Namna ya Kuanzisha na Kuendesha Biashara ya Kufua Nguo | Laundromat Business

Hii biashara ya dry cleaner inabidi uwe umejipanga kisawasawa hasa kwenye suala la generator maana umeme wa bongo ni kama ugonjwa wa moyo at any time you get screwed so namshauri angalie genrator zinaoendana na capacity ya hizo mashine anazotaka kuagiza all in i think for 7 million capital bado ni ndogo sana unless kama target ya biashara yake iko tofauti
 
Bado unaweza kuanza, kimkakati - mkoani sidhani kama italipa.

Kama upo Dar chagua eneo moja la kuhudumia kwa mfano vyuoni ukaanzania Mlimani ukaunganisha na vyuo vya jirani au nenda kwenye hostels kubwa kubwa. Hauhitaji kufungua duka ila unatakiwa kununua bajaj moja kuifanya kuwa duka la kutembea. Bajaj yako jaribu kuijengea ka-body and then tenga sehemu mbili; upande mmoja ya kuchukulia nguo chafu na upande wa pili kuchukulia nguo safi zinazorudishwa.

Kwa kuanza huhitaji mashine, ili kukupunguzia gharama za uendeshaji. Ajiri watu wawili wa kufua na mmoja wa kunyoosha na ku-pack nguo vizuri. Kazi hizi unaweza kuzifanya kutokea nyumbani (kama haukupanga chumba). Maji Dar ni mgao itakubidi kununua tank la kuhifadhia maji, ukipata ya kubeba lita 5000 itafaa sana. Ajiri mlinzi mmoja kukuangalizia nguo zilizoanikwa.

Hii ni biashara kama zingine hakikisha unapata vibali na kujitambulisha kama mlipa kodi ili kuhalalisha shughuli zako. Tafuta label yako ya kukutambulisha eg DOWANS Laundry Services. Label na contact zako zote ziweke kwenye bajaj, zing'arishe kadri utakavyoweza. Kazi kubwa utakayofanya mwanzo mwanzo ni kutambulisha biashara (promotion) na kazi hii itabidi uifanye bila kuona aibu. Kwa huo mtaji nakushauri kazi ya promotion ufanye mwenyewe na jinsi hiyo itakubidi pia uwe dereva bajaj.

Nakutakia mafanikio mema.
 
Mkuu asante kwa info nzuri sasa umenipa mwangaza zaidi, nadhani nimepata pa kuanzia.
ingawa bei inaonekana kama imesimama, vipi uliwahi kujaribu kucheck amazon na ebay kwa used mashine?
Kama unataka used ones nenda www.alibaba.com hapoo dubai utapat*....all the best...mimi nilipata wazimu...na biashara upate sehemnu nzuri ya kuiweka...utashangaa..baada mwezi linatokeaa jitu lenye pesa...halikujuaa,..wapi aka invest utakoma jibu lake next 2 doors balaa ndio linaanzia hapo
 
Hii biashara ya dry cleaner inabidi uwe umejipanga kisawasawa hasa kwenye suala la generator maana umeme wa bongo ni kama ugonjwa wa moyo at any time you get screwed so namshauri angalie genrator zinaoendana na capacity ya hizo mashine anazotaka kuagiza all in I think for 7 million capital bado ni ndogo sana unless kama target ya biashara yake iko tofauti

Hii mitaji itatuua jamani.

Mkuu mfano kama unaanzisha na mashine moja tu na ikitokea umeme hamna unafua manual tabu ipo kwa makoti ya suti,
target yangu ni mikoa ya singida au tabora najua wateja sio wengi sana, just kuanzia. Hii imekaaje?
 
Bado unaweza kuanza, kimkakati - mkoani sidhani kama italipa.

Kama upo Dar chagua eneo moja la kuhudumia kwa mfano vyuoni ukaanzania Mlimani ukaunganisha na vyuo vya jirani au nenda kwenye hostels kubwa kubwa. Hauhitaji kufungua duka ila unatakiwa kununua bajaj moja kuifanya kuwa duka la kutembea. Bajaj yako jaribu kuijengea ka-body and then tenga sehemu mbili; upande mmoja ya kuchukulia nguo chafu na upande wa pili kuchukulia nguo safi zinazorudishwa.

Kwa kuanza huhitaji mashine, ili kukupunguzia gharama za uendeshaji. Ajiri watu wawili wa kufua na mmoja wa kunyoosha na ku-pack nguo vizuri. Kazi hizi unaweza kuzifanya kutokea nyumbani (kama haukupanga chumba). Maji Dar ni mgao itakubidi kununua tank la kuhifadhia maji, ukipata ya kubeba lita 5000 itafaa sana. Ajiri mlinzi mmoja kukuangalizia nguo zilizoanikwa.

Hii ni biashara kama zingine hakikisha unapata vibali na kujitambulisha kama mlipa kodi ili kuhalalisha shughuli zako. Tafuta label yako ya kukutambulisha eg DOWANS Laundry Services. Label na contact zako zote ziweke kwenye bajaj, zing'arishe kadri utakavyoweza. Kazi kubwa utakayofanya mwanzo mwanzo ni kutambulisha biashara (promotion) na kazi hii itabidi uifanye bila kuona aibu. Kwa huo mtaji nakushauri kazi ya promotion ufanye mwenyewe na jinsi hiyo itakubidi pia uwe dereva bajaj.

Nakutakia mafanikio mema.

Mkuu wazo lako angalau limenitia moyo.

Mimi nimehamishiwa mkoa kikazi hivyo baada ya kutafiti nikaona biashara hii hakuna ndio maana nikaona nitumie nafasi hii kuanzisha.

Tatizo wanasema kufua makoti ya suti mashine ni lazima
 
Kama unataka used ones nenda www.alibaba.com hapoo dubai utapat*....all the best...mimi nilipata wazimu...na biashara upate sehemnu nzuri ya kuiweka...utashangaa..baada mwezi linatokeaa jitu lenye pesa...halikujuaa,..wapi aka invest utakoma jibu lake next 2 doors balaa ndio linaanzia hapo

Mkuu kweli huo ni mtihani mgumu, unaangaika kuanzisha kitu, ukianza tu from no where wenye mihela yao wanakuja hivyo hivyo.

Lakini ndio hivyo tunaambiwa wajasiriamali sikuzote ni ma risk taker.
 
Kama unataka used ones nenda Manufacturers, Suppliers, Exporters & Importers from the world's largest online B2B marketplace-Alibaba.com hapoo dubai utapat*....all the best...mimi nilipata wazimu...na biashara upate sehemnu nzuri ya kuiweka...utashangaa..baada mwezi linatokeaa jitu lenye pesa...halikujuaa,..wapi aka invest utakoma jibu lake next 2 doors balaa ndio linaanzia hapo

Interesting, though painfully true!

Hata hivyo, ndivyo law of demand and supply in a perfect competion market inavyotuonya. Mnapouza bidhaa zinazofanana kunatokea price war, na hiyo hushusha bei ya vitu. Lakini linapokuja jamaa lenye mtaji mkubwa, litashusha bellow economic level, na litakuwipe out kutoka kwenye soko.

Hata hivyo, unaweza survive na kamtaji kako kwa njia nyingi, na ya juu zaidi ni customer care na uaminifu. Kama una jina zuri, hata kama akaja mtu mwenye pesa pale, watu wataendelea kuwa Royal kwako bila kujali ukisasa wa machine ya rival wako.

Mfano mzuri, ni Salon za kunyolea nywele mijini, zipo zingine za kisasa kabisa, lakini hazina wateja na zingine ndogo zinafurika: Sababu ni kwamba custors wameshaipenda kazi yako hivyo wamejenga bond iliyo zaidi ya biashara.

So jirushe tu kama unaweza, na jitu likija na mipesa yake we unaweza ku-relocate au kubuni biashara mbadala au kuingia naye ubia kama yuko tayari!
 
Sikiza mkuu usikate tamaa, 7m unaweza kabisa anzisha hiyo kazi, tafuta machne ndogo tu ya kawaida kama hizi za majumba unapata machine nzuri tu kwa 1m inayofua na kukausha. haitaji 3phase. inauwezo wa kufua jeans 20 kwa saa. Muhimu ni sehemu ya biashara na matangazo. tengeneza office kali sana especially mapokezi fenicha zilizoenda shule, print bango moja kali sana liwe na picha ya mrembo mkali, bango liwe kubwa lijae pote kwa nje usiku liwake taa kali.

Usisahau kuandika unafua kwa machine za kisasa na wataalamu kutoka dar. tafuta mtu wa kunyoosha nguo mzuri asiwe wa hapo singida. usiruhusu watu kujua siri ya urembo wa ndani we wacha wababaike na urembo wa nje. weka na mfuaji 1 Wa mikono standby umeme ukikatika anacover. print vipeperushi vikali sambaza maotelini na maofisini. toa muda kwa mteja unaowezeka. mkuu mwanzo mgumu 7m kwa style hii utaweza. mwaka 1 utakuwa ushafunga hizo mashne.
 
Mkuu wazo lako angalau limenitia moyo.

Mimi nimehamishiwa mkoa kikazi hivyo baada ya kutafiti nikaona biashara hii hakuna ndio maana nikaona nitumie nafasi hii kuanzisha.

Tatizo wanasema kufua makoti ya suti mashine ni lazima

Mkuu, mkoa suti si nyingi sana labda Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma - zipotezee kwanza. Mkakati ni ule ule, badala ya kwenda vyuoni au kwenye hostels zungusha bajaj mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba huko ulipo utafanikiwa. Anza kwanza, utajiimarisha kadri siku zinavyoenda.
 
Mkuu nakushaurii pia angaliaa hata biashara zingine hapo vipi car wash? Nayo ni nzurii tafuta bar maarufu, fungua kwa pembeni...utapata hata gari 5 tu kwa siku za kawaida na hata 10 kwa kila week end inatosha kwa 7m unapata machine na kujenga /tank lako la maji na pump machine saafii kabisaa. Fikiriaa na hii piaa dry cleaner inasum bua kidogo kwa vimitaji vyetu maana ukikwama utashindwa kuuza kirahisi hizo machine.
 
Mayu nataka nikutie moyo kuwa unaweza kabisa kufungua hiyo biashara kwa huo mtaji wako wa m7 (nahisi ni hela yako ya uhamisho ).

Chakufanya kwanza anza na mashine ndogo ya wastani najua mkoani wateja mwanzo hawatakuwa wengi kivile, nunua washing mashine ya kama m1 hadi m2, inatosha sana kwa kufulia nguo za kawaida kama mashati, suruali, magauni, sketi, bauzi.pia mashuka, mapazia,nk.

Makoti hayafuliwi na washing mashine yana utaratibu wake wa ku dry clean, waweza tafuta kuna dry cleaner simple kwa aajili ya kusafishia makoti manual.

Pia tafuta mshine ya kusafishia makarpet ya kama lk5 inatosha sana nahii unaweza kuwafuata wateja hata majumbani si lazima walete ofisini.

Cha umuhimu tengeneza ofisi kali inayovutia nje na ndani, weka muudumu smati hakikisha unatoa muda sahihi kwa mteja kuja kuchukua nguo zake.

Hakikisha unapata mifuko ya plastiki na enga simple kuwekea nguo za wateja.

Siku za mwanzo uwe kipromotion zaidi kwa kutoa viofa vya hapa na pale mfano, mteja kaleta nguo kumi basi mbili mwambie unamfanyia free.

Mikoani kuna tv cable zinafanya matangazo bei powa sana, peleka matangazo,tengeneza vipeperushi vizuri jisifie sana kuwa unafua kutumia mashine na utaalamu wa kisasa zaidi.

Kaunta ukiweza weka ka pc pale, feed kila kitu ili uwe unatoa risiti nk utaonekana makini na smati zaidi.

Hakikisha at start zoezi unalisimamia wewe mwenyewe na hakikisha customer care ndio silaha yako no moja.

