaondoa watumishi wote wa serikali waliogushi vyeti. Pia ninakuombea usife moyo kwani wapo wengi watakao kukejeli na kukubeza kwa kazi hii nzuri sana unayoendelea kuifanya. Mimi baada ya kutafakari kwa kina lengo kuu la kuwaondoa hawa wafanyakazi nimeamua kukuunga mkono. Wapo watoto wengi wa masikini tena wenye uwezo mkubwa ila wameshindwa kupata fursa za ajira kwa sababu ya hawa matajiri waliofoji vyeti ili kuingia kwenye ajira za umma kwa kupitia mlango wa nyuma. Ninakuomba sana Mh. Rais uwapiganie hawa kani ndiyo wenye shida.

Pia Mh. Rais ninaomba baada ya kuwaondoa nafasi zote zitangazwe kwa weledi na usaili ufanywe wa halali na mwisho mwa siku wenye kaki wapewe haki yao ili nidhamu ya utumishi wa umma iweze kulindwa. Haiwezekani ofisi za serikali sikose hadhi kwa kuingiliwa na wafoji vyeti.

Mh.Rais napenda ujie kuwa mabadiliko unayoyafanya yatapingwa na mafisadi wengi ila naomba sana ujie tulio nyuma yako ni wanyonge na watoto wa masikini wa nchi hii. Silaha yetu kubwa ni kukuombea Mungu kila siku katika kazi yako nzuri.

Nakukubali sana Mh. Rais Dr. John Magufuli
Mungu azidi kukuongoza
 
Takwim za juu juu zinasema ccm ndio waliongoza kuwa na vyeti feki, hadi humu kuna mwanaccm kila siku analialia kutaka huruma ya magu, anaitwa R. b aje nimpe ajira
 
Nikitafakari kuhusu vyeti fake natamani na Waajiri wote na Maafisa Utumishi wao waliopelekea watumishi wenye Vyeti Feki kuwepo Ofisini nao Watumbuliwe. Haiwezekani unakaa na Mtumishi hadi miaka 30 hujui kama anamedanganya sifa za kuajiriwa. Walishindwa nini kupeleka Cheti cha kila Mtumishi kuhakikiwa kabla ya Awamu hii kuwashtukia. Waziri wa Utumishi inabidi udeal pia na hawa waliosabibisha Watumishi wa Vyeti Fake kuendelea kufanya kazi, wakiwapa vyeo, mafunzo na safari za nje.
 
Siwezi kumpongeza mpaka watu wote wanaopokea fedha ya serikali km mshahara wahakikiwe.
Huwezi kutoa sheria halafu isiwaguse wengine halafu kwa ujinga wako unataka utuaminishe hao vigezo vyao ni kujua na kusoma tu. Ni upuuz sana
''MUNGU WETU NI WA HAKI NA HANA UPENDELEO. HUTOA HUKUMU SAWA BILA KUMUANGALIA MTU"
ww hata km unalala kweny za ibada lkn unaupendeleo hakika Mungu hawezi kukuona. Mfano. Unarudi nyumban na zawadi lkn unawapa watoto wako zawad lkn kwa kubagua. Hizo zawad hazina maana tena.
MM SIWEZI KUMPONGEZA SBB ALICHOKIFANYA NI KIDOGO SANA. SIKU WATU WOTE WANAOPOKEA FEDHA YA SERIKALI KM MSHAHARA KUHAKIKIWA NDIYO NITAMPONGEZA. Kinyume chake ni uonevu tu
 
Back
Top Bottom