Nampenda lakini nahofia atanichukuliaje?

Fala kweli wewe.. Wewe upo kwenye banda lako la m/pesa umejuaje kuwa anajielewa au hana muda na watu! Sema na muda wewe, akifika kwenye kibanda chako anaweka hela au kutoa na kusepa.. Ana muda sana na hao wanaompa hela.. Ngedere kweli wewe, mwelezi hisia zako, kama na hivyo vikamisheni unavyopewa huko voda au tigo havijayeyuka..

fanya kazi mdogo wangu
jamaa povu limekutoka kama umenichangia mtaji aseee!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema unafanya kazi gani?
habari wa JF,

kama kichwa cha habari hapo juu kinavyosema kuna dada mmoja kwa jina Nancy, ni mteja wangu wa nguvu ktk huduma za simu pesa(miamala). Kila siku lazima aje aweke/kutoa/kutuma si chini ya mil.3 hadi 5. sasa basi kutokana na jinsi alivyoumbika, rangi yake, sauti yake na jinsi alivyo mkarimu kiukweli nimempenda na naitaji awe wifi/shemeji yenu.

Lakini ninachohofia ni kuwa endapo nitamuelezea hisia zangu huenda atasusa kuja tena kunichangia miamala, ama akanichukulia kama mtu ninayetumia kazi yangu kujinufaisha/kuwarubuni wadada. Kiukweli ni mdada anaejielewa kaenda hewani, hana mda na watu yaani yupo busy na mambo yake.

Tangu nimejitambua sijawahi kumwogopa wala kuwa domo zege kwa mdada yeyote ila kwa huyu dada sijui tuu nimekuwaje.. ila hofu yangu kubwa ni kupoteza mteja ambae mchango wake ktk biashara yangu ni mkubwa mno..

Ushauri jamani kipi nifanye kwa huyu bi dada, nijitose tu liwalo na liwe ama nijizuie ili nisipoteze uteja nae??

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom