Nampenda sana ila hiki kikwazo kinaninyima raha

RUKUKU BOY

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
1,457
1,662
Hi wakuu poleni na mihangaiko.

Mie ni kijana sijaoa Ila nipo kwenye mahusiano na mdada mmoja, nina kazi maisha yanaenda.

Huyu dada tupo wote more than 1.5 year, kwakweli mtoto wa watu ananipenda, ananiheshimu mno, ananijali, na nimcha Mungu na Mimi nampenda aswaa!

Tumepanga tutaishi wote in near future, Ila kitu kinachoniuma kwa mylove wangu ni mnene Sana, yaani ni chibonge na Mimi nina mwili wa kawaida tu, tukiwa wote utadhani mtu na mdogo wake, Ila najitahidi uyu mrembo apungue lakini yeye hana ushirikiano. yaani kwao wako vizuri anakula hovyo hvyo japo anajua Ni mnene.

Anakula vyakula vinavyo promote body weight kuongezeka, kila nikimuambia ajitahidi apunguze kula hovyo yeye anasema hawezi. Nampenda ananipenda, jamani nifanyeje huyu mtoto apungue uzito maana kadiri anavyokuwa anazidi kuongezeka yeye ata hashtuki.

Msaada wakuu, au nipige chini maana mwanamke mnene sometimes inaboa.
 
Huo mda mliokuwa wote umeonaje utendaji wake katika kutenda dhambi?


kama vyote umeridhika navyo, Hiko kimoja kisikusumbue mkuu, yeyote yule utakayempata lazima atakuwa na lake la kuvumiliwa, naye anakuvumilia kwenye Jambo Fulani.

Huenda angependa anayeweza kumbeba, ona anakuvumilia kimbaombao wewe.


Shaurilo
 
Huo mda mliokuwa wote umeonaje utendaji wake katika kutenda dhambi?


kama vyote umeridhika navyo, Hiko kimoja kisikusumbue mkuu, yeyote yule utakayempata lazima atakuwa na lake la kuvumiliwa, naye anakuvumilia kwenye Jambo Fulani.

Huenda angependa anayeweza kumbeba, ona anakuvumilia kimbaombao wewe.


Shaurilo
Haaaa mtoto anajiheshimu Sana, sio mtenda dhambi Sana, japo naye ni binadamu
 
Pole sana..!
Wekeni ratiba ya mazoezi ya asubuhi au jioni.. kukimbia,kuruka kamba wote..nk

pia mshauri apunguze vyakula vya mafuta na sukari..!

Lakini si ulimpenda akiwa chibonge! why unataka apungue..?
Haaa hakuwa chibonge Kama sahivi, afu tatizo hatuishi wotee
 
Nipe no,yake nijaribu kumshauri njia nzuri ya kupunguza mwili ndani ya ck 3 halfu utaleta mlejesho hapa.
 
Unajaribu kusemaje kwa mfano.
Ni chibonge kama huyu
D93621A0-00B0-4CD1-ABDB-A61D423FD5CD.jpeg
 
Ishi nae hivyo hivyo kama unampenda kweli... ubonge usiwe kikwazo
Jamaaa kaseme anaendelea kunenepa hovyo italeta matatizo ya afya huko mbeleni...mwishoe ata papuchi yenyewe aanze kuitafuta kwa tochi
 
Back
Top Bottom