Namna ya kutengeneza Batiki, dawa za chooni(Sabuni) na mishumaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namna ya kutengeneza Batiki, dawa za chooni(Sabuni) na mishumaa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by xkamzy, Sep 23, 2012.

 1. x

  xkamzy Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Wadau!
  Mtu yoyote mwenye uelewa juu ya utengenezaji wa Batiki, dawa za chooni(Sabuni) na mishumaa please naomba anisaidi hatua zake ziko vipi??
  Nawasilisha!!

  =============================================

   
 2. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hii ingefaa kama itapelekwa kwenye jukwaa la ujasiriamali. Mods, msaada tafadhali.
  Mkuu xkamzy ukijibiwa tutafaidika wengi.
  Asante kwa kuuliza kwa niaba ya wengine. Barikiwa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Hizo kozi zinztangazwa kila siku kwa ada ya sh. 10,000 tu. Ziko sponsoured na mashirika mbalimbali. Sikiliza WAPO FM utawasikia hao jamaa.
   
 4. j

  jotashi New Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello,kajiandikishe pale country side Motell,
  pale Kibaha mail moja, Dr Didasi Lunyungu anafundisha
  kuanzia tar 10/10-13/10/2012.
  Kujiandikisha elfu 10 tu,anafundisha vitu vingi,nenda utafaidika sana.
   
 5. Super H

  Super H JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 1,004
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hiyo na mimi ninahitaji sana kujifunza hasa sabuni ila mimi ninaishi mwanza kama kuna yeyote anayeweza kunisaidia asisite.
   
 6. m

  mdunya JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Piga simu 0717428105
  Kiseke kwangu vipi? Wameweka lami?
   
 7. K

  KICHWA BOGA Member

  #7
  Mar 31, 2015
  Joined: Apr 27, 2014
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  BATIKI ZA MASHATI na TSHIRT
  Kwa kufuata sheria ya kuu ya tie dye ambayo inakutaka kukunja malinda kwa mtindo wa nje ndani au mbele nyuma, hata kwa nguo yoyote iwe tshirt au shati utatakiwa kukunja kwa mtindo huo kutegemeana na ubunifu wa ua unalolitaka. Kisha utafunga kwa kamba na kuchovya kwenye rangi iliyoandaliwa kama hapo juu.

  MIKUNJO MBALIMBALI YA TSHIRT
  DUARA
  Ambapo unakunja katikati kisha unaweka alama namna hii.

  1.png
  kutengeneza malinda kama inavyoonekana katika picha hii hapo chini.

  2.png
  Kisha funga sehemu husika ambapo patapata rangi. Angalia picha hii.

  3.png

  Kwa picha na maelezo zaidi, tembelea CHANZO: ISHI MAISHA YAKO
   
 8. K

  KICHWA BOGA Member

  #8
  Mar 31, 2015
  Joined: Apr 27, 2014
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ujuzi sasa ni hazina
   
 9. CHAULA RICH

  CHAULA RICH JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2015
  Joined: Jan 8, 2015
  Messages: 3,901
  Likes Received: 692
  Trophy Points: 280
  ubarikiwe kwa kutokuwa mnyimi wa maarifa.
   
 10. A

  Adm Senior Member

  #10
  Apr 2, 2015
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante sana kwa elimu hii, Mimi mwenyewe nipo kwenye huo mpango wa kutengeneza batiki.
  Naomba anaefahamu wapi nitapata malighafi za kutengenezea batiki anisaidie Mimi nipo Dodoma mjini, nimeenda sido wamesema huwa hawauzi na nimejaribu kuulizia madukan nako vivyo hivyo. Naomba msaada kwa hilo
   
 11. Evelyn Salt

  Evelyn Salt JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2016
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 45,055
  Likes Received: 31,868
  Trophy Points: 280
  Njoo nkufundishe
   
 12. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2016
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Miss Salt heshima yako.
  Ningependa sana kujifunza kutengeneza dawa za choo (disinfectants ) sabuni ya maji kama termol kwa ajili ya usafi wa nyumba na nguo na dawa ya kusafisha tiles na sink.

  Natanguliza shukrani
   
 13. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2017
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  hii ni batiki ya mishumaa,
  njoo pm tuanze kufungua kiwanda.

  .......................

  KUTENGENEZA BATIKI

  MAHITAJI:

  1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.

  2.Sponji zenye urembo mbalimbali.

  3.Brash kubwa/ndogo.

  4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.

  5.Sufuria.

  6.Vitambaa vya mpira.

  7.Misumari midogo.

  8.Jiko.


  MADAWA:

  1.Sodium hydrosulphate.

  2.Caustic soda

  3.Mshumaa.


  KAZI ZAKE:

  1. Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.

  2. Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.

  JINSI YA KUTENGENEZA.

  (a) JINSI YA KUGONGA MISHUMAA:

  Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoe kidogo. Andaa kitambaa cha pamba (cotton) na kukitandika mezani, chovya kibao chenye picha kwenye mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo. Endelea kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.

  (b) JINSI YA KUWEKA RANGI:

  Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka sita. Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate vijiko vinne mpaka vitano. Changanya na maji ya moto,weka rangi kijiko kimoja. Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu. Tumbukiza vitambaa vya vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa dakika kumi mpaka kumi na tano. Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye kivuri ili mshumaa usiyeyuke.

  (c) KUWEKA RANGI YA PILI:

  Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi tu. Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza,maji,mudani uleule,

  Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule.Pima rangi kwa kufuata hatua zilezile. Tumbukiza vitambaa vitatu,geuza kwa mda uleule kisha anika.

  (d) JINSI YA KUTOA MSHUMAA:

  Chemsha maji yachemke vizuri,changanya na sabuni ya unga jikoni,tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa,geuza kwa mti,suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji.

  PIGA PASI TAYARI KWA KUUZA.
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2017
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Je, ulifanikiwa kupata hiki kitu rafiki?
  Kama bado na unahitaji wasiliana na mimi.
   
 15. madam boss

  madam boss JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2017
  Joined: Aug 19, 2017
  Messages: 648
  Likes Received: 674
  Trophy Points: 180
  Habari. Nimependa Sana somo lako

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
Loading...