Namna nilivyonusurika kufa kwenye ajali ya gari, Bongo unakufa huku unajiona

Kwema wadau?

Mwaka huu mwanzoni nikiwa nimetoka kusheherekea sikukuu ya mwaka mpya na nikiwa nimefanya maombi ya mipango yangu mingi kwa mwaka huu na kumsihi sana Mungu wangu aliye hai anijalie afya, uhai, furaha na amani tu mengine nayaweza hayanisumbui kabisa, basi sikuwa najua siku chache zijazo nitakutana na jambo baya na la kutisha kiasi icho.

Siku ya Tukio;

Nikiwa nawahi zangu kwenye majukumu yangu ya kikazi asubuhi kabisa hapa ndani ya Dar es Salaam tena nikiwa sina hofu wala kuwaza lolote, ile wazungu wanaita "the fear of unknown" kwamba kama kuna jambo baya linaenda kutokea basi kuna ishara flani huwa zinakusumbua kama kukosa amani and so, but mie siku hiyo haikuwa hivyo wala na nilikuwa nawaza tu niwahi kufika ofisini.

Ni asubuhi hio nikiwa ktk mwendo wa kawaida kabisa katika chombo private tu, ghafla kitu kikaniambia "be very careful" na nikaitii hii sauti so nikapunguza kabisa mwendo wa chombo changu na nikawa kawaida kabisa, haikupita hata dk 10 mbele yangu nikaona daladala mbili zinafukuzana kuwahiana abiria, kama kawaida yao hawa mabwana na ujinga wao wa kuwawahi abiria wa mbele zao, so hizi daladala hazikuwa upande wangu zilikuwa kulia kwanguwmie nikiwa kushoto so nilikuwa naziona face to face na nikajua kila mtu ni lazima aheshimu sheria za barabara na kukaa upande wake, sasa haikuwa hivi, yule dereva aliyekuwa anapitwa akafanya kumu overtake mwenzake nadhani bila kuangalia na labda atakuwa ni mjinga wa kuzaliwa wa kweli kweli, na ikumbukwe njia ilikuwa imenyooka so nimeanza kuwaona toka ka distance flani hivi mbele yangu wakifanya huo ujinga na haikuchukua hata dakika tatu tangu nianze kuwaona na kuniletea changamoto mbaya sana, yule dereva mwingine wa daladala alie overtake bila kuangalia nadhani ile gari ilimshinda au sijui kama shetani aliingilia kati ila nilishangaa tu kishindo kanigonga face to face wakuu, aisee nilishangaa sana lakini kuja kustuka naona damu zimejaa chini ya gari langu, airbag na watu wanapiga kelele, sikuzimia wala sikuskia maumivu ila nilikuwa kwenye mshtuko mkubwa sana sana.

Ile gari ilivyonigonga na ilizima pale pale yenyewe tu na kwangu huku sikuona tena ya mbele, nikawa najipapasa nikihofu yasije yakawa mambo ya uti wa mgongo kushtuka na kushindwa kuamka forever, nikajaribu kutikisha miguu naona mguu mmoja haurespond na kama bega linaniuma hivi, sikujua tena nini kimetokea ila mguu ulivunjika, bega kustuka na huu mguu uliovunjika ni tuseme ulikuwa umepasuka na ndo chanzo cha zile damu, na hii baadae nilikuja kujua ni kwamba nilikanyaga break kwa nguvu na kunyoosha mguu kwa kukaza labda kwa kustuka au hofu so gari ilivyopigwa kwa nguvu na kubonyea so presha yake na effect ndo ikaniletea hayo madhara.

Kilichofuata kuanzia hapo ikawa sina sauti tena, naona naamriwa tu vitu na wananchi waliokuwa wamejazana pale, kila mmoja akisema hivi na mwingine akisema vile na wangine wakirekodi kwa simu tukio lile na mie mwenyewe nikiwa bado nna mstuko mkubwa sana nawaza hivi ni mimi au naota? Nikiaskia sauti mkagueni vizuri labda ameumia kichwa?

Nikaskia shauri likiendeshwa juu yangu, wananchi wakasema tumpeleke polisi tukachukue PF3, wakaja kunitoa huku naona watu wameshika vichwa wakina mama wanalia na mie sasa nikaanza kuogopa uende nimeumia sana kuliko ambavyo najiwazia wakati huo, so najaribu kusimama mwenyewe siwezi, wananibeba na wanasema twende polisi, damu kila mahala na huo ni mguu tu, japo nna maumivu ya bega na mkono lakini najishangaa nasema kwa namna damu hizi zinavyotoka huko polisi ntafika nikiwa mzima kweli? Na kwa maeneo hayo kituo cha polisi kipo wapi sasa? Na je kutokea hapo mpaka kufika Hospitali itakuaje? Naona kabisa wananchi hawana elimu juu ya kuzuia damu kutoka na i feel like labda nijisaidie ila siwezi kufanya lolote, moyo unaenda speed sana na bado niko shocked tu.

Polisi hapakuwa mbali na hawakuwa na hiyana, ni kakituo ka dogo hakukuwa na jam ni walinihudumia ndani ya dakika 5 tu nikaipata pf3 tukaondoka na wananchi ambao walikuwa wamenibeba kwenye kirikuu.

So tukaelekea hospitali na hapa ntaomba nisitaje majina ya hospitali wananchi wasije wakaamua kwenda kuzichoma moto, so nikapelekwa hospital ya wilaya, mpaka nafika hospitali hapo nadhani labda nilikuwa nimebakiza damu lita mbili tu nadhani, so jamaa hakuna wanachokifanya, manesi wananitizama tu, nikawa mkali, wakasema wewe mgonjwa unamfokea nani? Daah bongo, akaja muuguzi mmoja akanichoma sindano ya tetenasi na nyingine sijui ni nini, nikamwambia wewe bwana embu fanya kitu kuzuia damu basi, wakaanza kunizuia damu na wakafanikiwa lakini nadhani mpaka muda huo labda nilikua nna lita moja tu mwilini, nikaanza kuskia kabisa moyo unasukuma kitu kisicho kuwepo.

Lakini pale pale najiuliza ina maana nchi hii mtu anaweza kufariki kisa mguu, mkono na bega? how could that be possible? Ila nikajisemea "mimi sitokufa mahala hapa na wakati wangu bado haujafika, ewe Mungu wa haki usinichukue nikiwa katika umri huu nna deni na wewe", sasa Mungu ni muaminifu sana, baada ya kusema maneno hayo nikawa najipa moyo mkuu na imani na japo naskia sina damu na ata kuongea tu tabu, moyo una push kitu kisicho kuwepo, kazi yangu ikawa ni kurudia tu hayo maneno hapo juu, natamani labda nilale niamke nikiwa fresh ila hakuna kitu siwezi ata kusinzia au kuzimia.

Ile hospital ya wilaya wakasema hatuwezi kumtibu, mpelekeni hospital ile ya taifa, na mpaka muda huo hapo kwenye hio hospitali wamenichoma sindano mbili tu, drip ya maji na wakanipa rufaa kwenda kwenye ile hospitali nyingine baba lao.

Mpaka muda huo, wadau wangu washafika so ikabidi tutafute private ambulance sababu hio hospital wanasema ambulance ipo moja na imempeleka mgonjwa mmoja hospital ya taifa so tuisubirie na hapo tumesubiria saa na nusu haiji ndo kufanya maamuzi ya private ambulance.

Kufika kwenye ile hospital baba lao la taifa aisee kumbe bora kule wilayani ambako hawana kitu, wale wako too slow, yaani unawaona kabisa hakuna kitu kinachoweza kuwastua, wamezoea matatizo na kila mtu anapita tu ana shangaa shangaa hivi anaondoka, vijana wadogo ndo wajinga zaidi pale yaani wako sector ya emergence ila wanachezea tu simu ambazo ata ukiziangalia simu zenyewe ni tecno na samsung A series, hakuna humanity, samahani kwa kuyasema haya ila ndo nimeyaona tena emergence kabisa sasa fikiria kule kwengine ndo kupoje?

So wadau wangu wakaanza kutilia mkazo na mikwala mingi ndo na wale kuanza kunihudumia, na kila dakika hapo emergence wanaletwa watu ambao wanalia kila mtu kama anachinjwa hivi.

Sina damu na moyo unapambana sana kwa zaidi ya masaa matano sasa toka tukio litokee, naskia njaa naskia kiu na kama siwezi kupumua vizuri iv yaan nna fosi, ajab sizimii wala sisinzii, so hawa nao wakaniwekea drip za maji, nawaambia wazee nahitaji damu nitoleeni haya ma maji yenu hakuna kitu yanacho nisaidia hapa, wananiambia ngoja tukuchukue vipimo kwanza na tuone, basi wadau wangu waka fosi ki mjini mjini mambo yakaanza kukimbizwa na nini, mpaka naingia chumba cha upasuaji ni masaa 11 yamepita toka nipate ajali na damu kuniisha mwilini.

Basi baadae nikaingia wodini tena na nini, kuanza kupona sasa na nini ila expirience ambayo sio ya kuombea.

Namshukuru Mungu wangu alie mkuu sana, sikufa siku ile na sitarajii kufaa miaka hii hii na amenipa uhai na ataendelea kunipa uhai na tukio hili limeniweka karibu sana na yeye.

Kule wodini na tiba zingine unashangaa wataalam wanakwambia "aah kitu ichi hakiwi covered na bima ya nhif, aah hapa inabidi ulipe kiasi flani, aah kamuone flani" yaan unashangaa jambo dogo lina mlolongo mrefu ambao ni very unnecessary.

Wodini mule wadau wakaanza kunipa habari za namna watu wanavyoteseka na wengine ambao hua wanafia emergence, so scarry wazee. Bongo hauna kitu unaondoka unajiona wakuu, so hata kutafta room private nalo mpaka mchongo eti daah aisee.

Naomba kuishia hapo, nilitoka hospital sikumaliza hata siku saba, nilifosi nikaondoka kibishi tu na kuendelea na tiba tokea nyumbani kwangu na Mungu mwingi wa rehema na neema basi nimepona ndio niko narudi rudi na mimi kwenye majukumu yangu mengine, wale walionosababishia hayo matatizo ndo nataka kuanza kuwashughulikia sasa na sitokuwa na msamaha ktk hili. Lakini sitosahau miezi miwili iliyopita wazee nilikuwa kama niko Ukraine mstari wa mbele pale kumpinga bwana Putin asiendelee na majeshi yake kuichukua Kyiv.

Sijajua wewe umewahi kuyapata yapi au umewahi kuyaona yapi ya kuhusu ajali hizi za barabarani na experience za ma hospital yetu ambayo unaweza uka dead unajiona! Basi itakua vyema ukishare nasi basi tukapata la kujifunza.

Wasalaam.
Hyo namba ya ID yako ndo inakupa mikosi mkuu
 
Bila kitu kidogo pale taifa unaachwa hivihivi
Manesi wodini wana nyodoo,nlishuhudia anachambana na mgonjwa kisa mgonjwa mwingine
,mtu anakaa Analia emergency kuanzia asubuhii mpaka usiku.kama hana bima ndo kabisaa
Xray utapanga foleni asubuhi mpk SAA kumi ndo utapata.
Wale wanaowaacha wagonjwa wao walio katika hali mbaya sana wodini wajitafakari..wale wahudumu sio.
Kuna bibi alikua anabanwa kifua nadhani,anapiga mayowe...we dokta wee njoo.manesi wanajua anasumbua tu.najiuliza why hawampi attention maana ni mzee sana pia.basi alipiga kelele kama dakika kumi akaja dokta aliekua anamuhudumia siku nzima.ni mwanaume.
With smile anamsikiliza akagundua pumzi zinapotea,ndo manesi wakaanza kukimbizana huku na kule kusogeza mitungi,wanampush kifuani,mara wafunge pazia.but it was too late.wakamtoa na kumpeleka kwenye korido kafunikwa.
Nkajiuliza wangewahi so wangeokoa uhai wa huyu bibi.nusu saa wanampuuza?
It was sad.
Nimeshuhudia kwa macho yangu
 
Unachosema ni kweli, niliwahi peleka mtoto hospitali ya serikali kidokta kinachati huku kinaandika, na mtoto alikuwa anahema kwa shida.

Nikamuuliza dokta mbona unaandika hata mtoto hujamuangalia, akataka kumgusa bahati mbaya nina hasira sana nikabeba mtoto nikampeleka private.
 
Kwenye hospitali za serikali za wilaya hizi kuna vidokta vinesi nesi vidogo vidogo vina dharau kweli, na visimu vyao vya infinix.
 
Mkuu haulazimishwi kusoma.

Au mnataka stori kama za wale jamaa ambao wanaandika kidogo alaf wanakwambia tutaendelea kesho, kesho tena tutaendelea kesho, huo muda wengine sina na kama mtu anataka kusimulia basi asimulie mara moja yaishe sio kutuletea series hapo.
YanI bongo nyoko,yani umetoka kuzungumzia uvivu wa wabongo,na jamaa naye kaamua kuonyesha hapa practicaly.
 
Pole kwa madhira hayo yaliyokukuta!
In short kwa nchi yetu ugonjwa wenye uhakika wa kupona ni UTI ! A little complication unaaga dunia!
Pia gharama za matibabu ni kubwa nimewahi kuishi nchi moja ya kiafrika kwa kweli huduma zao za afya ni sawa na bure unalipa Sh. 50 kumuona na daktar na 250 kununua dawa (dawa aina yoyote) na dawa zinapatikana.kwa gharama hizi zinawavutia wananchi kuwahi mapema pind tu tatizo linapoanza na sio kusubiri hatua za mwisho. Thus why I don’t wonder why they have low mortality rate!
Nilishangaa kwenda muhimbili na kuambiwa kama hauna Bima kumuona daktari tu ni elfu 30 mbali na vipimo na dawa! How many can can afford ?
Nchi gani iyo bro please itaje
 
Bila kitu kidogo pale taifa unaachwa hivihivi
Manesi wodini wana nyodoo,nlishuhudia anachambana na mgonjwa kisa mgonjwa mwingine
,mtu anakaa Analia emergency kuanzia asubuhii mpaka usiku.kama hana bima ndo kabisaa
Xray utapanga foleni asubuhi mpk SAA kumi ndo utapata.
Wale wanaowaacha wagonjwa wao walio katika hali mbaya sana wodini wajitafakari..wale wahudumu sio.
Kuna bibi alikua anabanwa kifua nadhani,anapiga mayowe...we dokta wee njoo.manesi wanajua anasumbua tu.najiuliza why hawampi attention maana ni mzee sana pia.basi alipiga kelele kama dakika kumi akaja dokta aliekua anamuhudumia siku nzima.ni mwanaume.
With smile anamsikiliza akagundua pumzi zinapotea,ndo manesi wakaanza kukimbizana huku na kule kusogeza mitungi,wanampush kifuani,mara wafunge pazia.but it was too late.wakamtoa na kumpeleka kwenye korido kafunikwa.
Nkajiuliza wangewahi so wangeokoa uhai wa huyu bibi.nusu saa wanampuuza?
It was sad.
Nimeshuhudia kwa macho yangu
Sasa ni wangapi wanakufa kwa uzembe na ujinga kama huu kwa mwaka?
 
Kwenye hospitali za serikali za wilaya hizi kuna vidokta vinesi nesi vidogo vidogo vina dharau kweli, na visimu vyao vya infinix.
Hahahaaha kamoja kaliniambia boss kuna kifaa hapa cha kuvaa kwenye goti kinauzwa laki saba lete hela boss tukuchongee ili uwe unatembea fresh😂😂😂 daaah yaani ata uwezo wa kufikiria ni mdogo sana jamaa hao.
 
Unachosema ni kweli, niliwahi peleka mtoto hospitali ya serikali kidokta kinachati huku kinaandika, na mtoto alikuwa anahema kwa shida.