Jitahidi upate ofisi sehemu nzuri kama katikati ya mji, unahitaji ofisi kwa maana ya sehemu ya kupokelea na kutoa nguo, hii ndio inayohitajika iwe ya viwango.

Pia unahitaji sehemu ya kufulia na kuanikia hii inaitwa factor, hapa inaweza kuwa hata nyumbani kwako kama utakosa sehemu utakayoshindwa kuigawa ofisi na factory.

Pia kuwa mjanja si kila mara uwe unatumia washing mashine wakati mwingine tumia watu wako kufua kawaida labda kwa nguo maalum.

Google namna mbali mbali za kufua aina mbali mbali na kupiga basi even how to dry clean suit nk jifunze mwenyewe kisha wafundishe watu wako na wasimamie.

Mwisho nakutakia kila la heri ndugu yangu na usisite kurudi ukumbini kutujuza yaliyojiri
 
sikiza mkuu usikate tamaa 7m unaweza kabisa anzisha hiyo kazi, tafuta machne ndogo tu ya kawaida kama hizi za majumba unapata machine nzuri tu kwa 1m inayofua na kukausha. haitaji 3phase. inauwezo wa kufua jeans 20 kwa saa. Muhimu ni sehemu ya biashara na matangazo. tengeneza office kali sana especially mapokezi fenicha zilizoenda shule, print bango moja kali sana liwe na picha ya mrembo mkali, bango liwe kubwa lijae pote kwa nje usiku liwake taa kali. usisahau kuandika unafua kwa machine za kisasa na wataalamu kutoka dar. tafuta mtu wa kunyoosha nguo mzuri asiwe wa hapo singida. usiruhusu watu kujua siri ya urembo wa ndani we wacha wababaike na urembo wa nje. weka na mfuaji 1 Wa mikono standby umeme ukikatika anacover. print vipeperushi vikali sambaza maotelini na maofisini. toa muda kwa mteja unaowezeka. mkuu mwanzo mgumu 7m kwa style hii utaweza. mwaka 1 utakuwa ushafunga hizo mashne.

Ulichoongea ni sahihi kabisa hata mimi nilitaka kumpa ushauri huu huu, Milioni 7 inatosha kabisa kuanzisha biashara ya Dry Cleaner ndogo ya kawaida tu kwani kwa mkoa uliopo nina uhakika kodi za vyumba vya biashara si kubwa kama DSM na pia kwa kuanzia nunua mashine za kawaida tu kama tunazotumia majumbani ila ziwe zenye capacity kubwa kidogo ambazo bei yake ni kuanzia laki 6 mpk milioni 1 nunua kama 3 hivi moja ya milioni na nyingine say za laki 8 na 6. Hakikisha mojawapo iwe inafua na kukausha kwa ajili ya wateja wenye haraka na hizo nyingine unatumia wakati mtu hana haraka kwa mfano akileta suti leo unamwambia aje kuchukua kesho kutwa

pia uwe na mtu (dobi) ambaye atakuwa anafua kawaida nguo za kawaida na kuzianika na kupiga pasi vizuri kisha kuzihifadhi kwenye mifuko maalum yenye nembo ya Dry Cleaner yako.

Mtaji ulionao ni mkubwa sana wala watu wasikukatishe tamaa ila cha muhimu ni kuangalia demand ya hiyo huduma ktk sehemu uliyopo ndio itakayokuahakikishia kuendelea kwa biashara yako

Kwa kuanzia jaribu kuwa na mashine moja ya milioni yenye kufua na kukausha halafu ukiona soko ni zuri ongeza nyingine mbili kama nilivyokushauri hapo juu na kama ikichanganya zaidi ndipo ufikirie kuagiza mashine kubwa kutoka nje kama wengine walivyoshauri ila kwa sasa anza na mashine za kawaida za majumbani ambazo bei yake ni nafuu na zinafanya kazi vizuri tu maana mie nina mashine nilinunua laki 5 Mlimani City wakati ndio imeanzishwa na inatumika mpk leo na inafua vizuri tu na nina uhakika hata ningeitumia kwa biashara ingemudu vizuri tu kwani inafanya kazi poa sana

Pia ukishaanza hiyo kazi tafuta tender kwenye mahospitali ya kufua mashuka na nguo zingine zinazotumika hospitali unaweza kutoka ila anza kidogo usiweke hizo hela zote mpaka usome soko kwenye ndio uweke hiyo M7 yote.

Wengi humu wanakuchuuza kwa kufikiria maofisi makubwa kwa zile dry cleaner za Shoppers Plaza au Namanga wakati, mikoani wala hmna wateja kihivo.
 
Je nikitaka ku specialise na kupiga pasi tuu je itafanikiwa?

NakIjua gharama ni umeme bas lakini sijajua nguo kupiga pasi ni kiasi gani
 
Hello wadau!

Nataka kuanzisha biashara ya dry cleaning somewhere in this country lkn nataka kuanza kwa small scale ili kutest biashara!nataka kujua mtaji kiasi gani ambao unaweza kuhitajika kwenye hiyo bussiness pia ni machine gani ambazo natakiwa kuwa nazo!na hz machine zinaweza kucost sh ngapi na zinapatikana nchini au mpk niagize na km kuagiza wakina nani ni reliable suppliers.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Hello wadau!

Nataka kuanzisha biashara ya dry cleaning somewhere in this country lkn nataka kuanza kwa small scale ili kutest biashara!nataka kujua mtaji kiasi gani ambao unaweza kuhitajika kwenye hiyo bussiness pia ni machine gani ambazo natakiwa kuwa nazo!na hz machine zinaweza kucost sh ngapi na zinapatikana nchini au mpk niagize na km kuagiza wakina nani ni reliable suppliers!

Mkuu MINA

Ningekushauri iwe ni laundry , pia ukapata chumba cha kutosha unaweka wash & drying machines watu wanakuja kufua kwa kulipia , pia ukawa na drop off services, biashara hii inaweza kuwa nzuri dar Arusha , kwa dar tafuta maeneo yaliyo karibu na hostels au vyuo

Yes, it can be a good business with affordable price.
 
Biashara hii hata mi nilishawahi kuiwaza nikatafuta hizo mashine ambazo ni for commercial use lakini sikupata muelekeo sahihi, nasubiri wadau wanaofaham hapa hii bizness, mi nataget soko la dodoma. Ushauri plz
 
Umeme should be number one concern. I believe umeme lazima uwe stable kabla hujawaza biashara hii.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Nilishawahi kutafuta kila kinachohitajika, kuanzia dryers, commercial washers na steamers lakini baada ya kugundua ni investment ya zaidi ya milioni sitini za kitanzania, nikakumbuka inabidi niwe na 'power plant' yangu, nikatia kapuni mawazo hayo.

Kama alivyododosa mdau hapo juu, umeme ni no1 concern mdau. Kwa links na machine zinazohitajika anza kwanza na used ebay ili uweze kujua brands zinazoongoza duniani. Ingia eBay - one of the UK's largest shopping destinations au ebay.com type commercial washers itakuja list, angalia zinazouzwa bei kubwa kuliko nyingine kwa kuchoose buy it now option halaf soma majina ya manufacturers kisa search google mpya zitakuwa zinauzwaje.

Cha pili kutathmini ni location na target customers, sehem zenye wahitaji wa huduma hizi tayari zina wadau wanapambana, jaribu kuwatembelea hoji wafanyakazi wote kuhusu biashara, utapata majibu if its worth investing.

Kila la kheri.
 
Natazamia kufungua biashara ya kufua nguo kwa hiyo nahitaji mashine kwa kazi hiyo. Tafadhali naomba mwenye kujua bei zake na mahali kwa kuzipata anipe taarifa.

Mashine ni kama zifuatazo

1. Dry cleaning machine (16kg)

2. Packaging Machine

3. Ironing table - aspiration with boiler, height adjustable

4. Stain removing machine

5. Industrial washing machine (16kg) - for blankets etc

6. Wringer (8kg)

7. Domestic washing machine

8. Semi-silent compressor

Natanguliza shukrani
 
Back
Top Bottom