Nampongeza JPM Namponda SHEIN

Ndesaika

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
219
92
Ndugu Wadau ,

Kwanza kabisa naomba ieleweke wazi kabisa mimi siyo mpenzi wa chama chochote cha siasa bali mimi ni mpenzi wa TANZANIA. Hivyo basi naomba ieleweke natoa maoni yangu haya kwa Mtazamo wa Kitanzania Kwanza siyo Chama Kwanza. Kwa Heshima kubwa Sanaa napenda kuchukuwa nafasi hii Kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Rais wetu JPM kwa utenda wake wenye kutupa matumaini sisi wa TZ wanyonge ambao tulikuwa tumekata tamaa kimaisha baada ya chama Tawala kutudharau kwa muda mrefu na kutuacha yatima kikikumbatia matajiri na familia zao tu. Asante Ndugu JPM. MOLA akuongezee ujasiri na nguvu katika utendaji wako Pia Akupe BUSARA iliyo kamilika katika maamuzi yako. Lakini napenda Pia kuchukuwa nafasi hii Kumponda au Kuponda Ndugu SHEIN kwa Uteuzi wake wa baraza la mawaziri lililojaa Urafiki/Uchama/Ushoga bila kuzingatia Uwajibikaji, Weledi Pia nidhamu katika utendaji wa kila siku. Kusema kweli asilimia kubwa ya wateule ni wahafidhina ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo walio changia kuidhoofisha znz na hawana jipya lolote watakalo weza kufanya kuleta maendeleo ya kweli znz. Ndugu SHEIN hebu Acha kuendesha Nchi kishabiki ya Kichama achana na hao wasaka tonge na kuwa mzalendo wa kweli ili Historia ije kukumbuka kwa mazuri yako. Ndugu SHEIN Ipende znz kwa dhati na kaa na Mwenzio Maalim ili mjenge znz mpya. Mkiwa na dhamira ya dhati ndani ya nafsi zenu hakuna linalo shindikana. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Aisee umeongea vizuri sana wewe utakuwa umetoka kanisani au msikitini maana umeongea busara sana
 
kitendo cha shein kumpa hamad rashid uwaziri ni kumtia hasira hasimu wake mkuu seif sharif hamad na CUF kwa ujumla ,
 
shein kapunguza idadi ya wizara alafu kateua mawaziri wasio na wizara maalamu,style mpya ya kubana matumizi.
 
Back
Top Bottom