Namna picha inavyoweza kuhaririwa 'Editiwa' na kutumika kufanya upotoshaji

NAMNA_PICHA_INAVYOWEZA_'EDITIWA'_NA_KUFANYA_UPOTOSHAJI.jpg


Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kumeibuka Application nyingi za kutengeneza picha, ambazo zinaweka kubadili muonekano wa picha kwa namna nyingi na hata kuleta sintofahamu baadaye

Upotoshaji katika picha ni kitendo Cha kuhariri (edit) picha kwa kuongeza kitu, kupunguza kitu kuwaaminisha watu kuhusu jambo fulani kutokana na muonekano mpya ulioutengeneza katika picha hiyo.

Upotoshaji wa picha huweza kufanywa kwa namna mbalimbali, zifuatazo ni namna chache kati ya nyingi:

1. Kuhariri au kutengeneza
Huu ni upotoshaji katika picha ambapo mpotoshaji hutumia utaalamu kuhariri au kutengeneza picha fulani kwa lengo la kuitoa uhalisia wake na kuifanya iwe kwa namna inayoendana na lengo lake. Picha huweza kuhaririwa kwa kubadili rangi, mavazi kubadili mazingira, kuambatanisha picha fulani na picha nyingine, kubadilisha muktadha, kushikishwa vifaa n.k

2. Kutumia picha pahali pasipokuwa pake
Upotoshaji katika picha pia huweza kutokea kwa kutumia picha fulani kwa wakati usiokuwa sahihi au mazingira yasiomuwa sahihi. Mathalani, mtu anaweza kutumia picha ya zamani kuihusisha na habari inayotokea sasa. Au kutumia picha isiyo sahihi na kuifanya inahusika kwenye tukio fulani.

3. Kufuta sehemu ya picha
Upotoshaji unaweza kufanyia kwa kufuta sehemu ya picha ili kubadili uhalisia wake. Mfano picha ilipigwa ikiwa na vitu 3 mtu anaweza futa 2 na kubaki kimoja na picha inakuwa imepoteza uhalisia wake

Angalizo: Si Kila kuhariri picha ni upotoshaji au ni vibaya. Ubaya na upotoshaji unaanzia pale ambapo kutengeneza au kuhariri picha hiyo kunalenga kuwaaminisha watu kuhusu jambo lililoongezwa au kupunguza katika picha

Hivyo, kabla hujaamini picha au kusambaza picha fulani, ni muhimu kutathmini kama picha hiyo ni halisi au imehaririwa. Ikiwa itakuwa shida kutambua ni Bora ukiipeleka katika Majukwaa ya uhakiki upate msaada zaidi
 
Yes, kweli uongo unafanyika sana kutokana na kuhariri picha ila uongo unakuwepo endapo mwenye picha anataka kufanya uongo kwa hadhira anayotegemea.

Yote kwa yote uhariri wa picha hauna ubaya kwa sababu ya teknolojia ilipofikia kwa sasa.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom