Namna ya kupika Pilau

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,568
16,903
Mahitaji

1)nyama/kuku
2)mchele kg 1
3)vitunguu maji 3 vikubwa
4)vitunguu thomu 1 kidogo
5)pilipili manga kidogo
6)uzile 1(bizari ya pilau) tbsp
7)mdalasini kijiti 5 vikubwa au kama ni wa unga 1 tbsp
8)hiliki 15
9)zabibu kavu kiasi

Namna ya kutaarisha

1)kata kata nyama/kuku then add maji saga kitunguu thomu na tangawizi tia na chumvi kiasi na uchemshe hadi viwive
2)weka mafuta robo kikombe kwenye sufuria safi weka jikoni hadi mafuta yawe moto then tia vitunguu maji ambavyo umevikatakata vikaange hadi viwe brown
3)weka mdalasini hiliki uzile zabibu na pilipili manga then changanya kwa dakika 2
4)weka soup yako pamoja na nyama/kuku kwenye mchanganyiko wako visubirie vichemke kwa dakika 5
5)add maji kulingana na mchele wako unavohitaji ili uwive vr
6)weka mchele wako then funika hadi uwe umewiza
7)then waweza kuutia kwenye oven kwa dakika 10 ili ukauke vizuri

8)pilau tayari kwa kuliwa
 
Pika mpenzi wee...uje uniambie imekua tamuje?
Next time ntakuekea iranian rice.
weka mwaya nmepika kaja rafiki yangu kabeba na kubeba teh af imeisha.
weka bana. me chapati napenda ila zinatoka pembe saba! zinakuwa lain sema ndo hayoo mapembe sasa! naishiaga kununua zile tayari nakuja kukaanga tu! lol
 
Usijali ntakuekea.....jaribu jaribu hadi zitakua za duara sasa ukinunua za tayari utajua lini kusukuma za duara lol..m
 
Ili kuepuka mapembe chukua kontena la round ama bakuli ya plastic utumie kukata. Ukishasukuma mshazari wako unaweka juu yake bakuli unakata around. Sekunde chache tu unapata chapati za hataree! Zile za tayari mbona hopless kabisa?!
weka mwaya nmepika kaja rafiki yangu kabeba na kubeba teh af imeisha.
weka bana. me chapati napenda ila zinatoka pembe saba! zinakuwa lain sema ndo hayoo mapembe sasa! naishiaga kununua zile tayari nakuja kukaanga tu! lol
 
Ili kuepuka mapembe chukua kontena la round ama bakuli ya plastic utumie kukata. Ukishasukuma mshazari wako unaweka juu yake bakuli unakata around. Sekunde chache tu unapata chapati za hataree! Zile za tayari mbona hopless kabisa?!
Thanks dia il do that. zile siyo basi tu tamaa na uvivu. ila kama ni mimi tuu huwa napikaga mapembe yangu!!
 
farkhina, mie bila kukaanga nyama iwe dark sijaenjoy pilau. Utamu wa pilau kwenye nyama iliyokolea viungo. Basi wakati natia thomu, natia na nyama bila mchuzi. Nakaaanga kwanza weeeh, then natia supu kidogo tu na kuifunika. Inakolea rangi. Supu ikikaukia natia mchele, nao naukaanga kiasi. Then natia supu ama maji ya moto kiasi cha kufunika tu mchele. Namalizia kama wewe.

Hebu jaribu uniambie utamu wake ukoje?
 
Last edited by a moderator:
Ili kuepuka mapembe chukua kontena la round ama bakuli ya plastic utumie kukata. Ukishasukuma mshazari wako unaweka juu yake bakuli unakata around. Sekunde chache tu unapata chapati za hataree! Zile za tayari mbona hopless kabisa?!

Hahahahahahaa shosti weee mkalii...kama anatengeza vileja vya round lol
 
farkhina, mie bila kukaanga nyama iwe dark sijaenjoy pilau. Utamu wa pilau kwenye nyama iliyokolea viungo. Basi wakati natia thomu, natia na nyama bila mchuzi. Nakaaanga kwanza weeeh, then natia supu kidogo tu na kuifunika. Inakolea rangi. Supu ikikaukia natia mchele, nao naukaanga kiasi. Then natia supu ama maji ya moto kiasi cha kufunika tu mchele. Namalizia kama wewe.

Hebu jaribu uniambie utamu wake ukoje?

Hahahhahaha lazima inogeee hapo ila si unajua shoga angu mchele mmoja mapishi tofauti?
 
Last edited by a moderator:
Hahaha shosti hii niliifanya wakati nafundishwa kupika na Mama Ngina manake kwetu child labour ilitutoa haswaa. Ukishaadvance unajua. Ili kupata round natural unakuwa unasukuma kila upande na kugeuza geuza. Na ukumbuke unga unanyunyiza kwenye kibao/meza na sio kwenye chapati wala kisukumio.
Hahahahahahaa shosti weee mkalii...kama anatengeza vileja vya round lol
 
Last edited by a moderator:
Usipike mapembe banaa. Unajua presentation ya chakula inaamua bei pia? Tofauti ya pilau ya mama ntilie na ya serena hotel ni vyombo na muonekano tu. Ila utamu uko kwa mama muuza. Lol
thanx dia il do that. zile siyo basi tu tamaa na uvivu. ila kama ni mimi tuu huwa napikaga mapembe yangu!!
 
farkhina, mie bila kukaanga nyama iwe dark sijaenjoy pilau. Utamu wa pilau kwenye nyama iliyokolea viungo. Basi wakati natia thomu, natia na nyama bila mchuzi. Nakaaanga kwanza weeeh, then natia supu kidogo tu na kuifunika. Inakolea rangi. Supu ikikaukia natia mchele, nao naukaanga kiasi. Then natia supu ama maji ya moto kiasi cha kufunika tu mchele. Namalizia kama wewe.

Hebu jaribu uniambie utamu wake ukoje?

swadaktaaa bibie.
Mie napika hivi nakaanga vitunguu maji, kisha vikiwa brown naweka nyama nliyoisha naweka na swaumu na ndimu kisha nafunika. Nyama ikishaiva na kukauka maji naikaaanga haswa ikaangike kisha viungo vya pilau visivyosagwa navikaanga pembeni kwenye kisufuria chake namwagia maji kidogo kisha naweka kwa nyama nakaaanga kwa pamoja mambo yakijipa naweka mchele na maji, viazi na zabibu baada ya mda nafunikia na moto juu[raha ya wali/pilau ufunikiwe juu na moto ] mama wee pilau lake tamu balaaa afu viungo wengi wanajaza matokeo yake pilau linatoka jeusiiiiiii. Raha ya pilau iwe na rangi fulani hivi si jeusiiii
 
Last edited by a moderator:
swadaktaaa bibie.
Mie napika hivi nakaanga vitunguu maji,kisha vikiwa brown naweka nyama nliyoisha naweka na swaumu na ndimu kisha nafunika.nyama ikishaiva na kukauka maji naikaaanga haswa ikaangike kisha viungo vya pilau visivyosagwa navikaanga pembeni kwenye kisufuria chake namwagia maji kidogo kisha naweka kwa nyama nakaaanga kwa pamoja mambo yakijipa naweka mchele na maji,viazi na zabibu baada ya mda nafunikia na moto juu[raha ya wali/pilau ufunikiwe juu na moto ] mama wee pilau lake tamu balaaa afu viungo wengi wanajaza matokeo yake pilau linatoka jeusiiiiiii.Raha ya pilau iwe na rangi fulani hivi si jeusiiii

Umewahi kuchanganya na njegere ama mahindi? Inapendeza zaidi...unatia hiyo mixed vegetables wakati unapamimina mchele.
1383937104925.jpg
 
farkhina nimeshaweka njegere sana linanoga balaaa mwana wee uwe na juice yako aaaaa hapa mate yantoka atiiii ila mahindi mhhhh mi mvivu wa kutafuna
 
Last edited by a moderator:
farkhina, mie bila kukaanga nyama iwe dark sijaenjoy pilau. Utamu wa pilau kwenye nyama iliyokolea viungo. Basi wakati natia thomu, natia na nyama bila mchuzi. Nakaaanga kwanza weeeh, then natia supu kidogo tu na kuifunika. Inakolea rangi. Supu ikikaukia natia mchele, nao naukaanga kiasi. Then natia supu ama maji ya moto kiasi cha kufunika tu mchele. Namalizia kama wewe.

Hebu jaribu uniambie utamu wake ukoje?

Hata mimi napendaje nyama iliyokolea viungo,lakini ikiwa imechemshwa tu na kupikwa pilau huwa sisikii ladha ya pilau kwenye nyama. Dahh ulivyoelezea mpaka mate yamenijaa,naipika kesho hiyo.
 
farkhina nimeshaweka njegere sana linanoga balaaa mwana wee uwe na juice yako aaaaa hapa mate yantoka atiiii ila mahindi mhhhh mi mvivu wa kutafuna

Hahahahahhha mengine yanakua laini sana...
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom