Nampenda Lakini...?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nampenda Lakini...??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Easymutant, Oct 28, 2010.

 1. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kuna mdada ambaye nimempenda sana na ningependa awe wa kufa na kuzikana kama mambo yangekuwa yapo ndivyo sivyo, mdada ni mfanyakazi anaposition nzuri tu na anajiweza kimaisha,
  kwa muda wa mwaka mmoja sasa nimekuwa na mawasiliano katika kipindi chote hicho hatujafanya wala kuvunja amri ya sita ila romance tumefanya,

  nilitaka kujua historia yake kwa ufupi na aliniweka bayana kwamba yeye ana mtoto wa kike(4) ambaye alizaa na mume wa mtu na anavyodai alikuwa anampenda vizuri na kumtimizia mahitaji yake kama nyumba ndogo yake, nikapenda kujua ni kwa nini ameachana na huyo mtu ambaye ni mume wa mtu na anadai kwamba anampenda na wameridhika? akanambia ukweli kwamba huyo mtu alifariki kwa ajali ya gari akavunjika kiuno toka mtoto wao akiwa na umri wa miaka miwili,

  Sikuishia hapo kwa sababu kama nilivyosema ni mtu ambaye anaweza/angeweza kuwa mke nikaona niendelee na maswali namshukuru pia alinijibu bila kuskip kipengele hata kimoja, nilimuuliza wewe najua ni mdada mzuri na unamvuto hivyo kwa miaka miwili ambayo umekaa bila huyo mtu wako (marehem) ni wazi kwamba unamtu/unatarajia kuwa na mtu mwingine mdada akanijibu ni kweli nilikuwa naye lakini distance zilitupa shida hivyo tukashindwa kuendelea (jamaa alikuwa anakaa Dar yeye Moshi) hapa aliskip some vipengelez...

  katika pilika pilika zangu za kila siku nilikuwa mwanza nikawa nimefikia hotel moja mwanza nikapenda kula samaki tu maana sato niliwamiss kimtindo nikasema nikipata samaki na the lite castle burudaaaani kabisa .. nikaenda mwaloni kuna bar moja wanasamaki wazuri sana watu walikuwa wengi na nikajiatach kwenye meza ambayo kulikuwa na mbaba mmoja like 46yrs hivi .. nae alikuwa anajiburudisha na serengeti bariiiid nikaona kampani imekuwa nzuri sasa tukaanza kuchati nikamwambia mie nimatokea sehm fulani na ninafanya kazi huko ..akanambia kijana hata mie nilishafanya kazi kwenye huo mkoa na bahati nzuri alitaja kuwa ameshafanya kwenye hiyo taasisi ambayo mchumba/mke mtarajiwa anafanya kazi.

  As a gentleman nikamwambia tu pale nina mchumba ambaye nataka Mungu akitujaalia tufunge ndoa
  uzuri anamfahamu huyo dada alikaa kimya mwa muda kidogo yaani hali flani kama anataka kupotezea storry akaanza kunipa story zingine za kuwa ametoka kakola (Kahama mining huko) aah! nikaona huyu vipi mbona tulikuwa kwenye line moja lakini ananitoa tena? nikaona isiwe tabu bado tunapiga mtungi kidogo kidogo nitamrejesha tu kwenye reli huyu..

  nikaanzisha story tena kwa swali la kizushi bro vipi hutaki niingie kwenye chama cha mavuvuzela? (waliioa na kuolewa) akacheka kidogo then akasema bwana mdogo ngoja nikwambia kuona ni vizuri sana lakini unatakiwa uchunguze niwapi unakwena kuoa akaleta mfano ule wa mababu zetu ambao walikuwa ukitaka kuoa wazazi ndo wanchukua jukumu la kuichunguza hiyo familia unakotaka kwenda kuoa, na walikuwa na maana yao kwa sababu kama familia ina historia ya ukoma watakwambia ...lakini kwa kizazi chenu mambo yamebadilika sana hivyo muwe makini sana..

  Alinipa ukweli wa huyo dada kwamba kila mwanaume anayemtokea na wanakuwa katika mahusiano mazuri huyo mwanaume anakufa na mbaya zaidi wote wanakufa kwa kuvunjika viuno wameshakufa wanaume watatu hadi sasa kwa ajali za gari na wanavunjika viuno, kama unakumbuka huyo dada alishawahi kuniambia huyo aliyezaa nae amefariki kwa ajali ya gari na huyo wa pili kulingana na huyu brother amefariki kwa ajali pia na watatu nae kafariki kwa ajali pia ...

  Mnishauri wanajamii mie kiuno changu nadhani bado nakihitaji na nipo kidogo confused kwa sababu mdada nampenda ila ninataka kumuuliza ukweli wote kama atakuwa yupo tayari kuniambia A-Z maana hizi pingu za maisha ambazo mnafungwa ni noma mazee...sio za kuingia kichwa kichwa..