Nikamuuliza dokta mbona unaandika hata mtoto hujamuangalia, akataka kumgusa bahati mbaya nina hasira sana nikabeba mtoto nikampeleka private.
Ni wanafunzi wanatoka muhas nadhani.wanawekwa field kwenye ishu serious nadhani..
Au wale wa kujitolea.
 
Bila kitu kidogo pale taifa unaachwa hivihivi

Sasa ni wangapi wanakufa kwa uzembe na ujinga kama huu kwa mwaka?
Ndo hivo yani..ukimpa buku teni nesi mmoja analysing bulimia mpaka mwisho..
Yaani kwenye vipimo unapitishwa mbele unaingizwa wakati umewakuta wengine foleni.
Na staff wote wanayajua Yale maisha ndo mana hawafuatiliani.
Akifanya hivi kwa watu kumi kwa siku ana laki..si hela hiyo?
Mishahara yao duni..wanajiongeza kihivyo
So pale ukienda kinyonge kufata utaratibu utachoka..
Japo wanasaidia ila najiuliza maskini wanaishije kwa hali hii..mi ni kama bahati vihelahela vilikuepo upande wangu.

Na taasisi nyingi za serikali ziko hivi.
 
Kwema wadau?

Mwaka huu mwanzoni nikiwa nimetoka kusheherekea sikukuu ya mwaka mpya na nikiwa nimefanya maombi ya mipango yangu mingi kwa mwaka huu na kumsihi sana Mungu wangu aliye hai anijalie afya, uhai, furaha na amani tu mengine nayaweza hayanisumbui kabisa, basi sikuwa najua siku chache zijazo nitakutana na jambo baya na la kutisha kiasi icho.

Siku ya Tukio;

Nikiwa nawahi zangu kwenye majukumu yangu ya kikazi asubuhi kabisa hapa ndani ya Dar es Salaam tena nikiwa sina hofu wala kuwaza lolote, ile wazungu wanaita "the fear of unknown" kwamba kama kuna jambo baya linaenda kutokea basi kuna ishara flani huwa zinakusumbua kama kukosa amani and so, but mie siku hiyo haikuwa hivyo wala na nilikuwa nawaza tu niwahi kufika ofisini.

Ni asubuhi hio nikiwa ktk mwendo wa kawaida kabisa katika chombo private tu, ghafla kitu kikaniambia "be very careful" na nikaitii hii sauti so nikapunguza kabisa mwendo wa chombo changu na nikawa kawaida kabisa, haikupita hata dk 10 mbele yangu nikaona daladala mbili zinafukuzana kuwahiana abiria, kama kawaida yao hawa mabwana na ujinga wao wa kuwawahi abiria wa mbele zao, so hizi daladala hazikuwa upande wangu zilikuwa kulia kwanguwmie nikiwa kushoto so nilikuwa naziona face to face na nikajua kila mtu ni lazima aheshimu sheria za barabara na kukaa upande wake, sasa haikuwa hivi, yule dereva aliyekuwa anapitwa akafanya kumu overtake mwenzake nadhani bila kuangalia na labda atakuwa ni mjinga wa kuzaliwa wa kweli kweli, na ikumbukwe njia ilikuwa imenyooka so nimeanza kuwaona toka ka distance flani hivi mbele yangu wakifanya huo ujinga na haikuchukua hata dakika tatu tangu nianze kuwaona na kuniletea changamoto mbaya sana, yule dereva mwingine wa daladala alie overtake bila kuangalia nadhani ile gari ilimshinda au sijui kama shetani aliingilia kati ila nilishangaa tu kishindo kanigonga face to face wakuu, aisee nilishangaa sana lakini kuja kustuka naona damu zimejaa chini ya gari langu, airbag na watu wanapiga kelele, sikuzimia wala sikuskia maumivu ila nilikuwa kwenye mshtuko mkubwa sana sana.

Ile gari ilivyonigonga na ilizima pale pale yenyewe tu na kwangu huku sikuona tena ya mbele, nikawa najipapasa nikihofu yasije yakawa mambo ya uti wa mgongo kushtuka na kushindwa kuamka forever, nikajaribu kutikisha miguu naona mguu mmoja haurespond na kama bega linaniuma hivi, sikujua tena nini kimetokea ila mguu ulivunjika, bega kustuka na huu mguu uliovunjika ni tuseme ulikuwa umepasuka na ndo chanzo cha zile damu, na hii baadae nilikuja kujua ni kwamba nilikanyaga break kwa nguvu na kunyoosha mguu kwa kukaza labda kwa kustuka au hofu so gari ilivyopigwa kwa nguvu na kubonyea so presha yake na effect ndo ikaniletea hayo madhara.

Kilichofuata kuanzia hapo ikawa sina sauti tena, naona naamriwa tu vitu na wananchi waliokuwa wamejazana pale, kila mmoja akisema hivi na mwingine akisema vile na wangine wakirekodi kwa simu tukio lile na mie mwenyewe nikiwa bado nna mstuko mkubwa sana nawaza hivi ni mimi au naota? Nikiaskia sauti mkagueni vizuri labda ameumia kichwa?

Nikaskia shauri likiendeshwa juu yangu, wananchi wakasema tumpeleke polisi tukachukue PF3, wakaja kunitoa huku naona watu wameshika vichwa wakina mama wanalia na mie sasa nikaanza kuogopa uende nimeumia sana kuliko ambavyo najiwazia wakati huo, so najaribu kusimama mwenyewe siwezi, wananibeba na wanasema twende polisi, damu kila mahala na huo ni mguu tu, japo nna maumivu ya bega na mkono lakini najishangaa nasema kwa namna damu hizi zinavyotoka huko polisi ntafika nikiwa mzima kweli? Na kwa maeneo hayo kituo cha polisi kipo wapi sasa? Na je kutokea hapo mpaka kufika Hospitali itakuaje? Naona kabisa wananchi hawana elimu juu ya kuzuia damu kutoka na i feel like labda nijisaidie ila siwezi kufanya lolote, moyo unaenda speed sana na bado niko shocked tu.

Polisi hapakuwa mbali na hawakuwa na hiyana, ni kakituo ka dogo hakukuwa na jam ni walinihudumia ndani ya dakika 5 tu nikaipata pf3 tukaondoka na wananchi ambao walikuwa wamenibeba kwenye kirikuu.

So tukaelekea hospitali na hapa ntaomba nisitaje majina ya hospitali wananchi wasije wakaamua kwenda kuzichoma moto, so nikapelekwa hospital ya wilaya, mpaka nafika hospitali hapo nadhani labda nilikuwa nimebakiza damu lita mbili tu nadhani, so jamaa hakuna wanachokifanya, manesi wananitizama tu, nikawa mkali, wakasema wewe mgonjwa unamfokea nani? Daah bongo, akaja muuguzi mmoja akanichoma sindano ya tetenasi na nyingine sijui ni nini, nikamwambia wewe bwana embu fanya kitu kuzuia damu basi, wakaanza kunizuia damu na wakafanikiwa lakini nadhani mpaka muda huo labda nilikua nna lita moja tu mwilini, nikaanza kuskia kabisa moyo unasukuma kitu kisicho kuwepo.

Lakini pale pale najiuliza ina maana nchi hii mtu anaweza kufariki kisa mguu, mkono na bega? how could that be possible? Ila nikajisemea "mimi sitokufa mahala hapa na wakati wangu bado haujafika, ewe Mungu wa haki usinichukue nikiwa katika umri huu nna deni na wewe", sasa Mungu ni muaminifu sana, baada ya kusema maneno hayo nikawa najipa moyo mkuu na imani na japo naskia sina damu na ata kuongea tu tabu, moyo una push kitu kisicho kuwepo, kazi yangu ikawa ni kurudia tu hayo maneno hapo juu, natamani labda nilale niamke nikiwa fresh ila hakuna kitu siwezi ata kusinzia au kuzimia.

Ile hospital ya wilaya wakasema hatuwezi kumtibu, mpelekeni hospital ile ya taifa, na mpaka muda huo hapo kwenye hio hospitali wamenichoma sindano mbili tu, drip ya maji na wakanipa rufaa kwenda kwenye ile hospitali nyingine baba lao.

