Namna ya kuishi na Ex wako ili usimkere mwenza wako

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
408
1,000
Katika mapenzi kumekuwa na changamoto kubwa sana juu ya kuishi na mpenzi wako pale anavyoishi na ma ex wake inapotokea kuwa kero kwako. Ni vigumu sana kuoa au kuwa na mpenzi ambaye hakuwahi kuwa na mpenzi mwingine huko nyuma kabla ya kuwa nawe. Ukibahatika kumpata bikra na ukaishi naye shukuru mungu japo kuna changamoto za kukosekana kwa uzoefu kwenye mambo yetu yale ya sita kwa sita.

Kama ulikuwa na uhusiano na mpenzi mwingine mkaachana na umepata mpenzi mwingine hakikisha unafuta na kukata kabisa mawasiliano na mpenzi wako wa zamani maana mawasiliano ya mara kwa mara humfanya mpenzi wake akose imani nawe pia huwa kero kwake sasa kwanini umkere mpenzi wako wa sasa kwa mtu ambaye huna uhusiano naye tena??.

Hakikisha unaepuka kumwongelea mpenzi wako wa zamani kwa mpenzi wako mpya, maana inaboa na kukera sana. Si kwa ubaya wala uzuri, ukimkandia sana mpenzi wako atajua hata yeye ipo siku utamkandia atajenga chuki na hofu kubwa juu yako, ukimsifia ndo kabisa mpenzi wako atajiuliza kwa sifa zote unazotoa mmeachana yeye ni nani basi atakuwa na wasiwasi juu ya nafasi yake katika penzi lenu.

Changamoto kubwa ni kama mlikuwa na Familia kama mlibahatika kupata mtoto basi huma budi kukaa na mpenzi wako na kumwomba uwe unawasiliana na mwenza wako wa zamani kwa faida ya mtoto na si vinginevyo.

Ni mawazo yangu juu ya namna ya kuishi na ma ex wako wa zamani bila kumker mpenzi wako wa sasa yaan usiwe na mawasiliano naye, wala usimzungumzie mbele ya mpenzi wako iwe kwa mabaya au mazuri. Tulete uzoefu wetu hapa ili kuimarisha ndoa na mapenzi yetu.
 

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,131
2,000
Mtia mada Nimekuelewaa, Japo asee X wangu wa kwanza kila nikikutana nae hainaga mistari tena, Ma X wanakuaga mitihan sana kweny mahusiano
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom