Namna ya Kumbadilisha Mpenzi wako

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,178
14,349
a
Katika mahusiano ni jambo ambalo linawezekana kwa mwanamke au mwanamume kumbadilisha mwenza wake kutoka tabia mbaya kwenda nzuri lakini ni muhimu kuzingatia yafuatayo, unapotaka kufanya jaribio la kumbadilisha tabia mwenza wako usijenge hoja za kumkosoa na badala yake anza kwa kumsifia yale mazuri aliyonayo kwani kwa kufanya hivyo kutamsaidia huyo mpenzi wako kuanza zana ya kujielewa yeye ni nani ,,kwa mfano kama mpenzi wako ni mlevi ukawa unatumia lugha kama kumkebehi na kumdhalilisha mbele za watu ukifikiri kuwa atabadilika inakuwa ni vigumu kwani inawezekana ndiyo kwanza akazidisha.

kinachotakiwa ni kumwambia kwa lugha tamu kuwa mtu kama yeye ambaye ana nguvu na mvuto hapendezi kulewa ,, taratibu ataanza kujielewa na mwisho atapunguza kabisa kama si kuachana nayo, kutumia changamoto za kukosoa kulaumu au kukaripia kama sehemu ya kumfanya mtu kubadilika tabia hakutasaidia mtu kubadilika na inawezekana akaongeza zaidi.tumia lugha tamu kumbadilisha umpendaye.

wengine wanakwama kutokana na kukosa hoja za msingi za kupinga tabia ya mtu na hii inatokana na kutokujiamini ama kusimamia maamuzi wanayotoa dhidi ya wapenzi wao lakini pia ni vyema kuelewa mtu atabadilika pale tu atakapokuwa na ushawishi wa kutosha kwamba mabadiliko anayopaswa kufanya yatakuwa na faida kwake na si vinginevyo
 
ngoja nitafute hata liteja nilichange nione kama litakubali

Bebii taratibu
Na sio umwambie wazi hayo maharufu yako ya bangio yananikera
Mwingine jamaa yake ni mlevi akitaka kumpiga kiss anageuza mdomo
Unamwambia tuu taratibu twende kwanza tukapige mswaki mwambie tuu hata kwa utani toka nile chakula asubuhi sijasukutua meno nahisi mdomo wangu una harufu mbaya twende tukapige mswaki
 
ngoja nitafute hata liteja nilichange nione kama litakubali

Utashangaa siku anakutoa ndani baruti na kukuitia mwizi hadharani. na watu walivyo hawana hiyana watakuangushia kipigo kumbe ni mwandani wake, hahahaaaaaaaaa!
 
bebii taratibu
na sio umwambie wazi hayo maharufu yako ya bangio yananikera
mwingine jamaa yake ni mlevi akitaka kumpiga kiss anageuza mdomo
unamwambia tuu taratibu twende kwanza tukapige mswaki mwambie tuu hata kwa utani toka nile chakula asubuhi sijasukutua meno nahisi mdomo wangu una harufu mbaya twende tukapige mswaki
sawa kaka mapenzi popote huwezi kupata mtu alie perfect 100%
 
Utashangaa siku anakutoa ndani baruti na kukuitia mwizi hadharani. na watu walivyo hawana hiyana watakuangushia kipigo kumbe ni mwandani wake, hahahaaaaaaaaa!

mazingira mnayoishi yanaweza kukufanya abadilike au asibadilike na the way unavyomtreat pia
 
sawa kaka mapenzi popote huwezi kupata mtu alie perfect 100%
nakubaliana na wewe kwa asilimia zote
Maana kusema kuwa utampata mtu unayemtaka na vigezo vyako vyote itakuwa ni issue
Unampata at least ambaye mkiwa pamoja mnabadilishana na kufundishana ndani kwa ndani
 
Unachekesha wewe,, nadhani hujui kuwa eksleta ya farasi n mjeredi.