Mpaka muda huo, wadau wangu washafika so ikabidi tutafute private ambulance sababu hio hospital wanasema ambulance ipo moja na imempeleka mgonjwa mmoja hospital ya taifa so tuisubirie na hapo tumesubiria saa na nusu haiji ndo kufanya maamuzi ya private ambulance.

Kufika kwenye ile hospital baba lao la taifa aisee kumbe bora kule wilayani ambako hawana kitu, wale wako too slow, yaani unawaona kabisa hakuna kitu kinachoweza kuwastua, wamezoea matatizo na kila mtu anapita tu ana shangaa shangaa hivi anaondoka, vijana wadogo ndo wajinga zaidi pale yaani wako sector ya emergence ila wanachezea tu simu ambazo ata ukiziangalia simu zenyewe ni tecno na samsung A series, hakuna humanity, samahani kwa kuyasema haya ila ndo nimeyaona tena emergence kabisa sasa fikiria kule kwengine ndo kupoje?

So wadau wangu wakaanza kutilia mkazo na mikwala mingi ndo na wale kuanza kunihudumia, na kila dakika hapo emergence wanaletwa watu ambao wanalia kila mtu kama anachinjwa hivi.

Sina damu na moyo unapambana sana kwa zaidi ya masaa matano sasa toka tukio litokee, naskia njaa naskia kiu na kama siwezi kupumua vizuri iv yaan nna fosi, ajab sizimii wala sisinzii, so hawa nao wakaniwekea drip za maji, nawaambia wazee nahitaji damu nitoleeni haya ma maji yenu hakuna kitu yanacho nisaidia hapa, wananiambia ngoja tukuchukue vipimo kwanza na tuone, basi wadau wangu waka fosi ki mjini mjini mambo yakaanza kukimbizwa na nini, mpaka naingia chumba cha upasuaji ni masaa 11 yamepita toka nipate ajali na damu kuniisha mwilini.

Basi baadae nikaingia wodini tena na nini, kuanza kupona sasa na nini ila expirience ambayo sio ya kuombea.

Namshukuru Mungu wangu alie mkuu sana, sikufa siku ile na sitarajii kufaa miaka hii hii na amenipa uhai na ataendelea kunipa uhai na tukio hili limeniweka karibu sana na yeye.

Kule wodini na tiba zingine unashangaa wataalam wanakwambia "aah kitu ichi hakiwi covered na bima ya nhif, aah hapa inabidi ulipe kiasi flani, aah kamuone flani" yaan unashangaa jambo dogo lina mlolongo mrefu ambao ni very unnecessary.

Wodini mule wadau wakaanza kunipa habari za namna watu wanavyoteseka na wengine ambao hua wanafia emergence, so scarry wazee. Bongo hauna kitu unaondoka unajiona wakuu, so hata kutafta room private nalo mpaka mchongo eti daah aisee.

Naomba kuishia hapo, nilitoka hospital sikumaliza hata siku saba, nilifosi nikaondoka kibishi tu na kuendelea na tiba tokea nyumbani kwangu na Mungu mwingi wa rehema na neema basi nimepona ndio niko narudi rudi na mimi kwenye majukumu yangu mengine, wale walionosababishia hayo matatizo ndo nataka kuanza kuwashughulikia sasa na sitokuwa na msamaha ktk hili. Lakini sitosahau miezi miwili iliyopita wazee nilikuwa kama niko Ukraine mstari wa mbele pale kumpinga bwana Putin asiendelee na majeshi yake kuichukua Kyiv.

Sijajua wewe umewahi kuyapata yapi au umewahi kuyaona yapi ya kuhusu ajali hizi za barabarani na experience za ma hospital yetu ambayo unaweza uka dead unajiona! Basi itakua vyema ukishare nasi basi tukapata la kujifunza.

Wasalaam.
Pole sana kaka mkubwa naimani umeiona baraka ya Mungu na Neema zake, Sasa usiache kushukuru na kumtumikia kwa nafasi uliyonayo
 
Back
Top Bottom