Namna mtu anavyo hack WIFI, nahisi kuna mtu anatumia kifurushi changu

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
Nimekuwa nikijiuliza swali hili kwa muda maana ninahisi kabisa kuna mtu ananifanyia uhuni huo. Data zangu zinaisha haraka sana, mimi hutumia simu ku connect kwenye laptop kupitia wifi. juzi nlipigwa na butwa jinsi ambavyo 1.5 GB zimeisha huku nikiwa sijadownload kitu chochote. Natumia mtandao wa Airtel na jambo hili si mara moja, mara kadhaa limekuwa likitokea hasa weekends.

Naanza kuhisi kuwa pengine kuna mtu anahack wireless yangu na kutumia ingawa ninatumia password. Otherwise ni nini kinachofanyika? Wadau naomba mnisadie katika hili. Ikiwezekana hata mimi niaze kuwa sasa nashare bundle yake. Maana kama yeye kaamua kuwa anashare yangu bila idhini yangu basi ijulikane moja tu kuwa tumeanzisha ushirika.
 
inawezekana pc yako huwa ina install automatic updates, au setting za synconsize sizo on kwenye smu yako zinakulaa data...
Hili ndilo linalowezekana pengine ungetuambia na security method ambayo WiFi yake anaitumia, tethering wireless kwenye simu huwa inaonyesha idadi ya device iliyounganishwa na na hiyo kwa hiyo angalia hapo hizo device vinginevyo pia unaweza kuset maximum namba ya device kuunganishwa na hiyo wifi yako na ukaweka 1.
 
ok . nashindwa kuelewa sasa tatizo litakuwa ni nini why bundle inaisha kwa kasi ya ajabu na sijadownload anything. maybe pia naomba niwasiliane na huyo friend of yours anielekeze wanafanyaje ku hack then nijue kama kuna jamaa ananifanyia huo mchezo maeneo ya home.

Mimi kwa uwelewa wangu mdogo wifi inaweza kuwa hacked lakini sio rahisi kama tunavyoona na kwa hali ya kawaida its not worth it...kuna rafiki yangu alihack wifi ya sehemu alitumia karibia siku nzima kuhack tena nakumbuka alitumia ubuntu os na security ya ile wifi wpa1
 
Disable automatic window update, Update firmware, Change username kwenye hiyo wifi na password. Password jaribu kutengeneza strong password in case of Upper and Lower case plus numbers Then wakati una set recommend one user na uwe una allow watumiaji wengine, tatizo litakwisha ili waweze ku access internet connection.
 
Hiyo Wi-Fi unatumia device gani kuirusha simu au moderms?

Kama simu ya Android unaweza kuona connected devices ili kudisable zingine zisizokuhusu
 
Nimekuwa nikijiuliza swali hili kwa muda maana ninahisi kabisa kuna mtu ananifanyia uhuni huo. Data zangu zinaisha haraka sana, mimi hutumia simu ku connect kwenye laptop kupitia wifi. juzi nlipigwa na butwa jinsi ambavyo 1.5 GB zimeisha huku nikiwa sijadownload kitu chochote. Natumia mtandao wa Airtel na jambo hili si mara moja, mara kadhaa limekuwa likitokea hasa weekends.

Naanza kuhisi kuwa pengine kuna mtu anahack wireless yangu na kutumia ingawa ninatumia password. Otherwise ni nini kinachofanyika? Wadau naomba mnisadie katika hili. Ikiwezekana hata mimi niaze kuwa sasa nashare bundle yake. Maana kama yeye kaamua kuwa anashare yangu bila idhini yangu basi ijulikane moja tu kuwa tumeanzisha ushirika.
Kama uliwahi kushare na mtu na unakua nae karibu, Siku akiwasha device yake Ina connect automatically kama pia WI Fi yako ipo ON
 
Back
Top Bottom