SoC01 Namna ya kusherehekea siku ya kuzaliwa iletayo hamasa mpya ya maisha

Stories of Change - 2021 Competition

Ntiyakama

Member
Sep 19, 2021
32
37
Baada ya kukumbuka kuwa kesho ni siku yake ya kuzaliwa; alikopa pesa, akafanya sherehe (birthday party) na baada ya sherehe hakuna alichowaza kingine zaidi ya namna ya atakavyolipa deni!

Anayekupenda hakumwagii maji, atakumwagia upendo ulio sheheni baraka, shauri jema, makanyo, maelekezo, pongezi / sifa unazo stahili na kukosoa kenye nia ya kurekebisha; ili uwe bora zaidi mwaka huu mpya kuliko uliopita

SIKU SABA KABLA;

Andaa mazingira ya kuwa na utulivu katika siku zitakazo fuatia baada ya hii; punguza/sitisha kabisa matumizi ya simu, punguza/sitisha kabisa matembezi yasiyo lazima, punguza/sitisha kabisha shughuri ambazo si muhimu sana (delegate if possible).

Tengeneza mazingira ya utulivu wa mwili pia fikra zako.

SIKU SITA KABLA;

Zitafakari hatua zako, ulizo tembea kwa mwaka mzima wapi umefanya vyema, wapi hajafanya vyema, wapi ulikwama sababu ya uzembe, wapi ulikwama sababu ya kukosa maarifa, maarifa yapi ulikosa, watu wa namna gani uliwahitaji zaidi, watu wa namna gani uliambatana nao zaidi, watu wa namna gani wamebadilisha maisha yako, nini ambacho huna na ulikihitaji zaidi, nini ulichonacho na hakikuwa na matumizi kwako.

Kwa kifupi wapi ulikuwa, wapi upo na wapi unatazamia kuelekea.

SIKU TANO KABLA;

Usizisahau, zikumbuke na zitafakari changamoto ulizopitia kwa mwaka huu unao-umaliza; zitafakari katika namna itakayo kupatia mafundisho.

Tafakari kwa nini zilitokea, nini kilikuwa chanzo chake; wewe mwenyewe, mazingira yako au watu wanao kuzunguka?

Nini kilikuwezesha kustahimili katika changamoto hizo? (kitambue na kizingatie; ni nguvu yako).

Andika mambo yote uliyojifunza kupitia changamoto ulizozipitia katika kipindi chote cha mwaka mzima.

Usipoteze muda wako kulalamika; “asingalikuwa flani/kisingalikuwa kile – nisingelikuwa hivi/nisingelikuwa hapa,” haitakusaidia, muda ni mchache kutosha kulalamika, tumia kilichopo mikononi mwako kusonga mbele, usipoze muda mwingi kufikiria ulichopoteza.

SIKU NNE KABLA;

Zitafakari nguvu zako na namna ambayo zimekusaidia kufika hapo ulipo, yatambue na yape thamani mafanikio uliyo yafikia.

Andika mambo yote uliyofanikiwa kayafanya vyema (hata kama ni kwa kiwango kidogo) tafakari kwa namna gani uliyafanikisha hayo, nini kilikuwezasha kuyafanya hayo yafanikiwe (andika na zingatia ipo nguvu ya ushindi wako hapa).

SIKU TATU KABLA;

Wasamehe wote walio kukosea kwa mwaka mzima unao umaliza, waombe msamaha wote uliowakosea, jisamehe mwenyewe pia kwa yote ambayo yanakudhoofisha kila uyafikiripo na kujiona kuwa wewe ni sababu ya hayo kutokea.

Msamaha utakupa mwanzo mpya, mwanzo mzuri, wenye hamasa, kutia moyo na kukuhamasisha. Msamaha utakuapatia kumbukumbu zizozo na maumivu. Tubu | Ungama dhambi zako.

“Msamaha ni kumbukumbu zisizo umiza”

SIKU MBILI KABLA:

Panga weka malengo ya mwaka wako huu mpya, unataka kubadilisha nini, unataka kufika wapi kiafya, kielimu / kitaaluma, kijamii, kiuchumi, kimaadili na kiimani.

Iko nguvu kubwa mno katika malengo, itakayo kuongoza na kukupa juhudi ya kujituma na kujibidisha zaidi ukitafuta kuyafikia malengo hayo.

Jewekee malengo, jiwekee malengo makubwa na panga mikakati thabiti itakayo kuongoza kuyafikia malengo hayo.

Malengo yanayo fanikiwa:

Ili kutimiza malengo yako, unapaswa kutambua namna ya kupanga malengo hayo.

Sio tuu kusema nataka au natamani kitu flani kitokee, kupanga malengo ni mchakato unaoanza na maono ya kile unachotaka kukifikia na kisha kuna kazi nyingi na ngumu za kufanya.

Zingatia yafuatayo katika kupanga malengo.

∆ Panga malengo yanayo kuhamasisha;

Yafanye na yaone malengo yako kuwa muhimu, hakikisha unaiona thamani katika kuyafikia malengo hayo. Kama unavutiwa kidogo na matokeo ya malengo yako, hutakuwa na nguvu za kutosha kuyapambania.

“kama matokeo ya malengo uliyojiwekea hayakuvutii sana; nguvu za kuyapambania malengo hayo zitakuwa dhaifu.”

Kufanya malengo yako yakuhamasishe, andika kwanini ni ya thamani na muhimu kwako. Jiulize ni kwa namna gani unaweza kuwashawishi wengine ili waone kuwa malengo yako ni muhimu; tumia majibu utakayo yapata kujifariji pale unapoanza kujitilia mashaka au kupoteza kujiamini.

∆ Yaandike malengo yako;

Tabia ya kuandika malengo yako, huyafanya yawe halisi na yenye hisia ya mguso, hautakuwa na sababu kusema kwamba umesahau kile ulicho kiandika.

Andika malengo yako na andika mikakati uliyo jiwekea ili kuyafikia malengo hayo. Yasome mara kwa mara.

∆ Weka mpango wa matendo;


Mara kadhaa wengi husahau kabisa kuweka mkakati wa kimatendo kuyafikia malengo hayo. Utekelezaji wako wa malengo ya mwaka mmoja yamo katika shughuri unazozifanya ndani ya kila saa moja, siku, wiki na mwezi mmoja mmoja, hakikisha haupotezi hata siku moja; kwa kufanya hivyo utajichelewesha zaidi kuyafikia malengo yako. Malengo pasipo matendo yatabaki kuwa ndoto pekee.

∆ Baki na malengo yako;

Kupanga malengo ni swala endelevu, pamoja na malengo mapya unayopanga kila siku na kila wakati; jijengee katika kumbukumbu zako tabia ya kubaki katika njia kuyaelekea malengo yako ya awali (msingi). Pata muda wa kuyapitia malengo yako (uliyo yaandika) kila mara.

Weka malengo katika kila unachokifanya, weka malengo ya saa, siku, wiki, mwezi, mwaka, miaka mitatu, miaka mitano, miaka kumi ijayo na malengo ya maisha yako kwa ujumla wake. Andika na yasome kila mara na ukiyafanyia kazi.

Zingatia;

Huwezi kuwa na malengo dhabiti ya mwaka mmoja kama huna malengo imara na yenye mpango sahihi wa kiutekelezaji katika kila saa, siku, wiki na mwezi.

Weka malengo ya muda mfupi, yatekeleze na pima namna yanavyo kujengea msingi dhabiti kuuelekea utekelezaji wa malengo yako ya mwaka mzima. Usianze na makumi kabla ya mamoja.

SIKU MOJA KABLA;


Pata muda mwingi wa kukaa pweke, penye utulivu mkubwa zaidi (meditate), fanya malejea ya mambo uliokuwa ukiyatafakari kwa siku tano zilizopita.

Pumzika kisha andaa namna yako ya kuisherekea siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwako (narudia; “namna yako ya kusherekea”)

SIKU YA KUZALIWA;

Pumzika
, furahi kwa namna ifaayo (zingatia usalama wako), wasalimu ndugu, jamaa na marafiki wengi kwa kadiri utakwavyo weza kufanya; usisahau kuwasalimu wale ulio wasamehe, pata muda wa kukaa pekeako mahala tulivu.

Tafakari kwa muda katika ukimya kisha yasome taratibu na kwaumakini malengo yote uliyo yapanga na kuyaandika juzi, jiahidie kuyatekeleza na kuwa mwaminufu katia hilo.

Mshukuru Mungu kwa mwaka uliopita na zawadi ya mwaka mwingine kwako, unayo kila sababu ya kufanya hivyo; toa zaka (usimwibie Mungu) wasaidie walio wahitaji (sadaka ya shukrani), muombe Mungu baraka kwa ajili ya mwaka huu mwingine wa maisha yako. Pumzika mapema.

“Sherehe (birthday party) kwa mtu mzima, inamaana sana kama inaleta hamasa ya uelekeo mpya na bora zaidi ya uliokuwepo.”
 
Back
Top Bottom