Namna pekee ya kuheshimika vyombo vyetu vya dola ni kuvitenganisha na wanasiasa

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kila zinapopigwa kelele kuundwa kwa katiba mpya watu huhusisha zaidi mawazo yao wakidhani ni kwa ajili ya maslahi ya kisiasa tu, hii ndio sababu ya kusuasua kwa mchakato wa katiba mpya, watawala wanahisi kua pengine watanyimwa fursa muhimu ya kulindiwa kura zao ili warudi kwenye nafasi zao.

Katika muundo wa majeshi yote duniani pamoja na kufundishwa sheria za kufuata kwenye majukumu yao lakini linapokuja suala la maelekezo lutoka "JUU" hua hakuna namna, askari hua hatakiwi kubisha wala kujadili maakizo ya kiongozi zaidi ya kutekeleza tu. Hapa ndipo shumtma mbali mbali zinakoanzia kama utaratibu huu unatumiwa kisiasa zaidi au kinyume chake.

Kwenye baadhi ya nchi hasa Marekani,uimgereza, Ufaransa,Ujeruman,Serbia na hata kwa majirani zetu wa Kenya pale. Mwenzetu wameweka miundo ambayo hata kiongozi wa nchi hawezi kutia mguu kwa maagizo kwenye vyombo hivyo bila sababu ya msingi ambayo hata bunge huridhia. Tujikumbushe tu juzi juzi hapa jinsi Rai wa Marekani alvyoanza kuvibwatukia vyombo vya usalama ndani ya nchi yake, majibu alyoyapata pamoja na Urais wake ilibidi awe mpole tu.

Ni Afrika tu ambako hata mkuu wa mkoa anaweza kuambatana na kundi kubwa la askari wa ulinzi na usalama kuvamia eneo flani, ni Afrika pekee ambapo hata mkuu wa wilaya tu anaweza kutoa amri kukamatwa na kutiwa ndani kwaa waandishi wa habari kutokana na sababu za hovyo tu.Haya yote ndio yanayofanya vyombo vyetu vya usalama kulaumiwa kila siku na kuhusishwana matukio ya hvyo hovyo.

Ni lazima ifike mahali tuviache vyombo vyetu vya dola viwe huru, hata upatikanaji wa viongozi wake wakuu usiwe wa kisiasa ufuate taratibu za kitaaluma zaidi. Hili jambo linaweza kutekelezwa na uwepo wa katiba mpya peke na sio amendments kwenye sheria za kikoloni.Vitenganishwe na siasa huwezi kusikua tena mambo ya utekaji,itesaji na mauaji ambavyo vimekua vikihusishwa navyo.
 
Hakuna asie fahamu kuwa vyombo vyetu vya Dola ndio no 1 wanao dumaza democrasi ya nchi hii,mifano iko mingi tu na Wananchi sio matasira au tuko Blind .

Wewe uwe siku zote na aidia za kiccm ccm tu kinyume na hapo basi utakua adui na hata kuonekana sio raia wa Tanzania na kukosa right zako zote .
 
Nadhani ungeweka Tanzania na si Afrika nzima
 
Hakuna asie fahamu kuwa vyombo vyetu vya Dola ndio no 1 wanao dumaza democrasi ya nchi hii,mifano iko mingi tu na Wananchi sio matasira au tuko Blind .

Wewe uwe siku zote na aidia za kiccm ccm tu kinyume na hapo basi utakua adui na hata kuonekana sio raia wa Tanzania na kukosa right zako zote .

Tatizo CCM wapangaji wakuu ni watu kama akina Makonda tusitegemee chochote zaidi ya vitisho na mauaji lakini cha maana hakuna.
 
Back
Top Bottom