Namna ya kutambua habari na taarifa uzushi

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
20210309_092807_0000.png


Mitandao ya kijamii imejitokeza na kuendelea kuwa vyombo vya kusambaza habari na taarifa mbalimbali na kwa mifumo mbalimbali. Ili kupata habari na taarifa zilizo sahihi, watumiaji wa mitandao ya jamii wanapaswa kujilinda dhidi ya habari na taarifa za uongo na uzushi. Watumiaji wanaotegemea mitandao kama vyanzo vya habari au taarifa wanaweza kutambua iwapo habari na taarifa hizi ni za uongo, uchochezi,uzushi au za kutusi watu wengine. Kuna namna za kugundua iwapo habari ni ya ukweli au la.

1. Kuwa na mashaka na vichwa vya habari vyenye mbwembwe: Habari nyingi za uongo zinakuwa na vichwa vya habari vilivyoandikwa kwa maneno na mpangilio unaoonyesha mbwembwe. Iwapo utaona kichwa cha habari chenye maneno ambayo kwa harakaharaka unashuku ukweli wake, kuna uwezekano mkubwa kwamba habari hiyo sio ya kuaminika.

2. Angalia vizuri anwani ya tovuti inayotumika: Kila tovuti ina anwani inayotambulika kimataifa na inaanza na herufi ‘www’. Angalia kwa makini anwani ya tovuti yenye habari. Iwapo habari iko kwenye anwani ya uongo au ambayo imeghushiwa ni dhahiri kwamba ni ya uongo. Mitandao mingi yenye habari za uongo inatumia anwani ambazo kwa haraka unaweza kudhania kwamba ni za mitandao ya habari inayoaminika. Ukiona hili, tembelea anwani ya uhakika na linganisha na ya mtandao wenye habari unayoishuku.

Chunguza chanzo cha habari: Hakikisha kwamba habari imeandikwa na mwandishi ambaye unamwamini kwamba ana sifa ya kuandika ukweli. Kama habari inatokana na taarifa za taasisi ambayo huifahamu, chukua hatua za kujiridhisha.

4. Angalia usanifu au mpangilio usio wa kawaida: Tovuti nyingi za kughushi zinakuwa na mpangilio wa maneno na usanifu usio wa kawaida. Kuwa macho ukiona hizi dalili.

5. Angalia vizuri picha: Mara nyingi habari za uongo zinakuwa na picha za kawaida na za video ambazo zimechakachuliwa. Inawezekana picha au video vikawa ni vya kweli lakini vikawekwa kwa mpangilio ambao unaleta maana tofauti na ile ya awali. Ukiona hili tafuta chanzo cha picha ili kuhakikisha ilikotoka.

6. Kagua/chunguza tarehe: Habari za uongo zinaweza kuwa na tarehe ambazo hazina mantiki au hata tarehe ambazo zimebadilishwa.

7. Thibitisha vyanzo vya habari: Chunguza vyanzo vya mwandishi wa habari husika ili kuthibitisha uhakika. Habari ambayo haina maelezo ya kuthibitisha uhalisia wake auinanukuu wahusika ambao hawatajwi ina kila dalili ya kuwa ni ya uongo.

20210309_093736_0000.png


8. Linganisha na taarifa za vyombo vingine: Iwapo hakuna chombo kingine chochote kinachotoa taarifa hiyo, ni dalili kwamba habari hiyo ni ya uongo. Habari inayoandikwa na vyombo vingi ina kila dalili ya kuwa ya kweli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom