NAMNA YA KUTUMA VIAMBATANISHO

GIPAMA

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,103
541
Wakuu habari za majukumu, naomba kuelimishwa kitu kimoja, unakuta tangazo la kazi linasema mwombaji atume barua, CV, vyeti vya elimu na cheti cha kuzaliwa.

Je, katika utumaji, kila kiambatanisho, unakituma katika file lake, ama vyote unaweka katika file moja!?

Asanteni.
 
Barua iweke peke yake kisha vingine ambatanisha vyote katika faili moja ukianza na CV,kisha background yako ya elimu,kisha vyeti ulivyohitimu ktk background ya elimu yako na hicho cha kuzaliwa.
 
Wakuu habari za majukumu, naomba kuelimishwa kitu kimoja, unakuta tangazo la kazi linasema mwombaji atume barua, CV, vyeti vya elimu na cheti cha kuzaliwa.

Je, katika utumaji, kila kiambatanisho, unakituma katika file lake, ama vyote unaweka katika file moja!?

Asanteni.
Wenye kujua wengine hapa tunaombeni elimu.
 
Wenye kujua wengine hapa tunaombeni elimu.
Sio kitu Cha kukuumiza kichwa sana na hakuna mtu anaconcentrate na ishu ndogo Kama hyo na kiufupi haina formula maalum bali inabidi ufuate maelekezo yaliyotolewa ktk tangazo la kazi kwa sababu waajiri wengine wanaspecify kila kitu jinsi ya kufanya.
Lakini Mimi nitakupa mbinu zifuatazo ili usichanganyikiwe.
1.Kama kwenye tangazo hawajafafanua vizuri jinsi ya kuattach viambatanisho Basi weka barua kwenye file la peke yake,CV file la peke yake,halaf vyeti vyote viunganishe kwenye file moja la peke yake.
2.Zingatia maelekezo coz Kuna waajiri wengine huwa wanataka attachments zote ziwe kwenye faili moja yaani barua,cv na vyeti viwe kwenye faili moja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom