Namna nilivyoweza kuacha POMBE, na kuamua starehe yangu iwe MSOSI

Kula kwa kiasi, kunywa kwa kiasi,

Ila wewe unaendekeza ulevi hadi kwenye kula, ona Sasa misosi yote hiyo unaenda kupigana mieleka au.

Anyway jiandae na,
Obesity
Bp
Diabetes
Kibamia

Kila la kheri
Ila umeboa kwanin utukimbie kweny kunywa pombe

puker
 
Habar za muda huu, ndugu zangu wana JF.

Kama tujuavyo tuliowengi ikifika mwishoni mwa mwaka...tunakwaida ya kujitathmini yale tuliyoyafanya kwa kipindi cha mwaka mzima. Katika nyanja ya mafanikio, uzembe/jitihada tulizozifanya katika kutimiza malengo tuliojiwekea.

Sasa katika kujitathmini, nikagundua...karibu 60% ya kipato nikipatacho kinaishia kwenye gambe. Nilisikitika nikajiona ni mjinga wa kujitakia.

Nikaamua kuweka nadhiri kwamba ifikapo 2021, niachane kabisa na habar za ulabu , nihamie kwenye starehe ambayo itakuwa cheaper kuliko pombe kwa namna moja au nyingine isilete matokeo mabaya katika maisha yangu.

Baada ya kutafakari kwa kina...nikaona nihamie kwenye msosi...yani vile vyakula vyote ambavyo vinafurahisha nafsi yangu ndio iwe starehe yangu pendwa.

Aisee since January kuanzia nyumban kwangu mpaka ofisini ni zaid ya super market achilia mbali misosi ya nje ya home na ofisini.

Kiukweli, natumia kiasi kidogo sana cha pesa na naenjoy sana..siwezi orodhesha vyote lakini hv nisehemu ya vyakula ambavyo havikosi kwenye ratiba zangu za kila siku...

1. Kitimoto rosti na ndizi huu mara nyingi ni mlo wangu wa jioni karibuni kila siku...siku ninazokosa ni chache sana, kinachobadilika ni aina ya mapishi tu. J3 inaweza kuwa kavu+ ndizi, J4 ikawa choma, j5 ikawa rost +vegetables, Alh ikawa makange ya ndizi mixed with kitimoto.

2. Mchemsho wa kuku wa kienyeji, Nafikir wale wahudumu wa uhuru bar ni mashahidi katika hili

3. Ugali nyama choma(Mbuzi)...napendelea zaidi nyama iwe ya nundu

4. Birian kila ijumaa huwez nikosa pale moroco kwa mama sakina

5. Wali maini ni chakula changu pendwa pia.

Achilia mbali..Makorosho, ma ice cream ya bakharesa(sio haya ma bolcon ya jerojero), na haya ma fresh juice ndio kila wakati.

Kiufupi since January naishi kama mgonjwa (Maana inaaminika Tanzania hatuli vizuri mpaka tuumwe.

MATOKEO.

Hapa ndio kwenye balaa. Mara ya mwisho nilipima nikawa na kilo 87/88, Jana nimepima nna Kg 96. Nimenenepa haraka mno kwa kipindi kifupi.

Ila kwenye upande wa financially nimeokoa hela nyingi mno.

Sasa ndugu zangu...hii lyf style nimeipenda sana tatizo naona kabisa huko mbele itakuja kuniletea matatizo. Nataman kuanza kufanya mazoezi tatizo huo muda ndio unakosekana

Nakaribisha mawazo yenu wadau. Najua watakaobeza hawakosekani.


Picha sio halisi ni kwa msaada wa google. Sinaga tabia ya kupiga picha chakulaView attachment 1703758View attachment 1703760View attachment 1703759View attachment 1703763View attachment 1703761View attachment 1703762
Safi Sana
 
Hivi vyakula vyote ulivyotaja hapa ni mtambo wa magonjwa, kwa kifupi jiandae kuwa mgonjwa mtarajiwa wa sukari na presha

1. Kitimoto rosti na ndizi huu mara nyingi ni mlo wangu wa jioni karibuni kila siku...siku ninazokosa ni chache sana, kinachobadilika ni aina ya mapishi tu. J3 inaweza kuwa kavu+ ndizi, J4 ikawa choma, j5 ikawa rost +vegetables, Alh ikawa makange ya ndizi mixed with kitimoto.
3. Ugali nyama choma(Mbuzi)...napendelea zaidi nyama iwe ya nundu
emoji39.png


4. Birian kila ijumaa huwez nikosa pale moroco kwa mama sakina
emoji4.png


5. Wali maini ni chakula changu pendwa pia.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kula kwa afya mdau kama ulivyoshauriwa na pia piga mazoezi ili kujiweka fit.
Mimi nagonga menyu hasa ila yote inaishia kwenye mbio nimeweza kumaintain uzito wangu kwa miaka mitatu sasa nacheza kwenye 72-76kg.
Kipindi cha nyuma wakati naishi kizembe na tungi kwa sana nilikuwa nacheza kwenye 88-90.
Kila la kheri mdau na hongera kwa kuachana na tungi.
 
Unaandaa bomu litakalokugharimu maisha yako yote maana aina ya misosi unayokula ni hatari sana
 
Hongera sana mkuu, nikupongeze kwa kuacha pombe sio kitu rahisi, pili umeamua kula chakula ni vizuri sna kwa afya yako.

Ushauri wangu jaribu kupata muda wa kufanya mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako.

Hongera sana mkuu
 
●Kula sana pombe {ulabu} angalau mara moja au mbili kwa wiki.
●Kula balanced diet lean protean,starch au wanga, vitamin, minerals na maji ya kutosha angalau glass nane kwa siku.
●Kula zoezi la kutosha.. mimi nakimbia 6km mara nne kwa wiki.


Umeacha pombe umejitafutia matatizo mengine umeongeza uzito mkubwa ndani ya muda mfupi.
 
Mkuu uzito wa mwili vipi hiyo ratiba ya chakula inahitaji mazoezi kama ya kuua nyangumi kwa upanga.
 
Kula kwa kiasi, kunywa kwa kiasi,

Ila wewe unaendekeza ulevi hadi kwenye kula, ona Sasa misosi yote hiyo unaenda kupigana mieleka au.

Anyway jiandae na,
Obesity
Bp
Diabetes
Kibamia

Kila la kheri
Ila umeboa kwanin utukimbie kweny kunywa pombe

puker
Ulevi una hasara nyingi kuliko faida boss
 
Sijasoma maelezo zaid ya kichwa cha habari...hongera sana kwa kuacha pombe ila mimi niko sehemu najipongeza kwa kuacha pombe kwa kunywa walau bia mbili kusheherekea wiki mbili za kutokugusa pombe.
 
Back
Top Bottom