Nampenda huyu dada lakini anampenda rafiki yangu

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,576
18,894
Wasalaam members wenzangu
mi nikijana mwenye miaka 23 nilimpenda dada mmoja mwenye umri wa miaka 24.Huyu dada alinivutia kwa vitu vingi Sana mpole, ana macho mazuri,ana voice yake ni nzuri Sana lakini pia ni mzuri sana na nikatamani niwe closer nae ili I we rahisi kumtongoza lakini pia huyu dada alikuwa rafiki wa rafiki yangu pia.Nakwel nilifanikiwa kuwa closer na huyu dada lakini katika maongezi yetu lazima jina la rafiki yangu litakuwepo kwake kulitaja.

Hii imekuwa ikinikasirisha Sana na kuniumiza hata Kama pia nikikutana nae lazima amuulizie rafiki yangu ukiachana na Hilo sisi wengine hatupi mkono katika salaamu tofauti na rafiki yangu hii imenifanya ninun'gunike niseme kimoyo moyo laiti angejua tabia ya kupenda ovyo wasichana aliyonayo rafiki yangu asingeonesha kumpenda tena.kuna siku moja wakati tukipiga story na huyu dada alipata homa ya gafla Sana ambayo ilikuwa Kali Sana nikabaki nifanyanye maana nilikuwa Sina hela ikabidi nikabidi nimpigie simu rafiki ninaywmuamini anikope hela na kweli nikatumiwa 30000 na jamaa yangu niliyoomba nikabidi nimpeleke hospital kwa ajili ya check up baada hapo tukaambiwa ana umwa Nini ikabidi nimpeleke kwake na kwasababu nilikuwa sipajui akanielekeza mpaka sehemu anayoishi hiyo sehemu alikuwa amepanga chumba kizima na pia nilimnunulia matunda pamoja na dawa akasema Asante nipo na me nikaondoka.

Tukio Hilo liliongeza ukaribu wangu na yeye tukawa tunachart Mambo mbalimbali. kuna sikunyingine wakati nimekaa sehemu moja akatokea mtu akanifumba macho nikazani huyo mtu atakuwa zuwena ambaye amekuwa akinishobokea Sana na me nilikuwa simtaki ndipo nikasema zuwena acha izo akanifumbua macho kumbe akuwa zuwena Bali yule dada ninayempenda akaniuliza zuwena ni Nani? Nikamjibu ni mwanafunzi mwenzangu wa chuo ni kweli alikuwa mwanafunzi mwenzangu na wa wote tulikuwa mwaka wa pili na Wala sikumdanganya ila siku zinapozidi kwenda Nina ona Kama ndo wakati sahihi kumtongoza ila tatizo langu me nilikuwa Domo zege kila nikipanga Leo naona inapita siku Bila kumtongoza na ukizingatia huyu dada ni mashalah alafu ni mtoto wa Tabora ninaweza nikakuta mwana si wangu.

Siku moja inabidi nimuombe nimtoe beach ili I we siku ya kumtongoza na kwasababu nikaona Kama kidogo kunamwelekeo wa kunipenda nikabidi nitumie trick ili aje maana huyu dada alinitoleaga nje out zangu mbili nikamwambie tumepanga kwenda beach me na rafiki yangu lakini tukaona si vizuri tuwe pekee yetu Basi tukaona ni vizuri na wewe rafiki yetu uje cos Leo ninamini upo free maana hiyo siku ita kuwa j'pili lakini kumbuka rafiki yangu ajui chochote na Wala sikumwambia tuende beach j'pili kiufupi ajui chochote nilitumia hiyo trick cos nilijua huu dada anampenda rafiki yangu na ni kweli akakubali kuja hiyo siku.

Na kweli tukakutana ila aliniuliza mbona hayupo rafiki yako nikamdanganya Kuna sehemu amepitia atakuja baadae kwa hiyo tukafika beach tutaanza kuogelea na jinsi nilivyomuona kwenye maji nikajua ajui kuogelea nikamuona anaboya akaniambia nairusha hili boya ukilipata utakuwa mshindi kwasababu me nikidume ikabidi nioneshe Kama me ni fund wa haya Mambo kwa mtoto mzuri.Nikaanza kuogelea kuifata hiyo boya nikajikuta ninaenda maji marefu Sana na boya linazidi kwenda nikaanza kula vikombe nilivyoona Mambo yanazidi kwenda kombo nikapiga maji ovyo ile hall huyu dada akabidi anifuate kumbe huyu dada ni fundi wa kuogelea seems tu alikuwa ananichora ndipo akanisaidia kile kitendo Cha kunishika tu niliona km nimeshikwa na malaika nilijisikia raha kwelkwel badae tukatoka alikuwa ananicheka kwa ile moment iliyotokea tukaa sehemu fulani karibu na beach nikasema moyoni hi ndio last chance ninaweza nisipate Tena nakumba hi ndio ilikuwa first kwangu kumtongoza msichana before ya hapo niliwahi kuwa na wasichana wawili tu ambao nilipata mteremko wao ndio walionitongoza yaani ilikua ni acheche niliweza kumtongoza ila alinijibu jibu atanipa siku nyingine baada ya hapo ilipita wiki mbili hiv akunijibu nikaona hapa nimekataliwa kisela ila wiki ya tatu nakumbuka ilikuwa j'5 nilipokea message yake inasema "baada ya kukaa kwa muda nimeweza kutafakari ombi lako kwa umakini na kukusoma nimejua we ni mtu sahihi kwangu na kwa maisha yangu ingawa moment fulani ulinidanganya kuwa utakuja na rafiki yako beach ila najua ulifanya hiv cos ulijua ninampenda rafiki yako na nimejua hili nilivyompigia simu rafiki yako na nikimuuliza kuhusu hilo lkn najua umefanya hiv cos unaipenda na nikujua vema when tulivyokuwa karibu nimegundua vitu vingi kuhusu wewe ni nakupenda na ninakutakia siku njema".

NB: Hadi hiv Sasa tuna mwaka mmoja kwenye relationship yetu na tunapendana Sana.Tittle yangu ya mada nimeiweka ktk namna tofaut na namna ambavyo watu wangefikiri.
 
Back
Top Bottom