Namna ya kubadili Maandishi kuwa Sauti

MiniActivist

Member
Dec 9, 2011
66
44
Nilikua online kusoma huku na kule kujua kama naweza kupata software ya kubadili maandishi yawe sauti, hatimaye nimefanikiwa.
Kuna namna tatu kuu unaweza kubadili maandishi kuwa sauti.
1. Online katika web pages mbalimbali zikiwemo;
http://www.zamzar.com/ ambayo ni bure
https://www.yakitome.com/upload/from_text hapa unalipia sauti ni nyingi.

2. Software ambazo unaweza kuzi-pakua na ku-install katika computer.
-Linguatec Voice Reader mb553> unaipata kwenye torrent searches
-SpeedReaderPro Sauti zake sijazifurahia sana.

3. Kwa watumiaji wa windows 7, unauwezo wa kutumia Notpad kuandika ki-app kinachobadili text kuwa audio. Chakufanya paste hii text hapa chini kama ilivyo kwenye Notepad kisha u-save kwa kuishia na .vbs ukikifungua utaona ki-dialog box cha kuandika text uki-click OK inasoma.

Dim msg, sapi
msg=InputBox("Enter your text for conversion","YuTubeMedia.com")
Set sapi=CreateObject("sapi.spvoice")
sapi.Speak msg

KAMA PANA MTU ALITAKA KUBADILI MAANDISHI KUWA SAUTI HAPA ATAMALIZA KIU YAKE.
 
Back
Top Bottom