Namna nzuri ya kuishi unapofikia umri wa miaka 50 na kuendelea

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,270
Ukiishi mpaka kufikia umri huu ni jambo la kumshukuru Mungu. Kutokana na huduma bora za afya wengi hufikia sherehe ya miaka 50, 60, 70, 80 hata 90.

Ukifika miaka 50 hata kama huna tatizo lolote la afya ni muhimu kuufanyia mwili check up. Punguza unywaji wa pombe kama ni mywaji pamoja na uvutaji wa sigara. Jitahidi katika mazoezi ya kutembea japo kwa saa moja kwa siku. Kwa wengi muda huu umemudu kununua gari ambalo hukupeleka sehemu nyingi. Unaweza kurudi kazini na kwenda matembezini kwa nusu saa kwenda na nusu saa kurudi.

Mboga na matunda iwe nusu ya mlo wako wa siku. Punguza kula nyama hasa nyekundu, Punguza wanga, maji yawe kinywaji kikuu badala ya juice.

Kama umegundulika na magonjwa ya moyo, kisukari au figo kumbuka kutumia dawa kama ulivyoshauriwa, ikiwezekana kuwa na blood pressure monitor au blood sugar monitor ujipime ukiamka asubuhi na kabla hujalala.

Kumbuka kuandika wosia.
 
Life is worthless kama unazaliwa afu toka umezaliwa wewe upo tu hospital na magonjwa kama vile uliletwa duniani kuumwa. Lakini hivi kwanini Tom Cruise ana miaka 50+ ila anaonekana yuko fiti na mamuvi ya action anafanya mwenyewe bila shida, wakati huku kwetu mru wa miaka 50+ anakua babu asiyejiweza.
 
Mkuu kabla ya kuvuka barabara si unaangalia kama kuna gari inakuja kwanza?
Ajali ni ajali tu. Wapo wanaopata wakiwa kwenye gari, wakiwa wanatembea gari ikaacha njia, pikipiki kuanguka,n.k.
unatoka asubuhi mzima lakini kurudi upo kwenye sanduku.
 
Ma celebrate wanafanya mazoezi sana na kula vizuri ili kutunza mwili. Ule mwili wa Tom Cruise ndiyo source yake ya income. Ana dietician, personal trainer, personal doctor.
Mimi sidhani kama mazoezi tu yanafanya mtu asiwe na muonekano wa kizee. Mfano Jackie Chan ana miaka 65 na ni mfanya mazoezi sana kwa ajili ya action muvi zake. Ila kuna actor wa kihindi anaitwa Anil Kapoor ana miaka 62 na ana muonekano wa ujana kuliko hata mwanaume aliyemuoa binti yake. Jack Chan ni mzee zaidi kwa huyu jamaa japo Jack anafanta mazoezi.
 
Denvers,
Siri kubwa ni ulaji wa mboga na matunda na maji mengi. Hawa wanakuwa na Dieticians wao wanawashauri vyakula vyenye source ya protein bila kula nyama.
 
wosia nimeandika ila pombe imenishinda kuacha!!!!
Punguza kidogo dada, Niliacha kula nyama kwa miezi mitatu nilipungua sana ila nimeanza kula tena japo siku moja kwa wiki kwakua sijapata reliable source ya protein.
 
Punguza kidogo dada, Niliacha kula nyama kwa miezi mitatu nilipungua sana ila nimeanza kula tena japo siku moja kwa wiki kwakua sijapata reliable source ya protein.
Mimi nyama sili sababu nyingi zinatoka Australia na sina meno, mimi nakula pork ila nachagua isiyo na mafuta na Lamb kwa wingi toka Switzerland I love lamb. Pombe nikiacha nitakunywa mataputapu yaani whiskey? Heri nijinywee wine ili nisogeze siku. Ukistaafu halafu huna shughuli napo taabu. We acha tu.
 
Huu mfumo mzuri wa kuzingatia mambo muhimu kiafya inabidi uanze mapema. Kukumbuka wakati umeshafika miaka 50 matokeo yake hayawi mazuri sana.

Ni vema kuanzia sasa mtu unaanza kutilia maanani na kuijali afya kwa kufanya mazoezi, aina ya vyakula, kupunguza sukari na mafuta, kufurahia maisha kadri iwezekanavyo.

Kuanza kula mboga mboga na kunywa maji mengi ukifikisha miaka 50 inakua umeshachelewa.

Tujitahidi kuwajengea huu utamaduni ndugu, jamaa na wale tunaowajali. Hauwezi kuacha kunywa vitu vyenye kemikali na madhara huku unawaacha ndugu, mke au watoto wanaendelea kutumia, haitakua na maana ukabaki vizuri peke yako huku wanaokuzunguka wako taabani.

Ahsante kwa kutukumbusha Sky Eclat chapati za kumimina niwekee 6 na bajia za 1000 nazipitia jioni.
 
Mimi nyama sili sababu nyingi zinatoka Australia na sina meno, mimi nakula pork ila nachagua isiyo na mafuta na Lamb kwa wingi toka Switzerland I love lamb. Pombe nikiacha nitakunywa mataputapu yaani whiskey? Heri nijinywee wine ili nisogeze siku. Ukistaafu halafu huna shughuli napo taabu. We acha tu.
Fanya mazoezi ya Yoga na kukimbia kama huwezi kukimbia basi jogging poa pia.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom