Nampendekeza huyu kuwa katibu mkuu wizara ya afya!!

Nadhani DR angefaa zaid kuwa PS pale, chaguo langu ni jamaa mmoja alikuwa wizara ya Afya, kisha NIMR anaitwa Dr. Peter Mbuji
 
Jamani hapa Mwana asha anakujaje wakati mada ni pendekezo la katibu Mkuu wa Wizara ya Afya? Mwanaasha angepata DIV I wengine wangesema baba yake kamuibia Mtihani au kapendelewa kwa vile Mtoto wa Mkuu. Tujadili Mada pale mahali pake ama sivyo tunapoteza muelekeo wa mjadala.
huyu jamaa namfaham ni bora hata mwana...jakaya kikwete aliyeiaibisha feza girls.mweupeee
 
Mtoa hoja amesema kweli, Hussein Katanga, ni mtendaji mzuri kabisa, hilo halina mjadala. Pamoja na utendaji wake bora uliotukuka mimi naamini TAMISEMI aliko panamfaa. Aendelee huko kwa maana yapo matatizo mengi ya kiutendaji ambayo bado yanahitaji ufumbuzi. Ukifuatilia taarifa za ukaguzi za hesabu za serikali za mitaa, utakubaliana nami kuwa hapo alipo bado anahitajika sana. Tumpe nafasi na aungwe mkono.
 
Huyu Bwana ni mchapakazi mzuri sana.Alikuwa Dar-es Salaam(sikumbuki Halmashauri gani), Akahamishiwa Singida kuwa Katibu tawala wa Mkoa then akaenda Morogoro.Mwaka jana aliteuliwa kuwa k/katibu mkuu kabla ya kuwa katibu mkuu kamili wa Wizara ya Maendeleo ya jamii na watoto na sasa ni Katibu mkuu TAMISEMI.Huko kote alikopita amekuwa mchapakazi mzuri sana kwa mfano mkoa wa singida na Morogoro alihakkikisha kwamba analipa madai yote ya malimbikizo ya wafanyakazi wa AFYA, amesimamia vizuri sana ujenzi na uboreshaji wa Hospitali za mikoa-Singida na Morogoro ndani ya muda mfupi sana....Ndipo Mheshimiwa Raisi akamwona na kumpandisha cheoBwn. Hussein Katanga!! nadhani anafaa kuchukua kiti cha Blandina Nyoni
Yale yaleeeeeeee..... aisifiaye mvua........
 
Katanga ni safi sana, anajiamini, anachapa kazi, yupo vizuri ku kichwa, mtanashati na hana mambo ya siasa. Nilijua ndo angechukua nafasi ya Luhanjo
 
Huyu Bwana ni mchapakazi mzuri sana.
Alikuwa Dar-es Salaam(sikumbuki Halmashauri gani), Akahamishiwa Singida kuwa Katibu tawala wa Mkoa then akaenda Morogoro.
Mwaka jana aliteuliwa kuwa k/katibu mkuu kabla ya kuwa katibu mkuu kamili wa Wizara ya Maendeleo ya jamii na watoto na sasa ni Katibu mkuu TAMISEMI.
Huko kote alikopita amekuwa mchapakazi mzuri sana kwa mfano mkoa wa singida na Morogoro alihakkikisha kwamba analipa madai yote ya malimbikizo ya wafanyakazi wa AFYA, amesimamia vizuri sana ujenzi na uboreshaji wa Hospitali za mikoa-Singida na Morogoro ndani ya muda mfupi sana....Ndipo Mheshimiwa Raisi akamwona na kumpandisha cheo

Bwn. Hussein Katanga!! nadhani anafaa kuchukua kiti cha Blandina Nyoni
Hussein Katanga
 
Naunga mkono hoja, huyu jamaa alikuwa MD Kinondoni na wala siyo Ilala kama ilivyoelezwa mwanzo, jamaa ni mchapakazi kweli na ndiye aliyeanzisha (Kinondoni bila uchafu inawezekana)
Nakumbuka siku moja alimuambia Londa wakati huo Londa akiwa Meya wa kinondoni kuwa mchezo wake wa kuchukua waandishi wa habari kila anapoenda na kuamuru walipwe na Halmashauri siyo sahihi na akatamka waziwazi kuwa "next time utatoa za kwako mfukoni"
Baadaye akawapiga marufuku madiwani kushinda kwenye ofisi za Halmashauri na kuwataka wakawahudumie wananchi kwenye kata zao.
Wakamuundia zengwe akahamishwa. Akipewa huyo nitaunga mkono jamaa ni mchapa kazi sana.
Hussein Katanga
 
Katanga ni safi sana, anajiamini, anachapa kazi, yupo vizuri ku kichwa, mtanashati na hana mambo ya siasa. Nilijua ndo angechukua nafasi ya Luhanjo
Mkuu hatimae Ile Ndoto yako ya CS kua Katanga imetimia,Kweli Kama una faa unafaa tu hata ipite miaka.Ulitabiri huyu awe mrithi wa Luhanjo,naona Sasa mama ameanza vizuri Sana hateui Mtu kwa kukurupuka lakini pia nimeaminia anawashauri wazuri na huenda anawasikiliza siyo Kama mzee wa Mimi Sipangiwi na kuteua watu wasiokua na uelewa wowote kuhusu Public Service anzia kwa Ma DED,Hadi CS huyu aliyedumu kwa mwezi mmoja tu.Ilifikia hatua Mtu anateuliwa u DED hata Check no Hana anaenda kuipatia kwenye Halmashaurii anayoenda kuongoza yani kisa tu mtukufu amempenda au amesifiwa na Mtu husika hii ilikua inawavunja Sana Moyo watumishi waliokaa kwenye Utumishi miaka mingi na wenye sifa,Mtu katoka from no where anakuja kua Boss wako hata hajui chochote kuhusu Utumishi wa Umma.

Huu uteuzi wa Katanga is the best appointment ever Hongera Sana mama Samia na Wasaidizi wako hapa mmelamba Dume,na nawashauri Mfate taratibu na miongozo ya Public service katika Kuteua wakuu wa Idara,Taasisi,Vitengo na n.k msiendeshwe na Matamanio yenu au kuwapa kazi Kama hisani au kusifiwa mnawatunuku vyeo muwe fear .Nawatakia Utendaji mzuri wa Kuongoza Taifa hili.
 
Back
Top Bottom