  Asanteni
   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mmh we bwana wewe uko juu km stor ya kweli uku chini km ni tungo bini simulizi vileeeeeee...!!!
  heeee km ni kweli pole jaman
  kaa nae chini dada akusimulie kwa kina juu ya wapenz wake wote na historia zao kwa undani
  km unamuda na unampenda kweli take time kwenda kwao na kuchunguza.
  zungumza na watu wanaojua familia yao kwa undani wakupe inn n out ya familia yao...
  kwa sisi tunaoamini ni kwamba kuna familia ambazo zimelaliwa na laana sana yaaan utakuta family hii inazaa vichaa wengi,family hii ina vilema wengi,famili hii ikizaa watoto wote wa kwanza wanakufa so inawezekana pia uyo dada kaandamwa na laana iyo
  EBU FANYA WIMA CHUNGUZA FAMILIA YAO THEN UTAJUA KINACHOMSIBU UYO DADA..usimfunue kwanza fanya subra..chunguza familia chunguza kaka ukweli utaupata
  si issue ukiona km hii laana ipo basi we sepa utampata mwingine
  womensoldiers r many out thr tak yr time 2xplore thm bt usistik apo UTAPOTEZA KIUNO WEWEEEEE shaurirooooooooo!!!!
   
 3. T

  The King JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni mimi naingia mitini maana wazuri na wenye sifa ya kuwa wake wako wengi. Si hali ya kawaida kabisa baadhi ya wanaume aliowahi kuwa nao wanaishia kupata ajali na kufariki. Kama bado unapenda kuchukua jumla jumla basi inabidi uandae lundo la maswali ili kujihakishishia huyo mdada hatakusababisha nawe uiage dunia.
   
 4. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mh!imenishtua kweli kupenda gharama! nionavyo mimi jaribu kumdadisi bila yeye kujua though hatakuwa muwazi sana lkn unaweza kupata picha, ya kama aliwahi kuwa na wanaume 3 na wote kufariki ktk mazingira yanayofanana. Ukishaprove hilo, kwakuwa ni watu ambao mnajichanganya na jamii naamni unaweza kupata mazingira mengine ya kupata ukweli,vinginevyo:nono::nono::nono:
   
 5. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Na inawezekana kabisa ndo maana yule baba wakati umeanza kumwambia habari za mchumba alibadilisha chanel ghafla,labda alishtuka akikumbuka na historia ya huyo mrembo wako,tafakari,muombe Mungu,chukua hatua.
   
 6. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Muokoke muende kanisani mkaombewe
   
 7. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Rose ni kweli ila nimeivurunda vurunda na kutoiweka live sana iwe hivyo kwa sababu muhimu but very true.
   
 8. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  kwani akimfunua kuna ubaya gani?mwache afunue, akija kuona haifai atamfunika tu!
   
 9. Egyps-women

  Egyps-women JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole sana endelea kufanya uchunguzi wa kina kuna dada mmoja hapa naye kila mtu anamuogopa kwa maswaiba kama hayo ila yeye ni mtu wa hukooooooooooo kwa wanchanki na wanchoki :tape:
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ukinywa mchuzi tu tayari umekula nyama au sawa sawa na aliye kula nyama.
   
 11. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  amfunue afu AVUNJIKE KIUNO?
  we vp bwana unataka mwenzio atembee km dig dig bila kiuno?toka zako uko
  usimfunue mwaya ...tunza kiuno babu oohh ohh mademu wapo weeeeengi lakini KIUNO KIPO KIMOJA...
  usimfunue uvungu b4 aujachek family history...izi mambo zipo babu
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii inatokea sana pindi mwanamke anapo kuwa na gundu inabidi akasafishe nyota.

  Kuna sehemu flani hivi kuna mwanamke mrembo kweli kweli kwenye kampuni hiyo lakini kila mfanyakazi akimtokea tu na akamega basi jamaa hana maisha marefu na kazi anaweza akadumu nae mwaka anafukuzwa kazi imetokea jamaa kibao wanao mega huyo mwanamke wanafukuzwa kazi inakuwa kama nuksi flani hivi nyota ya mwanamke huyo ni mbaya baadae ikabidi wamtimue yeye kazini hii inatokea sana
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Jamaa kesha kula mate tayari hapo hakuna tofauti na yule aliye kunywa mchuzi akaacha nyama jamaa nae tutegemee kuvunjika kiuno
   
 14. b

  bahati stanz Member

  #14
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu sio mtu, nahisi ni jini, kama sio jini basi ni mtu mwenye mapepo, nashauri kama ni wakristu muende kwa watumishi wa Mungu mpate maombi , kama islamic muende kwa mashehe mpate dua nzito, hapo mbichi na mbovu zitajulikana. Mungu awe nawe.
   
 15. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  ana ndege huyo dem sepa haraka sana au kama utaamua okaka kabisa nae umpeleka akaombewe.
   
 16. Tanzanite1

  Tanzanite1 Member

  #16
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asee hii kali lakini inawezekana uyo baba alipigwa kibuti na uyo binti sasa anataka amkoseshe bahati ila chukua tahadhari 'llinda kiuno' usinaniliu naye kamuulize kwanza ukweli wa mambo nashangaa lakini inakuaje hamna mtu ata mmoja mji huo anaoishi binti aliye wahi kukutonya ilo make friends na watu wanaomzunguka utapata habari kama kweli ziko manake tunavopenda kuongea
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ndugu nakushauri ujikalie kando tu. Maumivu ya kumpenda yataisha na utapata mwingine
   
 18. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Baba hawakukosea waliosema Lisemwalo lipo kama halipo...........Hapo ni kukimbia tu mkuu,na nasisitiza kimbia wewe wala usigeuke nyuma ukichelewa utajikuta umeoa mchawi shauri yako!
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  jamani nyie ina maana yeye aliumbwa asiwe na mwenza?
  Hebu mpeni ushauri wa matumani akate shauri yeye na mwenza wake wamrudie mungu yeye ni muweza wa yote
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kiuno
   
Loading...