Namna ya kuifanya jf iwe tanzania na sio wanamtandao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namna ya kuifanya jf iwe tanzania na sio wanamtandao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by akashube, Sep 29, 2010.

 1. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hivi karibuni baadhi ya wanahabari ikiwemo gazeti makini la Raia Mwema walitutaja sisi wana JF kama wanamtandao ambao tumempa Dk Slaa kura nyingi za Urais.

  Je wana JF tutawezaje kuifanya JF kuwa ya mamilioni ya watanzania badala ya maelfu ya watanzania kama ilivyo sasa. Hii ni kwa sababu wengi wetu tunaamini kwamba Jamii Forums ina kila kitu ambacho mtanzania anahitaji kuweza kupambana na dunia hii ya sasa iwe siasa, dini, elimu, maendeleo,masuala ya kijamii, sheria, afya,sayansi na teknolojia au jambo lingine lolote lile.

  Kuna watanzania mamilioni wanahitaji kupata yaliyomo JF kwa sababu zifuatazo:

  1. Ndani ya JF kuna habari kutoka vyanzo vyote vya habari ikiwemo Taasisi ya Ujasusi na Usalama TISS, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, JWTZ, polisi, magereza, RITA, TANROADS, TCAA, TAA, TCRA, BRELA, TBC1, NEC, BOT, TFDA,TBS, TRA,NCAA, TANAPA, TSHATDA, SIDO, VETA, M10, TAMISEMI, MKUKUTA, MKURABITA, TACAIDS, AMREF, CDC USAID, DANIDA, CIDA, SWISS AID, SECRET SERVICE IKULU, TPA, UDSM, IFM, CCM, MUHAS, UCLAS, UDOM, RFB, NECTA, BET, TEC, idara ya habari maelezo, IPPMEDIA, HABARI CORPORATIONS, NATIONAL MEDIA GROUP, MBWENI, NGERENGERE, KUNDUCHI, MONDULI JWTZ, END OF MOROGORO ROAD TISS ADMIN, KIJITONYAMA PSU, EMBASSIES, Professional firms( Law firms, Accountancy, Engineering, Medical), CCBRT, MMC, KCMC, Halamashauri zote, madiwani wote, wabunge wote, na Ofisi ya Rais mfano Menejimenti ya utumishi wa Umma, Magazeti yote, TV zote, Radio Zote, vyama vyote vya siasa, vituo vyote vya NGO's, Mipakani kote, Duniani kote, Mfano wawakilishi wengi wa CCM nje ya nchi ni wana JF, wawakilishi wengi wa vyama mbalimbali vya siasa maeneo mbalimbali duniani ni wanan JF....NK....NK

  2. Ndani ya JF kuna matangazo ya biashara, kazi, dharura na mengineyo


  3. Ndani ya JF kuna michango ya mawazo kutoka kada zote za watu, wasomi, wasiosoma,wanaoishi nchini, wanaoishi Afrika, wanaoishi nje ya Afrika, walio madarakani, wasio madarakani, marais, wabunge, madiwani, mabalozi, wasanii, wasomi, machinga, matajiri, maskini, wanasiasa, NGO'S, mashirika ya dini, wapagani kama Kiranga, wazalendo kama mzee mwanakijiji, wapiganaji kama Luteni,wakweli kama Invisible, wasio na woga kama FL1, wafuatiliaji kama kandambilimbili, wanachama tawala kama Ninja, wanaharakati halisi kama mwanahalisi, Wapenda uhuru kama Mtu wa Pwani na weingineo.


  HIVI SASA KUNA MAKAMPUNI YA SIMU AMBAYO KUTOKANA NA USHINDANI WA BIASHARA YAMESABABISHA INTERNET IWE KAMA SIMU YA MKONONI. TUNAENDELEA KUPIGANA VIFAA VYA INFORMATION TECHNOLOGY KAMA CELLPHONES NA LAPTOPS HATA KAMA NI ZA MTUMBA KWA BEI NAFUU BILA KODI VIKIPATIKANA HADI VIJIJINI, UMEME UKAWA WA KUTOSHA, KISHA MODEM ZA BEI RAHISI ZIKAPATIKANA, NA ELIMU IKABOREKA KWA WANANCHI WOTE WA TANZANIA BASI WANANCHI WENGI MNO WATAKUWA HEWANI NA JF.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  asante
   
Loading...