chofachogenda
Senior Member
- Oct 6, 2016
- 104
- 190
SEHEMU 1: JINSI YA WAZUNGU WALIVYOTOKEA DUNIANI
Binadamu wa sasa alizaliwa Afrika na kutokana na mtu mweusi watu wa aina yote duniani walipatikana . Swali je ni kwa namna gani rangi tofauti za ngozi zao zilipatikana au maumbo tofauti ya sura hata nywele zao zilipatikana?
Ili ni swali ambalo bado halijibiki kwa urahisi lakini sayansi imefikia maendeleo mazuri katika kulijibu swali hili hasa chuo cha Havard ambacho kilijikita kwenye masomo ya jeni au vinasaba. Genetic studies of Havard University ambacho mwaka 2015 kilijikita katika uchunguzi wa mabaki wa binadamu wa sasa (modern human) katika ulaya ya kale.
KUTOKA TUMAI MPAKA OMO 1: KUZALIWA KWA BINADAMU
Kutokana na nadharia ya kisayansi, Dunia iliumbwa takribani miaka bilioni 13 iliyopita.Mpaka miaka milioni 65 iliyopitan kiumbe ambacho kilikuwa kinatawala dunia kilikuwa ni Dinosau ( Dinosaur).Ambapo kutoweka kwao kulitokana na gimba(asteroid) kugongana na hii sayari hivyo kuruhusu kutokea kwa wanyama wadogo
Miaka milioni 10 iliyopita, kiumbe (primates) kilimzaa sokwe kiumbe ambacho kinafanana na binadamu kwa mara ya kwanza katika historia.Hicho kiumbe kilikuwa kinaitwa Tumai na mabaki yake yalipatikana nchini Chad yakiwa na umri wa miaka miloni 7.
Kutoka Tumai , kiumbe hicho kinachofanana na binadamu kiliendelea kubadilika taratibu ndani ya Afrika kupitia Homo erectus,Homo habilis, Homo naled,Homo rhodesiensis n.k. Mabaki ambayo yanapatikana Mashariki na kusini mwa Afrika.Baadhi ya hao ya binadamu wa mwanzo walisambaa katika mabara mengine lakini walitoweka kutokana na changamoto za kimazingira.
Takribani miaka 200,000 iliyopita , binadamu wa sasa (Homosapiens) alizaliwa akiwa na komwe, kidevu, ubongo na sifa nyingine sinazomtambulisha kama binadamu wa sasa. Hapa tunazungumza kuhusiana na Omo 1 ambaye mabaki yake yalipatikana Kibishi kusini mwa Ethiopia.Hao ndio walikuwa Waafrika wa kwanza wanaume kwa wanawake walioenda kuitwaa dunia.
WAAFRIKA WALITAWANYIKA DUNIA NZIMA
Miaka 100,000 iliyopita, Viumbe hawa kutoka Afrika walianza kwenda nje ya bara la Afrika kwa kuingia Palestina/Israel na Yemen. Huyu alikuwa binadamu wa kwanza kuikalia Asia yote. Kwa upande mwingine Afrika Magharibi waafrika wenye maumbo mafupi (Mbilikimo) walitumia mkondo bahari wa Antlantic kufika Brazil miaka 50,000 mpaka 65,000 iliyopita hivyo ndivyo walivyoingia Amerika ya kusini. Kutoka kusini –mashariki ya bara la Asia waafrika waliwasili Australia miaka 50,000 iliyopita na wakavijaza visiwa vya Pacific mpaka Hawaii. Na hatimae waliingia ulaya miaka 40,000 iliyopita na kufika nchi za skandinavia na Uingereza.
Hawa watu weusi kutoka Australia na Pacific waliungana Marekani . Watu weusi ambao waliwasili moja kwa moja kutoka Afrika kwa kiasi kikubwa waliijaza Marekani tangu mwanzo
Hivi ndivyo dunia nzima ilijazwa na watu weusi na kwa maelfu ya miaka kulikuwa na watu weusi tu dunia duniani kote .Swali je wazungu, waarabu na waasia walizaliwaje au walitokeaje?
KAZI MUHIMU YA VITAMIN D
Vitamin D ni element ambayo inawezesha mwili kufyonza calcium ambayo hutumika kutengeneza mifupa. Hata hivyo moja ya hatua muhimu katika utengenezaji wa vitamin D inahitaji miale ya jua.Kama kukiwa na jua la kutosha mwili hutengeneza vitamin D. Il kwa kuwa jua ni kali san Afrika linaweza kuleta madhara kwenye ngozi na kusababisha kansa, kwa hiyo mwili unatengeneza pigment zinazoitwa melanin ili kuilinda ngozi. Watu weusi ni weusi kwa sababu miili yao ilitengenezwa ili kuendana na jua la Afrika .
Melanini inaruhusu kiwango muhimu cha miale ya jua kupenya na kutengeneza vitamin D kwa ajili ya mifupa na wakati huohuo kuilinda ngozi dhidi ya jua kali .
Wakati mtu mweusi alipowasili ulaya magharibi alikutana na hali ya barafu. Kipindi hicho hata Uswisi ilikuwa barafu tupu. Hiyo zama ya barafu (Ice Age) ilikuwa ni miaka 130,000 iliyopita na kuisha miaka 10,000 iliyopita ilikuwa inaitwa wurm glaciation.Baridi lilikuwa kali mno na jua lilikuwa adimu katika mazingira hayo.
Melanin ilizuia hiyo miale kidogo ya jua kupenya kwenye ngozi na vitamin D ikawa inatengenezwa kwa kiwango kidogo sana .Kutokana na upungufu wa vitamin D uliosababishwa Melanin kulitokea ulemavu na vifo vya mapema (premature death).
Kutokana na tafiti iliyofanywa na Clemens TL na wengine mwaka 1982 na Carolina na Bolina na wengine mwaka 2014, inasema kwamba wazungu wanazalisha sana vitamin D Kuliko watu weusi wakiwekwa katika mwanga wa jua ulio sawa. Matokeo yake ili mwili uweze kusurvive na kuendana na mazingira ikabidi iondoe melanin hasa kwenye maeneo ambayo jua lilikuwa adimu………..itaendelea
Wako: Benjamins
Credit: AHHA (African History,Histoire Africaine)

Tumai