Hongera kama kwako kila kitu kiko perfect
Na huhitaji somo la kubadilika
Ila kuna watu wamewatoa wenzi wao kutoka kuwa walevi na kuwa wacha Mungu wazuri tena kwa maneno tuu malaini wala si kwa mjeledi kama unavyotaka tuamini
 
nimesema hayo kila siku. hebu tumtafute lolyz, lolyzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz, njoo huku bwana, kuna mambo yanakusubiri

Mkuu afadhali umekuja bana maana watu hawataki kubadilika wanakuwa rigid na hawaamini katika mabadiliko ambayo mengi yanaletwa tuu na maneno laini wala sio mjeledi
 
nakubaliana na wewe kwa asilimia zote
Maana kusema kuwa utampata mtu unayemtaka na vigezo vyako vyote itakuwa ni issue
Unampata at least ambaye mkiwa pamoja mnabadilishana na kufundishana ndani kwa ndani
yaa unaangalia awe na zile sifa za msingi at least avuke boarder yaani 50% then iyo ingine utajitaidi hadi 80% maana mia uwezi kumfikisha then iyo deficit utaichukulia tu ivo ivo ila kuna wengine ni balaa, si unaona hata huku yule MS BAN kibao ila halichange bwana daah
 
Kweli nakubaliana na wewe
Ila tuseme wazi kuwa huwezi mbadilisha mwenzako ndani ya nyumba kw akejeli na dharau
Kila siku unamsimangia kitu hicho hicho tuu
yaani mpaka anakereka
Ila kwa maneno mazuri ya kumtia moyo atabadilika
yale mapungufu ndio ya muhimu katika kuhakikisha kuwa mnafikia lengo la mabadiliko
 
hebu nipe tip hapa kama mpenzi wako ni msaliti utamchange vp?
 
hebu nipe tip hapa kama mpenzi wako ni msaliti utamchange vp?

Kuna kitu katika dhana nzima ya mapenzi kimepungua
Jitahidi wewe mwenyewe kutimiza vile anavyovitaka vile alivyokupendea wakati may be wa kukuaaproach na ongeza juhudi binafsi yaani asipumue kwenye dhana nzima ya mapenzi
tatizo unajua tukishazoeana sana tunajisahau tunaona vitu vingine kama priviledge kwa yule anayepokea na ndo maana wengi wakiwa kwenye ndoa hata dhana nzima ya kukutana inakuwa kama anasa badala ya kitu cha lazima
 
Rocky kumbadili mtu mzima ni kazi sana, unaweza ila asilimia ndogo saana, mtu awezi acha asili yake, anaeza badilika kwa muda kama ni mwanzo wa mahusiano ili akuvutie, with time anarudia lifestyle yake, hiyo naongelea tabia tu ya mtu, ulevi na mengine asilimia ya kubadilika inaongezeka
 
Tukijifunza kuheshimiana, kuthaminiana kuongea kwa lugha ya staha katika mahusiano yetu basi ni dhahiri kwamba tunajenga mahusiano yaliyo bora na msingi wa mahusiano yoyote yale ni kupeana heshima kwa wahusika wawili haijalishi kipato au umri kama tukiweza kufuata na kujali ni kitu gani tunapaswa kufanya basi ni dhahiri tutadumisha hata pale ambapo tulikuwa hatuwezi kuparekebisha
 
Tukijifunza kuheshimiana, kuthaminiana kuongea kwa lugha ya staha katika mahusiano yetu basi ni dhahiri kwamba tunajenga mahusiano yaliyo bora na msingi wa mahusianoi yoyote yale ni kupeana heshima kwa wahusika wawili haijalishi kipato umri kama tukiweza kufuata na kujali ni kitu gani tunapaswa kufanya basi ni dhahiri tutadumisha hata pale ambapo tulikuwa hatuwezi kuparekebisha
TF always mtu mwenye hayo uliyotaja anadondokea kwa mtu ambaye hata haeleweki, sielewi huwa inakuwaje, atafanya yote hayo bado mwenzake hawezi rudishia
 
TF always mtu mwenye hayo uliyotaja anadondokea kwa mtu ambaye hata haeleweki, sielewi huwa inakuwaje, atafanya yote hayo bado mwenzake hawezi rudishia
You are absolutely right kabisa yaani huwa inakuwa ni tofauti kabisa, huwa najiuliza ni kweli ndio mtu uliyepangiwa uwe naye au ni mambo yanatokea tu kwenye maisha
 
binafsi naamini kubadilika ni lazima mtu uamue mwenyewe kutoka ndani yako,unaweza ukawa influenced kuvaa,the way u talk etc lakini mtu hawezi kukulazimisha ulale na mwanamke/mwanamme kama wewe hujaamua,i can influence a friend to drink beer today but kama hajaipenda then sitegemei kama kesho atakunywa unless ameamua kufanya hivyo.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom