Namna ya kujenga hostel ya wanafunzi, nzuri lakini kwa gharama nafuu

TensorFlow

JF-Expert Member
Feb 11, 2020
811
968
Wakuu,

Kuna sehemu vijijini nimeona wanafunzi wa shule ya sekondari (day) wanapata shida sana, tatizo mojawapo nililoliona ni makazi yao ya kupanga kuwa duni. Sasa nikawaza kuwasaidia hawa wanafunzi kwa kujenga hostel simple kwa ajili yao.

Plan yangu ni kila mwanafunzi awe na chumba chake -- self-contained, yaani kikiwa na choo na bafu. Ataweza kupika ndani akitaka kwa kutumia jiko la gesi au umeme, lakini kutakuwa na jiko (sehemu) dedicated kwa ajili ya kupikia. Pia kutakuwa na sehemu ya kusomea, na pia nitaweka huduma zote za kistationery mpaka internet cafe.

Kutakuwa na mlinzi, na mwanafunzi hawezi kupanga bila mzazi kukubali. Kutakuwa na fomu maalumu ya makubaliano na taratibu za kuishi mahali hapo.

Eneo nililonalo ni ekari moja na ipo karibu na hiyo shule. Ingawa sitaweza kujenga hostel kukidhi mahitaji ya kupanga ya wanafunzi wote lakini itakuwa ni mwanzo mzuri wa kutatua tatizo.

Sasa wadau hebu naomba michango yenu, uzoefu na namna ya kuijenga hii hostel kwa gharama rahisi zaidi. Mambo gani muhimu ya kuzingatia? Changamoto ni zipi?

tf.
 
Back
Top Bottom