Nampongeza Askofu Gwajima kwa kuwa mwanasiasa mwenye mvuto zaidi kwa sasa Tanzania

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
246
500
Waswahili husema kila zama na kitabu chake, pia kila msimu na ndege wake

Katika historia ya siasa zimepita Zama mbalimbali ambazo zilibeba wanasiasa mbalimbali wenye mvuto. Kwa kutaja wachache ni Kama vile Mwl Nyerere, Sokoine, Mrema, Lowassa, Magufuli, Slaa, Zito na wengineo

Maisha hayamuachi mtu, watu huja na kupita

Baada ya kupita hao wote, kwa Sasa ni Gwajima. Naipongeza CCM kwa kuendelea kuzalisha wanasiasa wenye mvuto mbele ya wananchi wa Tanzania.

Natoa Rai kwa chama kuilinda tunu hii kwa maslahi ya chama na Taifa letu.
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,377
2,000
Mkuu hata hapo ufipa wanajua hili.

Hamna mtu mwenye muda na jizi la kura.

Nje ya mada, hivi Tiss mnaadhisha lini chama kingine cha upinzani dhidi ya cdm? Au bado mnapima upepo kama kitatoboa? Kizazi cha sasa sio kile cha kuchaguliwa chama na watawala majizi ya kura, bali kinachagua chenyewe kitakacho.

Naona sasa hivi mnapima upepo kila mara naona post zenu mkisema inabidi kianzishwe chama kingine, lakini response ya matakwa haya ni ndogo kupita maelezo. Kama vipi mpeni Zito na ACT yake, ila shida itakuwa ni yeye kushawishi watu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom