Namna ya kuchangia faini ya Tsh. Milioni 350 waliyohukumiwa kulipa Viongozi wa CHADEMA

Habari wakuu?
Unaweza kuchangia kwa aina hizo mbili. Nimeitoa kwenye akaunti yake ya Instagram .
Shime wana mabadiliko
thisis_moza_20200310_1.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja. Namna ya kuchangia haraka ili tuwaaibishe kwa mshikamano kwa ajili ya haki na demokrasia. Tupeni namba ya simu, benki ili tuchangie na mengine baadaye.
 
Tutawachangia ila wajifunze kutumia midomo yao siyo kilasiku kutukana harafu wanakuja kutaka tuwachangie! Mi nitatoa 150000 ila wasirudie! Wajifunze siasa za hoja cyo za fujo.
Pumbav,tunakujua wewe ni lumumba buku 7 na huna lolote!Hutatoa hata mia na umeandika hayo ili tu kujenga picha unayoitaka wewe!Lumumba mnahangaika kutumia kila angle kujustify ushenzi uliofanywa na mahakama kwa maagizo ya jiwe!Haki haijatendeka,hata waliomuua Akwilina wako kitaa wanakula maisha kwa maagizo ya Jiwe!
 
Wacha wakalale Segerea hadi watakapopata mkwanja. Walipe tu hizo faini au la wakate rufaa. Sheria msumeno inakata kila upande.

BTW Mahakama ziweke utaratibu sio watu kulundikana mahakamani bila sababu zozote za msingi, ni upotezaji wa pesa za walipa kodi kwa askari wa usalama nk. Mahakama ziangalie hili.
 
Baada ya SAA 11 jioni hii nimeingia bar mbili nikitafuta nipate japo soda baridi kupoza kiu.
Niliyokuta yamenishangaza. Mjadala ni kuchangia fedha kulipa faini, hadi Barmaids wanasema watatoa miatano miatano! Hii inatisha sana, kumbe nguvu ya Chadema ni zaidi ya tuijuayo.

Ikikaza kamba ccm inayaacha madaraka ndani ya SAA 24 tuu maana jeshi letu LA wananchi haliwezi kukubali kupiga mama zao na baba, kaka na Dada kama wameamua kubadili wanasiasa.

Chadema toeni maelekezo watu wapunguze idadi ya bia na soda za kunywa jioni hii na kutuma hela.
Watu laki moja (kwa uchache) wakipunguza bia mbili tuu kuzinywa na kutuma hela zake zitapatikana 300M

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitachangia ila ningekuwa mimi ningebaki gerezani mpaka kieleweke haiwezekani kesi ya mauaji mtu umpe option ya kulipa fine yaana hukumu ya mauaji ina faini? watanzania kweli tuliingia chaka.
 
Back
Top Bottom