Nampongeza Mwanakijiji kwa Uzalendo na Kuwapeleka mbio Mafisadi Kwa Hoja

AirTanzania

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
1,139
1,033
Kwa Jinsi mambo yaliyotekea jana kwenye TV ya Taifa inayoongozwa na Mafisadi Papa kuudanganya Umma kwa kupitia Station hiyo. Jana kulikuwa na Makamu mwenyetiki wa kamati ya Nishati ya Bunge kwenye tbc1 alikuwa anafoka kuhusu Mwanakijiji. Kwa kweli naona limewachoma na kuwauma lakini ukweli umewafikia hivyo Mwanakijiji yuko USA lakini anawapeleka mbio hawa Mafisadi huku Bongo. Swali nililokuwa najiuliza kuwa Je kama Mwanakijiji angewapo hapa bongo hawa Mafisadi wangekuwa wanalala vizuri, yuko mbali wanamuogopa hoja zake je angekuwapo hapo Dodoma nafikiri wangejiharia kwenye masuti yao:teeth:
 
Live long Mwanakijiji!
hoja zako si za kiuanaharakati tu bali ni za kiukombozi
 
Kwa kweli naona limewachoma na kuwauma lakini ukweli umewafikia hivyo Mwanakijiji yuko USA lakini anawapeleka mbio hawa Mafisadi huku Bongo. Swali nililokuwa najiuliza kuwa Je kama Mwanakijiji angewapo hapa bongo hawa Mafisadi wangekuwa wanalala vizuri, yuko mbali wanamuogopa hoja zake je angekuwapo hapo Dodoma nafikiri wangejiharia kwenye masuti yao:teeth:
Mkuu.
TZ zinatumika njia tofauti za kumdhibiti mtu.
Vitisho..kupewa mikopo mikubwa,.kumwagia acid, kutuma majambazi kwa mlengwa, au kukufikiria ni mwizi au jambazi na polisi au jeshi kukumaliza, ajali za gari, kukolimba na kumchakachua mtu kwa hongo au cheo na kumfumba mdomo......Wengi hunasa katika moja ya mitego hii.
Sasa kama mzee wetu angekuwa bongo basi angepambana na vitu kama hivyo. Wengi wa wanaharakati hunasa katika mitego hii.

Mitego yote hiyo ukiweza kuikwepa basi unabambikiwa kesi, bonge la kesi..ili utumie muda wako wote mahabusu na mahakamani, pia wanaku-discredit kupitia vyombo vya habari. Unapata picha ya mtu yoyote yule ambaye kwa miaka zaidi ya 20 kila mara yuko mahakamani? wee wacha tu. Ndio sababu tumepata jina "Bongo"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom