Namna ya Kudhibiti Ubora wa Bidhaa/Huduma Zako

Jun 21, 2021
5
10
1639833086804.png


Dhana/mbinu ya uthibiti wa ubora katika biashara yaani "Total Quality Management" (TQM) kwa mara ya kwanza ilianza kutumika miaka ya 1980 na kampuni za Kijapani, baadae mwanzoni mwa miaka ya 1990 Kampuni za Amerika ya Kaskazini na zenyewe zilianza kuitumia mbinu hii.
Kwa upande wa Amerika ya Kaskazini, mbinu hii iiendelezwa na kuboreshwa na Washauri wa Kitaalamu (Consultants) kama W. Edwards Deming, Joseph Juran n.k.
Dhana ya Uthibiti wa Bora (TQM) imejikita katika misingi ifuatayo;
  1. Kuongeza ubora wa bidhaa au huduma zako maana yake ni kuhakikisha unapunguza matumizi katika uzalishaji au uendeshaji wa biashara yako, Upunguzaji wa matumizi katika uzalishaji au uendeshaji wa biashara yako utakuja tu endapo utadhibiti/kupunguza makosa "mistakes", utatumia muda katika uzalishaji/uendeshaji wa bashara yako kikamilifu n.k
  2. Utakapoweza kuongeza ubora wa bidhaa zako/huduma zako kwa kufanya niliyoainisha hapo juu, basi utakuwa na uzalishaji wenye tija
  3. Pindi unapokuwa na bidhaa au huduma zenye ubora, basi nafasi yako katika soko (market share) itakuwa kubwa kiasi cha kukuwezesha kutoza bei ya juu kwenye bidhaa au huduma zako (above average market price)
  4. Bidhaa au huduma zako zitakaponunuliwa kwa bei ya juu, basi faida ya kampuni/biashara yako (company's profitability) itaongezeka na kukuwezesha kubaki sokoni kwa muda mrefu.
  5. Utakapoendesha biashara yako kwa faida (having a profitable business), basi utaweza kutengeneza ajira kwa watu (creates more jobs)
Kuhakikisha kampuni/biashara yako inadhibiti ubora, unapaswa kuchukua hatua zifuatazo;
  • Uongozi wa kampuni (Management) uwe na imani (philosophy) ya kutokukubali makosa (mistakes), mapungufu (defects) na malighafi zisizo na ubora katika mchakato mzima wa uzalishaji/utoaji wa huduma.
  • Kuundwe kitengo cha udhibiti wa ubora ambacho msimamizi wa kitengo (Quality Supervisor) atapewa nafasi ya kufanya kazi na watendaji kutoka idara mbalimbali za kampuni yako. Hatopaswa kuishia hapa tu, pia atapaswa kuwa na utaratibu wa kutoa elimu juu ya ubora wa bidhaa/huduma mara kwa mara kwa watendaji wa kampuni yako.
  • Uongozi wa Kampuni (Management) ujenge mazingira yatakayowafanya watendaji wa kampuni kutokuwa na woga wa kutoa taarifa juu ya tatizo lolote linalojitokeza.
  • Uongozi wa Kampuni (Management) unapaswa kuwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa wafanyakazi juu ya mbinu/njia mpya katika uzalishaji, masoko, usambazaji n.k ili kuifanya kampuni kuendana na mabadiliko katika "industry"
  • Kuhakikisha kampuni inakuwa na na bidhaa/huduma zenye ubora ni jukumu la kila mmoja kwenye kampuni kuanzia mlinzi "security officer" mfagiaji (office's cleaner) mpaka Afisa Mtendaji Mkuu (C.E.O)
Kampuni ikifuata taratibu hizi, kwa hakika bidhaa/huduma zake zitakuwa na ubora na kuweza kuifany kampuni kuwa na nguvu ya kiushindani (competitive advantage). Kampuni nyingi za Kimarekani mwanzoni mwa miaka ya 1980 hazikuona umuhimu wa jambo hili, tofauti na kampuni za Kijapan, ambapo historia inatuambia kwamba kwenye miaka hiyo ya 1980, kampuni nyingi za kijapani ziliongoza kwa ubora katika bidhaa na huduma.

Ahsante
HEINZ MANAGEMENT CONSULTING
Consultancy, Project Management, Strategy, Fundraising & Training
PC 12119
Email: heinzconsultancy@gmail.com

Dar es Salaam

1639833071217.png
 
Back
Top Bottom