Namna nilivyofunga ndoa kwa harusi nzuri na kubwa (ya ndoto yangu) bila kuchangisha wala kukopa

Niliudhuria sherehe ya bwana mmoja ( anafanya kazi TANAPA) , alifanya show yake Malaika Beach(Mwanza). Sikua mwanandugu wala jamaa ila taarifa za sherehe iyo ya ndoa niliipata jioni na kupewa kadi kuhudhuria shughuli iyo usiku. Katika sherehe iyo nilisikia majirani zangu kwenye meza yetu wakisema kuwa jamaa hajajukua hata mia mbovu ya mtu. MC alikua Masanja
Kha!kha!,eti mia ya mtu mbovu.
 
Mimi sina ela na katika harusi yangu nimepanga nitumie laki 5 Tu Kwa watu 20 nguo zote zitakodishwa Mimi na mke wangu wasaidizi nao ivyoivyo Kama ikiwa lazima Ila japo sioni ulazima siowi kumfurahisha mama wala Baba wala mjomba wala Bibi naowa kwaajili ya maisha yangu mwenyewe kama uyo. Mwanamke akikataa wala sitalazimaisha mapema snaa naachana naye
Mimi nimeshaweka cap ni watu 50 wengind watashuhudia mapicha mitandaoni

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Gharama nyingi zipo upande wa mwanamke, sherehe wanataka iwe kubwa na vile unataka mke huna budi kuchangia usije ukanyimwa mke.

Gharama kwa upande wa mume ni wakina mama ndo wanapenda kukuza jambo na kulifanya liwe kubwa huku gharama zikiteketea.

Pressure kubwa inayotoka kwa wanandugu na watu wa karibu inaongeza gharama.

Nina ndugu yangu mmoja alitumia pesa nyingi sana kwenye harusi yake baada ya mwaka ndoa imekufa. Huku bado madeni ya harusi hayajaisha, ndoa imedumu mwaka mmoja tu
Huwezi nyimwa mke wakati wameshakubali mahari

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Mwisho wa siku watu tunatofautiana sasa ukute familia yenu inachangia harusi na sherehe za watu mara kwa mara unawezaje kuwaambia wazazi wako eti sitaki michango wakati wao wanachanga na ww ni kijana wao pekee lazima sherehe yako inoge bwana maana ukitoka hapo sherehe nyingine utafanyiwa ukiwa ndani ya jeneza.

My future husband.. usidanganyike na haya .. yaani hutoeleweka. Sisi wahorombo hatunaga show mbovu wala ndogo
Usidanganyike.... kama hutaki changisha hakikisha una mfuko umenona..

Bia ziwepo, menu ziwepo, uviiri wa kutosha, henessy za wazee ziwepo etc. Kuhusu gari sijali sana hata tukapanda xt. Ila hapo ukumbini hapo.. we only live once... ni kwa furaha yangu na siyo kufurahisha dunia. Haitojirudia. Kukopa hatukopi ilaaa lazima tule gambe. Hv wakwe wako wasinywe bia kirahisi tu? Apaaa ndengaa
 
Mwisho wa siku watu tunatofautiana sasa ukute familia yenu inachangia harusi na sherehe za watu mara kwa mara unawezaje kuwaambia wazazi wako eti sitaki michango wakati wao wanachanga na ww ni kijana wao pekee lazima sherehe yako inoge bwana maana ukitoka hapo sherehe nyingine utafanyiwa ukiwa ndani ya jeneza.
Umemaliza. Na hiko ndo hufanya wazazi wagome. Kwetu mabinam wengi wamekua wakigomea lakini wapi. Halipiti. Yaan lazima watu wale na kunywaa. Kila mtu anataka high table wewee
Nilikua sitaki sherehe at first ila baada ya kujitathmini sana basi niseme tuu natakaka nataka nataka tena sherehe
 
Nami najipanga kimyakimya.
Nishatangaza nia na taratibu zinaendelea kimyakimya.

Kama watachanga ni sawa
Ila binafsi Naandaa 2 Million.
Inatosha kabisa, cha muhimu hakikisha mambo mengi unasimamia wewe na si kamati kubwaaaa, kamati yako iwe ndugu zako unaoona wana ubahili fulani
 
Umemaliza. Na hiko ndo hufanya wazazi wagome. Kwetu mabinam wengi wamekua wakigomea lakini wapi. Halipiti. Yaan lazima watu wale na kunywaa. Kila mtu anataka high table wewee
Nilikua sitaki sherehe at first ila baada ya kujitathmini sana basi niseme tuu natakaka nataka nataka tena sherehe
Watu wengi familia zao zimejitenga hazina ushirikiano ndio maana wanafanya sherehe kwakuogopa kuchangisha ila kama familia ina watu michango lazima na sherehe lazimaa
 
Inatosha kabisa, cha muhimu hakikisha mambo mengi unasimamia wewe na si kamati kubwaaaa, kamati yako iwe ndugu zako unaoona wana ubahili fulani
Sawa mkuu.
Ila hapo umesema mambo mengi nisimamie mm. Sasa nikisimamia mm si kamati itaonekana naingilia majukum yao?

Fafanua hapo mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom